Meya Raibu: Hakuna Corona Moshi, Haya ni Mashambulizi dhidi ya Uchumi wetu

Jul 19, 2020
20
75
Akihojiwa na Kituo cha Nungwi online Fm Mstahiki Meya Wa Manispaa Ya Moshi Juma Raibu amekanusha vikali uwepo Wa Mgonjwa wa corona katika manispaa hiyo.

Hii inakuja ikiwa ni Masaa machache Tu toka Shule ya ISM kutangaza kufunga shule hiyo baada ya Mwanafunzi Mmoja kukutwa na Viashiria vya corona

Meya Raibu amesema tayari amewaelekeza Wasaidizi wake wafuatilie shule hiyo ili kuchukua hatua stahiki kwani Mwenye mamlaka ya Kupima na kutangaza Juu ya Ugonjwa huo ni Waziri Mkuu wa Nchi na sio Vinginevyo.

Meya Raibu Pia amesema Kesho Litatoka tamko Rasmi la serikali juu ya Taharuki hiyo ambayo ameifananisha na Vita vya uchumi dhidi ya Mkoa wa Kilimanjaro hasa katika nyanja ya utalii.

All - Rounder

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
2,670
2,000
Kuna mambo makubwa mawili tu ukubali kuwa nawe sasa CORONA imeshaanza kukuinga na kushambulia Watu wako ili uanze kupata Misaada kirahisi hasa ya Chanjo ambazo kwa bahati nzuri sasa zipo za aina Tatu, au Ukanushe kuwa CORONA haipo ili ujizolee Sifa za Kisiasa na Kimataifa lakini huku chini Watu wako wanakufa kila Uchao na kutoa Amri kuwa anayekufa kwa COVID-19 basi Familia iambiwe tu kuwa ni Pneumonia hiyo.
 
mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
8,932
2,000
Kuna mambo makubwa mawili tu ukubali kuwa nawe sasa CORONA imeshaanza Kukuinga na Kushambulia Watu wako ili uanze kupata Misaada kirahisi hasa ya Chanjo ambazo kwa bahati nzuri sasa zipo za aina Tatu, au Ukanushe kuwa CORONA haipo ili ujizolee Sifa za Kisiasa na Kimataifa lakini huku chini Watu wako wanakufa kila Uchao na kutoa Amri kuwa anayekufa kwa COVID-19 basi Familia iambiwe tu kuwa ni Pneumonia hiyo.
Miaka yote tangu kuumbwa dunia watu wanakufa. Wizara ilihimiza kuwa kila mwenye dalili apimwe, na wanaopimwa Corona majibu yatoke kwa haraka.

Swali kwetu sisi, ni je kwanini kila anayekufa Leo iambiwe ni corona?
 
Aladeen04

JF-Expert Member
Sep 6, 2016
1,970
2,000
Kuna mambo makubwa mawili tu ukubali kuwa nawe sasa CORONA imeshaanza Kukuinga na Kushambulia Watu wako ili uanze kupata Misaada kirahisi hasa ya Chanjo ambazo kwa bahati nzuri sasa zipo za aina Tatu, au Ukanushe kuwa CORONA haipo ili ujizolee Sifa za Kisiasa na Kimataifa lakini huku chini Watu wako wanakufa kila Uchao na kutoa Amri kuwa anayekufa kwa COVID-19 basi Familia iambiwe tu kuwa ni Pneumonia hiyo.
Hivi Pneumonia inaweza kuibuka ghafla tu kwa mtu ambaye hana historia ya huo ugonjwa?
 
All - Rounder

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
2,670
2,000
Miaka yote tangu kuumbwa dunia watu wanakufa.... Wizara ilihimiza kuwa kila mwenye dalili apimwe, na wanaopimwa Corona majibu yatoke kwa haraka.

Swali kwetu sisi, ni je kwanini kila anayekufa Leo iambiwe ni corona ???
Na kwanini Wote wanaokufa na CORONA katika Taifa lako la Madafu Madaktari wameagizwa wawe wanasema kuwa kutokana na Pneumonia tu?
 
UHURU JR

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
9,809
2,000
Kuna mambo makubwa mawili tu ukubali kuwa nawe sasa CORONA imeshaanza Kukuinga na Kushambulia Watu wako ili uanze kupata Misaada kirahisi hasa ya Chanjo ambazo kwa bahati nzuri sasa zipo za aina Tatu, au Ukanushe kuwa CORONA haipo ili ujizolee Sifa za Kisiasa na Kimataifa lakini huku chini Watu wako wanakufa kila Uchao na kutoa Amri kuwa anayekufa kwa COVID-19 basi Familia iambiwe tu kuwa ni Pneumonia hiyo.
Hivi hao wauguzi siku hizi hawaogopi corona kiasi cha kuwakimbia wagonjwa wa corona kama ilivyokuwa mwanzo?

Halafu kwahiyo baada ya mtu kufa kwa corona na kusingizia pneumonia wanawapa ndugu mwili wa marehemu aliyekufa kwa corona wakauzike kwa mazishi ya kawaida bila kujali?
 
Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
6,493
2,000
Christmass na Mwaka mpya nilikuwa Kilimanjaro kujifunza maisha ya wachaga, na katika pita pita zangu nilifika mpaka hospitali moja kubwa ya rufaa iliyopo Moshi (nakwepa kuweka jina la hiyo hospitali hapa) na niliona mambo makubwa matatu.
1. Huwezi kuingia hapo hospitali bila kuvaa barakoa. (Ni lazima, na kuna mgambo mkali wa kusimamia hilo)

2. Lazima utakase mikono getini kabla ya kuingia ndani ya Hospitali.

3. Kuna wodi maalum ya wagonjwa wa Corona na ilikuwa imejaa wagonjwa!
 
mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
8,932
2,000
Christmass na Mwaka mpya nilikuwa Kilimanjaro kujifunza maisha ya wachaga, na katika pita pita zangu nilifika mpaka hospitali moja kubwa ya rufaa iliyopo Moshi (nakwepa kuweka jina la hiyo hospitali hapa) na niliona mambo makubwa matatu....
Wanachukua tahadhari safi sana
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom