Meya Jiji la Mwanza Mbaroni kwa mauaji ya Katibu wa CCM

Mongoiwe

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
524
263
Mstahiki Meya wa JIJI LA MWANZA Leonard Bihondo na diwani wa CCM kata ya Isamilo kwa tiketi ya CCM, amekamatwa na jeshi la polisi jana jioni Uwanja wa Ndege wa Mwanza wakati akitokea Dar es salaam. Kukamatwa kwakwe kunatokana na kudaiwa kuhusika na mauaji ya Katibu wa CCM kata ya Isamilo ambaye aliuawa kwa kuchomwa na kisi ofisini kwake Mei 14 mwaka huu majira ya saa 6:30 mchana kweupe.

xle6gm.jpg

Bihondo akiwa amevali mavazi yake ya umeya.

2nbzhb4.jpg

Katibu wa CCM kata ya Isamilo ambaye ameuawa kwa kuchomwa na kisu ofini kwake.
 
tatizo siyo kukatama, tatizo siyo tuhuma tu; tatizo kuthibitisha. Lakini kama kuna uzito mkubwa wa ushahidi ni lazima kwanza ajiuzulu. Hatuwezi kuwa na viongozi wenye mawingu ya shutuma na wanaendelea kuwa madarakani.
 
CCM hawa!!! Na yule chizi ndani ya upstairs yake -- MS -- anakazania kuwa CCM na JK ni imara itashinda tu kwa halali! haya mambo yanaashiria mwanzo wa mwisho wa chama hicho kinachotawala kwa nguvu za dola, kutishana kuuana na kukandamiza wapinzani tu. Hawajui kushinda kwa njia za uhalali.
 
Ilinukuliwa katika vyomba vya habari kwamba Waziri Masha alikuwa aonane na Katibu kata huyo (marehemu) wa Isamilo siku iliyofata kabla ya kifo chake. Hapa nilikuwa naweka ANGALIZO TUU kwa wale wanaofanya uchunguzi wa kifo hicho.
 
tatizo siyo kukatama, tatizo siyo tuhuma tu; tatizo kuthibitisha. Lakini kama kuna uzito mkubwa wa ushahidi ni lazima kwanza ajiuzulu. Hatuwezi kuwa na viongozi wenye mawingu ya shutuma na wanaendelea kuwa madarakani.
Ni kweli Mwanakijiji, kazi ipo katika kuthibitisha tuhuma, ila mpaka sasa habari zinaeleza kuwa kukamatwa kwake kunatokana na kukamatwa kwa muuaji siku ya tukio. Huyu muuaji ambaye anatoka Kigoma JUmanne Oscar (30) inadaiwa baada ya kubanwa vilivyo alisema yeye alifuatwa Kigoma kwa ajili ya kuua na Mpambe wa karibu ya meya huyo ajulikanaye kwa jina la Baltazal Shushi ambaye pia baada ya kukamatwa na polisi alisema alitumwa na aliyekuwa kampeni meneja wa Meya Abdul Hausi ambaye naye alikamatwa na kumtaja Meya.
Mkataba wa mauaji ulikuwa ni malipo ya sh. 10 milioni na muuaji alipokea milioni 2 za awali 8 ilikuwa akabihiwe baada ya kazi.
kwangu mimi siwezi kushangaa Meya huyu kuhusishwa na mauaji hayo kwani ni katika Jiji lake la Mwanza, Desemba 22 mwaka jana Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Frederick Katulanda alivamiwa nyumbani kwake na kukatwa mapanga wakiwa na mpango wa kumuua wakati akichunguza Upotevuwa wa Milioni 200 vilizoibwa kupitia akaunti za jiji. Wavamizi wa mwandishi huyo waliachiwa chini ya usimamizi wa kamanda Rwambow. Aliyekuwa Mbunge wa Mwanza Marehemu sasa Ally Shomari alimwagiwa Tindikali ofisini kwa mtindo huo wakati alipokuwa akihoji mapato ya jiji yalipo katika mwalo wa soko la samaki la Kirumba.
Mungu ameamua kumpiga kofi na kuwaonyesha nguvu zake, maana za mwisi 40
 
Kwa CCM hayo mambo ni ya kawaida kwao
 
Mwaka huu tutaona mengi kwa ajili ya uchaguzi.ehe mwenyezi mungu tusaidie roho hii chafu iondoke
 
CCM hawa!!! Na yule chizi ndani ya upstairs yake -- MS -- anakazania kuwa CCM na JK ni imara itashinda tu kwa halali! haya mambo yanaashiria mwanzo wa mwisho wa chama hicho kinachotawala kwa nguvu za dola, kutishana kuuana na kukandamiza wapinzani tu. Hawajui kushinda kwa njia za uhalali.

Mwalimu JKN aliisha sema sumu ya ubaguzi lazima ikurudie, walianza na wao wapinzani sisi sisiemu, sasa wapinzani wamekuwa weak kwa mizwengwe yao matokeo yake sasa wote wanataka kugombea uongozi kupitia chama hichohicho wakati nafasi ni chache, matokeo yake ni ndani ya sisiemu wenyewe wanaanza kubaguana na hata kuuana.

Ningekuwa strategist wa mambo ya usalama wa nchi ningeshauri sisiemu ijaribu kuachia mwanya wa angalau kuwe na strong opposition ili kuwagawana hawa wanaotaka uongozi na ubunge. Haiwezekani kila mtu awe mbunge haiwezekani kabisa. Huu ni mwanzo tu bado tutaona akina kalimanzira watatumika sana kujaribu kutoa watu roho za wapinzani wa wagombea.

Ila hii ya kutumia umafia katika individual level imeenda too far japo katika group level hili ni la kawida kabisa kwa wapenda kutawala.
 
Huyo KATIBU wa CCM wa kata aliyeuawa alikuwa ana maslahi gani kwa huyu mtuhumiwa? Mtu kufikia kupanga mipango ya kutoa uhai wa mtu mwingine lazima kuwe na something very big at stake! Wameendelea kufanya haya mambo siku nyingi, sasa wataumbuana vizuri..
 
SAKATA la kifo cha katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Isamilo wilayani Nyamagana mkoani Mwanza, Bahati Stephano (50) aliyefariki dunia baada ya kuvamiwa ofisini kwake na kuchomwa kisu, limeingia katika hatu nzito baada ya Meya wa jiji la Mwanza Leornad Bandiho Bihondo (64) (pichani) kukamatwa na jeshi la polisi kwa kuhusika.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Simon Sirro alisema kuwa kukamatwa kwa meya huyo kumetokana na taarifa za siri ambazo watuhumiwa watatu wa awali wamezitoa hivyo kufanya watuhumiwa kufikia wane.

Katibu huyo aliuawa mei 14, mwaka huu majira ya saa 6:30 mchana baada ya mtuhumiwa aliyetambulika kwa jina la Jumanne Oscar (30) kuingia ofisini kwa katibu huyo akisingizia kuwa na shida za kiofisi na baada ya kuruhusiwa kuonana naye alisikika wakibishana naye na baadaye alionekana akitoa kisu na kumchoma.

Kwa mujibu wa mashuhuda baada ya kuona mabishano hayo waliamua kufuatilia na kumuona kijana huyo akitoa kisu na kumchoma katibu huyo, upande wa titi la kushoto na tumboni, baada ya kufanya hivyo inadaiwa alitoka mbio kutaka kutokomea, lakini wasamalia wema wakiwemo wafanyakazi wenzake na marehemu wamkimbiza na kumkamata akitaka kujitosa ziwani” alisema Kamanda Sirro.

Jana akizungumza na waandishi wa habari kamanda Sirro alisema, meya Bihondo alikamatwa Juzi saa 10 alasiri katika uwanjwa wa ndege wa Mwanza alipokuwa akitokea safarini jijini Dar es salaam kwa safari zake za kikazi.

‘Bwana Bihondo tunamshikilia kama mtuhumiwa, hii ni kwa sababu baada ya kufanya mahojiano na watuhumiwa wengine watatu walimtaja yeye kuwa miongoni mwa watu ambao wanahusika. Jeshi langu bado linaendelea na uchunguzi na tutamfikisha mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika” alieleza Sirro.

Bihondo anaungana na watuhumiwa wengine ambao ni Jumanne Oscar aliyekamatwa siku ya tukio na kueleza kuwa alifuatwa Kigoma kwa kazi ya kuua na mtuhumiwa Baltazal Shushi (43) ambaye naye baada ya kutiwa mbaroni alimtaja kampeni meneja wake Abdul Hausi (45) wote wamekamatwa.

Alisema licha ya Bihondo kukamatwa bado kuna watuhumiwa wengine wanatafutwa na jeshi lake (lakini hakuwataja kwa sababu za kuhofia kuharibu upelelezi) na kusisitiza kuwa jeshi lake litahakikisha linawatia mbaroni na kukomesha mtandao wa watu waliozoea kuhusika na mauaji.

‘Niwaombe wananchi wazidi kutoa ushirikiano, kwani bila ya ushirikiano jeshi langu halitaweza kuwabaini mtandaao wa wauaji” alisisitiza Sirro. Habari hii imeandikwa na Frederick Katulanda. SOURCE: MWANANCHI
 
Kaa ni kweli, yaani hili zee la miaka 64 bado linang'ang'ana kuingia bungeni ili 'kuleta mabadiliko au maendeleo'.. lol.

Lakini lipi halikutegemewa hapa kwene nchi ambayo uongozi ni ufalme na si utumishi wala unyenyekevu? Uongozi ni kama blank cheque ya ku-exercise fantasies zooote za utajiri, misifa na kutetemekewa?
 
tatizo siyo kukatama, tatizo siyo tuhuma tu; tatizo kuthibitisha. Lakini kama kuna uzito mkubwa wa ushahidi ni lazima kwanza ajiuzulu. Hatuwezi kuwa na viongozi wenye mawingu ya shutuma na wanaendelea kuwa madarakani.

seconded!
 
Huyu muuaji ambaye anatoka Kigoma JUmanne Oscar (30) inadaiwa baada ya kubanwa vilivyo alisema yeye alifuatwa Kigoma kwa ajili ya kuua na Mpambe wa karibu ya meya huyo ajulikanaye kwa jina la Baltazal Shushi ambaye pia baada ya kukamatwa na polisi alisema alitumwa na aliyekuwa kampeni meneja wa Meya Abdul Hausi ambaye naye alikamatwa na kumtaja Meya.

Alibanwa vilivyo vipi? Walim-waterboard? Ushahidi wa mtu aliyebanwa vizuri hivyo kweli unaaminika?

Amandla........
 
Back
Top Bottom