Meya Ubungo: RC amelazimisha bango la mtaa wa Wanyama kuondolewa, kisa waliomleta ni Clouds Media

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,706
2,000
image.jpeg


UFAFANUZI

1.Huyo aliyeshika bango lililozinduliwa jana na VICTOR WANYAMA kama jina la mtaa, Anaitwa ISIAKA WAZIRI ni mtendaji kata UBUNGO

2.kweli wameling'oa leo asubuhi baada ya mtendaji kata kupokea maagizo kutoka kwa Mkurugenzi wa ubungo baada ya kuamrishwa na DAUDI ALBERT BASHITE waliondoe kuhakiki kama vigezo vya kupendekeza jina la mtaa vilifuatwa.

3.Bango limerudishwa ofisi za kata ubungo na kama wataona litarudishwa kwa nguvu wameshauriwa na DAUDI ALBERT BASHITE wakaliache central mpaka taratibu za kuhakiki ziishe.

4.Ni kweli jambo hili litailetea Nchi aibu sababu hata mgeni wetu Victor Wanyama anaweza kuona siasa za chuki za kuangalia "nani kafanya" na si "nini kimefanywa"

5.Ni kweli Hasira za DAUDI ALBERT BASHITE,dhidi ya clouds media waliofanikisha kufika kwa VICTOR WANYAMA,ndiyo imepelekea kukomoa kwa kuliondoa bango lenyewe.

6.Ni sahihi kuwa CCM imewauma sana ndiyo maana tangu jana walitaka kupindisha ukweli kwa kivuli cha *UZALENDO" Lakini leo baada ya kujua kuwa na MBWANA SAMATA aliandaliwa barabara, wametumia WA NEC wa CCM waliopo serikalini kuharibu tukio kama viongozi (Halmashauri ya manispaa Ubungo)

7.kuhusu afisa habari wa manispaa aliyetumwa kukanusha na kusema taratibu zilikiukwa,sina hakika kama akilini yupo sawa,sababu naona DAUDI ALBERT BASHITE emelazimisha aonekane kwamba kwenye mchakato huo wakutoa jina la mtaa alipaswa kuwemo si kweli kwasababu mimi nimeweka sheria aisemi DC au RC anahusika bali ni halmashauri tuh asilazimishe kuingia kwenye sherehe isiyo mhusu. Mimi naweka sheria hapa na Mkuu wa mkoa aweke inayompa mamalaka ya kushirikishwa.

Sheria namba 8 ya mwaka 1982 (sura namba 288) na sheria namba 6 ya mwaka 1999 ,ndiyo inayotoa mamlaka kwa serikali za mitaa kutunga na kutoa majina ya barabara za ndani ya halmashauri na barabara za mitaani.

*Soma sheria namba 8 ya mwaka 1982(sasa inaitwa sura 288) kifungu cha 55(1)j-to name or re name,where necessary,all streets(such names to be affixed in conspicuous places),and to cause the buildings in such streets to be numbered;*

Na
BONIFACE JACOB
MSTAHIKI MEYA
HALMASHAURI YA UBUNGO

senior councilor.

======

Hatua hii imekuja baada ya Victor Wanyama kukabidhiwa Mtaa. Zaidi soma=>Mcheza Mpira Victor Wanyama, apewa jina la mtaa jiji Dar, Meya atoa ufafanuzi
 

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,210
2,000
Ingekuwa raha sana kama mikwaruzano hiyo ingekuwa kwenye VIWANDA vya UBUNGO au Mambo ya Maana.
Meya Boresha ubunifu utakaokupa Kiki ya Kudumu.

Ni sawa na MESSI kufunga hat-trick kwenye ligi ya kombe Mbuzi wakati La-liga anashindwa kutoa hata pasi.
Nguvu na ugomvi upelekwe kwenye mambo ya msingi
 

Allen Theonest

JF-Expert Member
Jun 18, 2017
400
500
Ingekuwa raha sana kama mikwaruzano hiyo ingekuwa kwenye VIWANDA vya UBUNGO au Mambo ya Maana.
Meya Boresha ubunifu utakaokupa Kiki ya Kudumu.

Ni sawa na MESSI kufunga hat-trick kwenye ligi ya kombe Mbuzi wakati La-liga anashindwa kutoa hata pasi.
Nguvu na ugomvi upelekwe kwenye mambo ya msingi
Ikiwa jambo dogo kama hilo la bango linawatoa nyongo, kikijengwa kiwanda huko ubungo si mtakufa kwa pressure kabisa
 

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,210
2,000
Ikiwa jambo dogo kama hilo la bango linawatoa nyongo, kikijengwa kiwanda huko ubungo si mtakufa kwa pressure kabisa
kama umekiri ni dogo basi limefanywa kwa fikra ndogo (ingawa huyo jamaa huwa namkubali kwa kukomaa), naona wahusika waliamua kumfuata hukohuko kwa level alizojiweka...
 

offg76

JF-Expert Member
Dec 3, 2016
368
500
Kama mna anzisha mambo ya msingi ndani ya mkoa, kwanini mkuu wa mkoa huo ambae ndo kiongozi mkuu katika mkoa wake msimjulishe? Kwani kuna ubaya gani mkimjulisha mkakati wenu wowote kwa manufaa ya mkoa wenu?

Lazima tufuate chain of command, vinginevyo tutabaki kulaumiana bure, bashite amehisi kudharaulika.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom