Meya Raibu awakonga nyoyo wawekezaji, KCBL wamwaga Mikopo ya Bajaji na Pikipiki Moshi

Feb 7, 2019
41
45
KCBL YASHUSHA NEEMA YA MIKOPO YA BODABODA NA BAJAJI MOSHI, MEYA RAIBU ATEMA CHECHE

Na Mwandishi Wetu, Moshi Kilimanjaro


Benki ya KCBL imetambulisha rasmi huduma yake kabambe ya kuwakopesha Wajasiriamali na Wananchi wa Manispaa ya moshi mikopo ya vyombo vya Moto vya pikipiki na bajaji.

Akizindua huduma hiyo Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo ndugu Juma Raibu amewataka Vijana na Wananchi wa Moshi Kuendelea Kuunga Mkono Ushirika na Benki hiyo ya KCBL Katika Ukopaji Na Kufungua akaunti mbalimbali ikiwemo Fixed Deposits.

"Benk Hii ni Mali Yetu Na Heshima Kwetu wanaushirika na Wananchi kwa Ujumla hata Mimi Ni Mwanahisa Wa Benki Hii Nawaomba Sana Kufungua Akaunti na Kupata Huduma Benk Hii Kwani inasaidia Wanyonge Na Wanaojiweza Pia Tuwaunge Mkono Katika huduma Zote za Benk hii ya Ushirika"

Mstahiki Meya Manispaa ya alizindua Mkopo wa Bajaji ambao Kijana Wa Kwanza Kununua Bajaj Hizo Ni Baraka Kaale Akifatiwa Na Neema Mwingira Ambaye Nae Alikopeshwa Bajaji mpya Aina Ya TVS kwa TShs 2,500,000 za Kitanzania Na Wao Benk Kutoa Sh 5,100,000

Pia Meya Raibu aliwaasa Wakopaji na Wateja na Wafanyakazi wa benki Hiyo Kuwa Waaminifu,Waadilifu, wakweli na Wanyenyekuvu Na Wenye Weledi Katika kajukumu Yao.

Kwa upande wake Meneja Wa biashara wa Benki Ya KCBL Ndg Muba Alisema Juma Raibu Ni Mdau Muhimu Sana Wa Benki Yetu Kuachia mbali Kuwa Mwanahisa

"Mh Tunajua uwezo wako Nguvu Zako Katika kutetea Wananchi Ndio Maana Hatujasita Kukuita Kutuzindulia Mradi Huu Tukuhakikishie Tutafata yote Ulioelekeza kama Ulivotukubalia Kukopesha Watumishi Wako"

Wasalaam.
View attachment 1816396View attachment 1816398View attachment 1816399
 
Huyu Meya si ndiyo alikwapua pesa za hii benki TAKUKURU wakamuamuru azirudishe bado hawajakoma wanamkaribisha tena!
 
Back
Top Bottom