Meya: RC Gambo hataki nipeleke rambirambi kwa wafiwa, hajaweka kamati, anaagiza Mil 50 za rambirambi

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Meya wa Jiji la Arusha Mjini Kalisti Lazaro anaongea na waandishi wa habari muda huu.

'RC Gambo hataki nipeleke rambirambi kwa wafiwa, hajaweka kamati, anaagiza Mil 50 za Lucky Vicent zipelekwe Mt. Meru kwanini?

Meya Arusha Kalisti Lazaro amesema rambirambi ambazo zitapitia ofisni kwake hatazipokea atawaelekeza wanaotoa kwa wafiwa na sio kwake.


===========
Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro amesema kuwa ataelekeza fedha zote za rambirambi kwa wafiwa badala ya kuzipeleka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Aidha amehoji ni kwanini fedha za rambirambi zilizochangwa kwaajili ya msiba wa wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja kuchotwa Sh.milioni 1.5 kupelekwa kama rambirambi katika msiba wa bwana na bibi harusi waliosombwa na maji Kata ya Sambasha iliyopo Wilayani Arumeru kama pole.

Meya, Lazaro aliyasema hayo leo Jijini hapa wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuachiliwa na Jeshi la Polisi leo majira ya saa 12:30 asubuhi kisha kwenda ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini.

Amesema fedha hizo za rambirambi zitakazochangwa na watu mbalimbali kisha kuletwa kwake kama Meya wa Jiji la Arusha, atazielekeza kwa wafiwa moja kwa moja badala ya kwa RC Gambo kwani RC huyo anaonekana kutumia fedha hizo kwa malengo mengine na kumtuhumu kuwa anachukua fedha zinazochangwa na kupeleka kwenye misiba ambayo ilitokea kipindi cha nyuma kama rambirambi.

Amesema wafiwa wanahoji ni kwanini fedha zilizobaki zilazimishwe kujenga jengo la Wagonjwa Mahututi (ICU) Sh,milioni 56 huku akijua kabisa fedha hizo zimechangwa kwaajili ya rambirambi kwa wafiwa.

“Yani hili jambo ni la ajabu sana nimefika shuleni kutoa rambirambi na si mimi bali nimewasindikiza umoja wa shule binafsi na nikaomba viongozi wa dini wafanye sala kwaajili ya kuanza kutoa fedha hizo lakini cha ajabu nakamatwa kwa kosa gani na mimi nasema sitaelekeza fedha kwa RC Gambo ambazo ni za rambirambi bali zikija kupitia ofisi yangu nitazielekeza kwa wafiwa ambao wapo kwenye kila Kata,” alisema

Naye Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alisema tukio lile ni tukio la aibu na wakati Fulani walimshauri RC Gambo awe mtu mzima akiendelea na mambo haya hatafika mbali.
 
Cheap politics,
Walishazoea siasa za chuki na kuvizia vizia wanataka kugeuza msiba kua siasa.
Waache uhuni kama walivyo fanya kwa Kamanda mawazo ahadi Nyingi afu mpaka Leo hakuna hata moja ama walivyo ahidi kwenye msiba wa Chacha wangwe ama,

Uhuni wa vyama vya Upinzani huo, Meya na Mbunge wao ni viongozi afanye kuwatumikia wananchi watamuelewa kwa kazi anayofanya sio kwa usanii huo
 
Viongozi wa upinzani wana laana ya kupenda pesa zisizo zao.

Wamezidi sasa

Uamuzi mzuri kama ni kusaidia hospitali ya mkoani hapo.
 
Meya wa Jiji la Arusha Mjini Kalisti Lazaro anaongea na waandishi wa habari muda huu.
'RC Gambo hataki nipeleke rambirambi kwa wafiwa, hajaweka kamati, anaagiza Mil 50 za Lucky Vicent zipelekwe Mt. Meru kwanini'>>> Meya Arusha Kalisti Lazaro'
Yeye Meya na Chadema ndio wapigaji, kama utaratibu wote wa mazishi na msiba umeratibiwa na ofisi ya mkuu wa mkoa iweje na yeye akusanye kivyake michango ipitie kwake??
Ivi uyo Meya ni mkubwa kuliko Bunge ama watanzanie wengine wote ambao wamepitisha michango yao kwa mkuu wa mkoa??
Aache Ujinga na yeye uyo Meya
 
Enzi za Mfalme Suleiman,ili uwe Mfalme mwenye nguvu,utawale kwa amani na uwe na eneo kubwa la utawala iwe kwa kuteka au kwa hiyari.ilihitaji uwe na watumwa wengi,wapagazi wengi,jeshi kubwa la farasi (vifaru vya kale) na utajiri wa mifugo kama ngamia na kondoo.

Ukimiliki haya yote,na hasa jeshi la Farasi na Mifugo,basi wewe ulikuwa ni Mfalme mkuu,bingwa na mkalia kiti cha ufalme bila presha na taharuki.Haya yote ndio yalikuwa ishara ya ufalme wenye nguvu.

Wakati Mungu wa Suleiman,amemtaka Mfalme Suleiman ataje chochote ambacho angataka kukipata ili aweze kutawala vizuri.Mfalme Suleiman alimwambia Mungu wake "EEE BWANA UNIPE HEKIMA ILI NIWATAWALE WATU WANGU KWA HAKI,MAANA TUNDA LA HAKI NI AMANI NA UPENDO"

Mfalme Suleiman alikuwa na nafasi ya kuomba apewe jeshi kubwa la farasi,alikuwa na nafasi ya kupewa nguvu za kijeshi ili awatawale watu wake kwa mabavu na kijeshi,Lakini Mfalme aliomba kitu kimoja tu...Nayo ni HEKIMA.Sasa ndio naelewa,kwanini mfalme Suleiman aliamua kuomba HEKIMA dhidi ya Jeshi kubwa la farasi na Utajili.

HEKIMA ni msingi wa uongozi,Hekima hutenda kwa HAKI...Haki huleta amani,haki huinua Taifa.Tunda la Haki ni Amani na Upendo.
 
Back
Top Bottom