Panzi Mchanga
Senior Member
- Jul 31, 2015
- 127
- 133
Huyu Jacob ni Meya bahaluli, anazalilisha hii nafasi sana
Ni kweli kabisa.
Meya anatakiwa awe na uwezo wa kuwasiliana na jamii na kuihifadhi hadhi ya ofisi yake. Public statement kama hii inasomwa na watu wengi sana. Ndani na nje ya nchi. Huyo aliyetajwa hapo kama DAUDI ALBERT BASHITE ni nani? Mwandishi akitaka kumtafuta kumhoji (wa kutoka Malawi kwa nfano), atampata kumuuulize maswali?. Huyo aliyetajwa anaweza kuwajibishwa? Mkifungua malalamiko mtamwita nani? Mimi sina shida na jina la mtaa provided taratibu zimefuatwa. Majina ya mtaa yana sababu zake za kuwa kama jina lilivyo.
Kuna kitu Mungu ameepusha hii nchi. Pengine huyu Meya angekuwa ndio Waziri wa fedha!
Mimi nafikiri agenda kuu siyo hiyo nia ya kuupa jina huo mataa. Agenda ni hizi:
- Hii michezo inaandaliwa kati ya Cloud na wapinzani. Wana predict exactly reaction itakuwaje na wanafanya simulation ya namna ya ku-respond kwa ajili ya kufikia lengo-publicity.
- Hili lilikuwa ni dili na pale ilikuwa kusafisha hewa. Baada ya hapo watu wangepewa tenda ya kutengeneza vibao ubungo nzima.
Nadhani angewauliza wana mtaa kero yao isingekuwa makibao hayo. Dr Slaa wakati akiwa mbunge kule Karatu, halmashauri ilikuwa role model. Jiji la Dar chini ya upinzani ni shida tu. Ushuru wa parking ni shida. Mpaka kwenye madimbwi wanakusanya. Hakuna maboresho yoyote; barabara za mtaa ni mbaya kuliko wakati mwingine wowote.
Meya apange shuhuli zake kwa nia ya kuwasadia wananchi.