Meya Ubungo atuma salamu za rambirambi Uingereza

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,471
2,000
Jacob.jpg

Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amesema Halmashauri yake inaungana na Manispaa ya London, Uingereza kuomboleza vifo vilivyotokea katika tukio la moto kwenye Jengo la Grenfell Tower.

Tukio hilo lilitokea Juni 13 mwaka huu na Kamanda wa Polisi, Stuart Cundy alisema idadi ya watu 58 wanakadiriwa kufariki dunia katika jengo hilo lililokuwa na watu wapatao 600.

Jacob ambaye pia ni diwani wa Ubungo (Chadema), alisema hayo jana wakati wa salamu zake kwa Meya wa London, Sadiq Aman Khan alizoziwasilisha kupitia kwa Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke.

Kwa niaba ya Manispaa ya Ubungo, natuma salamu za rambirambi kwa Balozi wa Uingereza ambaye atafikisha ujumbe huo kwa meya Khan.

“Tunawapa pole sana wafiwa na majeruhi na famila zilizofikwa na janga hili,” alisema Jacob ambaye pia ni Mjumbe Kamati Kuu ya Chadema.

Katika salamu hizo, Jacob alisisitiza kuwa Manispaa ya Ubungo inaungana na Uingereza kwa ajili ya kuombeleza vifo hivyo na kumuomba Mungu aziweke mahali pema peponi roho za marehemu sanjari na kuwaombea majeruhi wapate ahueni haraka.

Chanzo: Mwananchi
 

Duduwasha

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
5,713
2,000
Duh hata kutoa pole wengine wanaona mtu anatafuta kiki? Sikuhizi hatupo sawa na umoja umeisha. Full ubaguzi
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
23,313
2,000
Huyu jamaa anapenda sifa sana, naamini ndio anaongoza kwa kuleta image mbaya ya CDM Dsm.
Hugo meya Hakutoa salamu za Pole kwa familia za wananchi na polisi waliouawa na magaidi kibiti na mkuranga anakurupukia kutoa nje ya Nchi kichwa chake huyu anajijua mwenyewe
 

okaoni

JF-Expert Member
Jun 25, 2011
1,396
2,000
Anatuma rambirambi uingereza halafu zipo kwenye magazeti ya bongo kiswahili. Tukio linatokea majuu rambirambi inasambaa bongo
 

exaud morrey

JF-Expert Member
May 22, 2017
332
250
Hugo meya Hakutoa salamu za Pole kwa familia za wananchi na polisi waliouawa na magaidi kibiti na mkuranga anakurupukia kutoa nje ya Nchi kichwa chake huyu anajijua mwenyewe
Huwezi kumpangia mtu atoe wapi vilevile angetoa mbona ingeishia serikalini
 

mikeimani

JF-Expert Member
Jun 20, 2015
2,702
2,000
Congo wanauliwa kila kukicha sijawahi kumsikia akiwatembelea, achilia mbali kuwatumia salami za rambirambi

Au majirani zake wakongo sio watu ?
 

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,725
2,000
Hugo meya Hakutoa salamu za Pole kwa familia za wananchi na polisi waliouawa na magaidi kibiti na mkuranga anakurupukia kutoa nje ya Nchi kichwa chake huyu anajijua mwenyewe
Wewe ulitoa pole huko Rufiji na Mkuranga? je unaweza kutuambia ni kiongozi gani wa juu wa Serikali aliyeweza kutoa pole kwa wananchi wa Rufiji na Mkuranga wanaouawa? Pole ilitolewa tu kwa vifo vya wale polisi lakini kwa wananchi sijawahi sikia. Hapo Meya ameamua kuonyesha mfano nini kama binadamu tuliostaarabika tunatakiwa kufanya kwa nchi nyingine.
 

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,725
2,000
Congo wanauliwa kila kukicha sijawahi kumsikia akiwatembelea, achilia mbali kuwatumia salami za rambirambi

Au majirani zake wakongo sio watu ?
Ni vema ukaelewa hasa nini maana ya kutokea kwa janga ukiisha elewa hautaendelea na upuuzi uliouandika.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom