Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 56,667
- 30,584
Sio swala la kumwachia Hon. Waziri pekee. Nimependa hata manispaa kushiriki kupinga hili jambo.
Magazeti mengi leo yameandika swala la taasisi ya BWM kupewa kiwanja chenye makaburi. Embu tumheshimu Mungu tuwe na hofu na Mungu. Unanunuaje kiwanja huku unaonyeshwa makaburi ndani ya kiwanja chako bado unaona sawa?
Hii ni dhambii isiyozuilika na pongezi kubwa kwa Meya Jacob kugomea hiili swala maana ni kuwakosea haki marehemu...
Nani anataka kumchimbua ndugu yake saa hizi kisa tu kapewa mtu kiwanja kauziwa na manispaa? Jamani are we serious?
Mh jacob waliohusika wote pigeni chini kama wameweza kuwauza marehemu wanashindwaje kuwamaliza ninyi mlioko hai?
Hawa sio kabisa!
==================
MSTAHIKI MEYA BONIFACE JACOB wa Manispaa ya Kinondoni,ameagiza kusitishwa kwa shughuli yoyote ya ujenzi katika eneo ambalo lilikuwa na makaburi ya wananchi kata ya kawe(mbezi beach)..
Meya Jacob ametoa agizo hilo leo akiwa katika eneo ambapo alikwenda kwa nia ya kutaka kujua namna ambavyo Taasisi ya Benjamin Mkapa foundation ilivyonunua eneo hilo la makaburi kinyume na taratibu,wakipata idhini ya kufukua makaburi ya watu bila ushirikishwaji wa ndugu wa miili iliyozikwa eneo hilo,hali iliyopelekea malalamiko kumfikia baada ya wananchi kuona ufukuaji wa kimya kimya usiku wa manane katika sehemu wanayoifahamu kama ya kuzikia(makaburi)tangu miaka ya 1979.
Hatua hiyo imekuja baada ya baadhi ya wananchi kuandamana kudai eneo hilo ambalo inadaiwa liliuzwa na viongozi wa Manispaa hiyo.Mmoja wa wananchi hao alimueleza meya kuwa hawakupatiwa taarifa yoyote ya uuzwaji wa eneo hilo,"kulikuwa na makaburi zaidi ya 45 ya ndugu zetu tumekuja januari, mwaka huu kwa nia ya kufanya usafi makaburi ya ndugu zetu tumekuta yamefukuliwa, tulipohoji tukaambiwa kuwa pameuzwa na mnunuzi ni mkapa foundation, " alisema mfiwa mmoja.
Baada ya kauli hiyo, Jacob alimtaka ofisa Mtendaji wa kata ya kawe, Hamaton Bhao kulifafanua jambo hilo ambapo alisema mchakato huo ulifanyika kati ya juni na septemba, 2013,"mchakato ulifanyika katika ofisi yamtaa na kata, ilipofika septemba ilipendekeza mkapa foundation wapatiwe hati ya eneo kwa ajili ya matumizi ya ofisi,huku wakituhaidi kutununulia gari ya wagonjwa(ambulance) na jenereta tukipitisha walichukue na ndipo taarifa ikapelekwa manispaa".
Naye ofisa mipango miji, Irene Mbaga alisema ramani ya mipango miji inatambua eneo hilo ni eneo la wazi(open space) na si eneo la makaburi isipokuwa wananchi walijenga utamaduni wa kuzikia hapo.Baada ya kauli hiyo, meya alisema eneo hilo limeuzwa kinyume cha sheria na hivyo inapaswa lisiendelezwe,"ni aibu, kashfa hii imekuja manispaa siwezi kukabiliana na hili nahitaji kuona hiyo payment voucher ili tujue kama kweli walilipa kununua na fedha hizi zimekwenda kwa nani, pili sababu kubwa zaidi ni hakuna anayeruhusiwa kuhamisha makaburi,zaidi ya serikali na Taasisi zake " alisema.
Hata hivyo Meya Jacob alisema kwamba kusitishwa kwa kiwanja hicho kwa ajili ya uchunguz wa wahusika wote walioshiriki kuuza kwa Benjamin Mkapa foundation na kama iliuziwa na fedha zipo apewe eneo lingine lakini si makaburi na itakuwa ni mwendelezo wa kufuatilia viwanja vyote vyenye makaburi vilivyovamiwa hata kusababisha migogoro na viwanja vya wazi vilivyoibiwa.
Aidha Mheshimiwa diwani wa kata ya kawe,Muta Rwakatare,amemshukuru Mstahiki meya kwa kuliona na kuliingilia kati jambo hilo,alilosema lililenga kuletea aibu manispaa na kata yake kwa kuuuza maeneo ya kuzikia,huku akiomba pia makaburi ya Ruveti na Mlalakuwa kulindwa na kuwaondoa wavamizi.