Meya Ilala: Niliahidi kujenga madarasa matano shule ya msingi Bunyokwa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Bonyokwa kwa Mara nyingine tena ametembelea mradi wa ujenzi wa madarasa mawili (2) unaoendelea katika shule ya Msingi Bonyokwa. Mhe. Kuyeko ameridhishwa na kiwango kizuri cha madarasa yaliyojengwa shuleni hapo na kuwataka mafundi waliojenga vyumba hivyo viwili vya madarasa waanze Mara moja ujenzi wa vyumba vingine vitatu vya madarasa katika shule hiyo.

Katika ziara hiyo Mhe. Kuyeko alisema kuwa moja ya ahadi alizozitoa wakati wa kampeni ni kujenga vyumba vitano vya madarasa katika shule ya msingi Bonyokwa. Shule hiyo imekuwa na upungufu mkubwa wa madarasa na madawati na kupelekea watoto kusomea chini ya miti huku wakiwa wamekaa chini. Kuyeko amasema wananchi wa Bonyokwa walimuamini yeye (Kuyeko) na ndiyo maana wakamchagua hivyo hilo ni deni kwangu. Na njia pekee ya kulipa deni hilo ni kutimiza ahadi zangu zote kwa wananchi wa Bonyokwa na wana Ilala wote. Hivyo basi ahadi ya kujenga madarasa itakamilika mapema iwezekanavyo.

Aidha, kukamilika kwa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na kuanza ujenzi wa vyumba vingine vitatu jukumu linalofuata ni kufanikisha mpango wa upatikanaji wa madawati, meza na viti. Pia ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa utaenda sambamba na ujenzi wa ofisi za walimu katika shule hiyo.

Katika kuonyesha kuwa Mhe. Kuyeko hafurahishwi na ukosefu wa madarasa, vyoo, meza na viti mchakato wa upanuzi wa shule ya Msingi Kifuru umeanza. Mchakato wa awali wa upanuzi wa shule hiyo unalenga kununua maeneo yanayoizunguka shule hiyo ambapo tayari wakubwa wa Ilala walishatembelea eneo hilo na kilichobaki ni Mkurugenzi kulipeleka jambo hilo Mbele ya Baraza la Madiwani wa Manispaa
Ilala.

Katika kupambana na upungufu wa vyumba vya madarasa, vyoo, madawati, meza na viti Mhe. Kuyeko amesema zoezi hilo pia atalisimamia kwa karibu sana katika Manispaa mzima ya Ilala. Amewaomba Madiwani na na watendaji wote wa Manispaa ya Ilala tujitoe kwa hali na Mali katika kutatua matatizo ya wananchi wa Ilala na taifa kwa ujumla.

Imetolewa Leo 18/06/2016
Na Alex Massaba
Katibu wa Meya Manispaa ya Ilala.
0656568256
 

Attachments

  • IMG-20160618-WA0078.jpg
    IMG-20160618-WA0078.jpg
    86.8 KB · Views: 35
  • IMG-20160618-WA0079.jpg
    IMG-20160618-WA0079.jpg
    63.9 KB · Views: 38
Back
Top Bottom