Meya Issaya Mwita atoa tamko

Mayor hajui Sheria
Kwanza aliomba mahakama arudishiwe umeya Ina maana alikuwa anajua kuwa yeye Sio meya.Sasa alisema yeye Ni meya kivipi?

Hiyo akidi ya theluthi mbili Ni ya wajumbe waliohudhuria kikao haihesabu hata wale waliosusa kikao
Akidi ilitimia ya kumwondoa

Akidi ilitimia na uamuzi ungekuwa halali iwapo wajumbe ingalau 17 waliohudhuria hiyo juzi wangepiga kura ya "NDIYO, SINA IMANI NA MEYA" ukiondoa kura ya Meya mwenyewe ambaye kwa vyovyote asingejikataa mwenyewe.......

Lakini inasemekana kati ya 18 waliopiga kura za "NDIYO" ni 16 tu nje kabisa ya theluthi mbili inayotakiwa kisheria ndiyo waliunga mkono azimio huku wawili 2 wakilikataa.......

Hata hivyo, Meya wa manispaa ya Kinondoni Bwana Chaurembo anashangaza kidogo kwa kutoa maana mpya ya tafsiri ya 2/3.....

Kwamba, 2/3 ya wajumbe ktk swala hili inakokotolewa kutoka idadi ya wajumbe waliosaini azimio na mahudhurio ya kikao cha namna hii, which means katika wajumbe 18 (akiwemo aliyefojiwa saini), theluthi mbili yake ni kama wajumbe 13 hivi.....!!

Kwa mujibu wa CCM kanuni ya 2/3 kwa kikao chao cha tarehe 9/1/2020 ilikidhiwa na hivyo uamuzi wa kumuondoa Meya Isaya Mwita ni halali kikanuni na kisheria.....

Nadhani mjadala uko hapa, kuwa kweli au siyo kweli??
 
Mayor Issaya Mwita anaandika...

Na Issaya Mwita.
Mayor wa Jiji la DSM.

Marafiki zangu nawashukuru kwa maombi na dua zenu

Kuna watu wengi hawakumuelewa hakimu kwa maamuzi yake ile jana

Nilifungua kesi 6/01/2020... Siku ya Jumatatu, katika maombi yangu nilimtaka hakimu anipe mambo mawili

1. Kwanza anipe zuio la muda na kwamba mimi Isaya Mwita niendelee kuwa Mayor Mpaka pale mahakama itakaposikiliza kesi yangu ya Msingi

Na nikaieleza mahakama kwamba tayari kuna procedure mbalimbali za kuniondoa katika nafasi yangu

Maombi yangu ya pili ilikuwa ni muda wa kudumu mpaka nitakapoipata haki yangu

Kwa kuwa maombi yangu niliyapeleka kwa hati ya dharura tulipangiwa kusikiliza 8/1/2020.

Tarehe 7 jioni wajumbe wa baraza tulipata barua ya kuitwa kwenye kikao na kwamba kikao kitakuwa 9/01/2020... Alhamisi saa 4 asubuhi ...

Kwa hiyo nikaipeleka barua ile ya wito mahakamani asubuhi ya 8/01 ambayo ndiyo ilikuwa siku ya kusikiliza kesi hiyo ...

Barua ile wa wito haikupokelewa ...kwa mizengwe tuu ...na mawakili wa serikali wakiongozwa na Naibu wa mwanasheria Mkuu ndugu Malata ... wakasema barua hiyo ilipaswa kufailiwa kabla ya samansi kuwafikia

Kesi yetu ikaendelea siku hiyo ya tarehe 8 na tulitegemea kupewa status quo...lakini hakimu hakutoa siku ile ..akapanga Siku ya 9... mchana

Kumbuka kwamba wito wa kikao cha baraza ni saa 4 hiyo hiyo 9/01/2020

Ikanilazimu kuhudhuria baraza siku hiyo ...na kama mlivyosoma kwenye vyombo vya habari .... Marafiki zangu hawa wakapiga kura na kupata 16 votes ...

Ikumbukwe kwamba baraza la jiji la Dar es salaam lina wajumbe 26

Wabunge 5... kila mbunge anaiwakilisha wilaya (Halmashauri)
Mameya 6
Na madiwani 15 ...kila Halmashauri inaleta madiwani watatu watatu ... hivyo basi idadi yetu inakamilika kwa kuwa na wajumbe 26

Sasa marafiki zangu kutafuta 2/3 ya 26 unaweza kuona ni 17.3 ...

Kanuni zetu za kudumu ..Toleo la 1982 kama lilivyotangwa na gazeti la serikali ...

Kanuni 12... unaonesha kwamba ...ili kumuondoa Mayor..2/3 ya wajumbe watasaini ili kupata uhalali wa kuitisha mkutano Maalum wa kumuondoa meya ...Kigezo hicho madiwani walikikidhi

Sasa utata ulikuja pale ambapo ..marafiki zangu hawa walimtegemea yule Diwani aliye wasainia kutotokea kwenye kikao ...wakabaki wamepigwa butwaa... Mara wakafanya maamuzi ya haraka .."Tumsainie jina lake" kweli walifanya hivyo ...mimi na baadhi ya wajumbe tulichelea kuingia ... nilipoingia ndiyo nikagundua jina la Diwani yule limekuwa fojali...

Hapo ndipo kizaa zaa kipoanza

Lakini baadae tulikubaliana tukaendelea tukapiga Kura CCM wakapata 16 na sisi tumebaki na kura 2 tu

Kanuni ya 84 (1) inasema Meya ataondolewa madarakani kwa 2/3 ya wajumbe wa Halimashauri hapo ndipo walipokwama.

Wakaanza maigizo kwamba ni 2/3 ya wajumbe waliohudhuria kikao wakasahau kwamba ni 2/3 ya wajumbe ndiyo iliyoitisha kikao kile

Turudi sasa kwa Maamuzi ya Mahakama ...

Kwangu mimi sioni kama Hakimu amekosea kwani hatukupeleka barua ile kwa muda ...
Hivyo alikuwa sawa kuninyima struts quo ...

Lakini pia maamuzi hayo wangekuwa na maana sana ile siku ya 8/01/2020 au 9/01

Maamuzi ya jana hayana athari yoyote kwangu kwa kuwa tayari kile nilichotaka kukizuia kilishafanyika 9/01/2020 ... na kwamba sasa Azimio la kutaka kuniondoa limekosa uhalali wa kikanuni

Asanteni sana.

Uwiano wa madiwani (wajumbe) wanaounda baraza la madiwani wa Jiji la DSM kati ya CCM na vyama vingine ukoje kwani?

Iweje CCM wawazidi wakati toka mwanzo idadi ya wajumbe wa baraza toka vyama pinzani ilikuwa kubwa na ndiyo maana wakaongoza Jiji?

Kwa anayejua, tafadhali atujuze hapa
 
Kwa hiyo mwenye kura ya VETO ya umeya wa Dar ni huyo diwani wa CUF pekee ambaye hakutokea.
 
Kwanini waziri hajatoa kulalamikiwa kuboronga uchaguzi wa serikali za mitaa matokeo yake aliipongeza ccm?
Yeye yupo kwenye mpango na yeye ndo aliyeratibu na TISS anahusika na ubabaishaji huu
Naomba ufafanuzi wa haya.
1. Theluthi mbili ya akidi ya wajumbe wa kumtoa Meya haikufika kikanuni , sasa ni kwa nini kikao kikaendelea?
2. Ni kwa nini Waziri mwenye dhamana na Tamisemi hajatoa tamko lolote hadi sasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba ufafanuzi wa haya.
1. Theluthi mbili ya akidi ya wajumbe wa kumtoa Meya haikufika kikanuni , sasa ni kwa nini kikao kikaendelea?
2. Ni kwa nini Waziri mwenye dhamana na Tamisemi hajatoa tamko lolote hadi sasa?
MIMI KADRI YA MAELEZO YA MEYA AKIDI ILIFIKIWA YA WAJUMBE WALIOHUDHURIA ILI KUPIGA KURA YA KUMTOA.WALIFIKIA 18 JUMLISHA NA MEYA MWENYEWE NI 18. Ila wawili walipinga na kulikuwa na mjumbe aliyetegemewa awepo ili theluthi mbili ya wajumbe wakumwondoa ya 17 iseme ndio. WAJUMBE WAHUSIKA WA KUMWONDOA AMEELEZA NI 26. Huko marekani hata ukiwa mgonjwa unafuatwa upige KURA.
 
Mayor hajui Sheria
Kwanza aliomba mahakama arudishiwe umeya Ina maana alikuwa anajua kuwa yeye Sio meya.Sasa alisema yeye Ni meya kivipi?

Hiyo akidi ya theluthi mbili Ni ya wajumbe waliohudhuria kikao haihesabu hata wale waliosusa kikao
Akidi ilitimia ya kumwondoa

Kuandika kwenyewe tu hueleweki sembuse pointless zako
 
Naomba ufafanuzi wa haya.
1. Theluthi mbili ya akidi ya wajumbe wa kumtoa Meya haikufika kikanuni , sasa ni kwa nini kikao kikaendelea?
2. Ni kwa nini Waziri mwenye dhamana na Tamisemi hajatoa tamko lolote hadi sasa?
Waziri hajatoa tamko kwa sababu Jiwe hajamwambia lakufanya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom