Meya Moshi awakabidhi wazabuni wanane kwa TAKUKURU

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,230
2,000
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi, Juma Raibu ameagiza kukamtwa kwa wazabuni wanane wanaodaiwa kula fedha za Halmashauri zaidi ya Sh47 milioni pamoja na viongozi wa vikundi 45 vya asasi za kuweka na kukopa (Vicoba).

Viongozi hao wanadaiwa kuwa wameshindwa kurejesha zaidi ya Sh94 milioni walizokopa tangu mwaka 2015.

Raibu ametoa agizo hilo leo, Machi 31,2021 alipowaita viongozi hao ofisini kwake kutaka kujua hatma ya fedha hizo ambazo walikopewa na Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.

"Wote hapa niliowaita mmehujumu fedha za serikali, hili jambo linakera sana haiwezekani tangu mwaka 2015 mpaka leo hamjarejesha fedha hizi mnazodaiwa na Halmashauri zaidi ya Sh94 milioni, hili halikubaliki nawakabidhi leo mikononi mwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mtuambie mnarejeshaje fedha hizi," amesema na kuongeza:

"Naomba muondoke na hawa watu watuambie tunapataje fedha zetu ambazo tuliwapa kwa upendo mkubwa, mimi sina mzaha kwenye fedha za serikali," amesema Raibu.

"Takukuru naomba pia niwakabidhi wazabuni wanane waliokwapua fedha zetu za Halmashauri zaidi ya Sh47 milioni watuambie wanazirejesha hizi fedha za serikali,” amesema Raibu.

1617191535759.png
 
Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
14,382
2,000
Wakati mwingine huwa majukumu na mipaka ya TAKUKURU vinanichanganya sana.
 
Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
590
1,000
Si walishangilia Magufuli amefariki sasa watakula hela za wanyonge?

Lissu aliwaingiza chaka.
 
peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
2,557
2,000
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi, Juma Raibu ameagiza kukamtwa kwa wazabuni wanane wanaodaiwa kula fedha za Halmashauri zaidi ya Sh47 milioni pamoja na viongozi wa vikundi 45 vya asasi za kuweka na kukopa (Vicoba).

Viongozi hao wanadaiwa kuwa wameshindwa kurejesha zaidi ya Sh94 milioni walizokopa tangu mwaka 2015.

Raibu ametoa agizo hilo leo, Machi 31,2021 alipowaita viongozi hao ofisini kwake kutaka kujua hatma ya fedha hizo ambazo walikopewa na Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.

"Wote hapa niliowaita mmehujumu fedha za serikali, hili jambo linakera sana haiwezekani tangu mwaka 2015 mpaka leo hamjarejesha fedha hizi mnazodaiwa na Halmashauri zaidi ya Sh94 milioni, hili halikubaliki nawakabidhi leo mikononi mwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mtuambie mnarejeshaje fedha hizi," amesema na kuongeza:

"Naomba muondoke na hawa watu watuambie tunapataje fedha zetu ambazo tuliwapa kwa upendo mkubwa, mimi sina mzaha kwenye fedha za serikali," amesema Raibu.

"Takukuru naomba pia niwakabidhi wazabuni wanane waliokwapua fedha zetu za Halmashauri zaidi ya Sh47 milioni watuambie wanazirejesha hizi fedha za serikali,” amesema Raibu.

Kazi ya takukuru sio kukusanya madeni watu waliokopa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom