Meya Raibu: Kwa mazoezi nilioyaona leo, wanaotaka kuandamana nawashauri waache mara moja

Jul 19, 2020
39
128
Mgeni maalumu Mstahiki Meya wa Moshi Juma Raibu akiongea katika hafla ya Jeshi la polisi ya kuwapandisha vyeo askari wake katika ngazi za staff sajenti,sajenti na koplo amewataka wanaopanga kufanya maandamano kuacha mara moja kwa sababu maandamano hayo sio halali na jeshi la polisi aliloliona katika mazoezi kwenye hafla hiyo halina mchezo na wahalifu wanaopanga kuifanya nchi isitawalike.

Meya Raibu aliendelea amewahasa maafisa hao wa Polisi kuwa nanukuu

"Najua mmpepata vyeo hivi sio mapambo bali mkavitumikie kwa kusimamia ueledi kwa sababu wananchi wengi wanawategemea kama msaada wao na daraja la matatizo yao ya kijinai, uaminifu ukweli na uwajibikaji, lakini pia wapo baadhi ya askari wanageuza kesi za madai kuwa jinai acheni hii"
Pia Meya huyo alimpongeza mgeni rasmi ndugu kadio kwa kazi njema ndani ya wizara hiyo akisaidiana na Mhe Waziri simbachawene na IGP Sirro.

Meya huyo alimaliza kwa kusema "Tuendelee kumuunga mkono Mhe Rais Samia Suluhu hasani kwa uchapakazi bora, na nimpongeze mhe Rais kwa kuwapandisha vyeo askari wa Polisi zaidi ya elfu 23, na zaidi ya elfu 40 wa vyombo vingine vya dola" Mwisho wa kunukuu.

Mgeni rasmi katika hafla alikuwa Chrtopher kadio katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani akiambatana na Kamishina wa polisi na Mwakilishi wa IGP ndugu wakulyamba.View attachment 1893628
IMG-20210815-WA0003.jpg
View attachment 1893625View attachment 1893626View attachment 1893627
 
... kilichobaki sasa ni vitisho na matumizi ya mabavu hata kwa wanaotaka ku-exercise haki zao za kikatiba au sio?
 
Back
Top Bottom