Meya Ilala azindua mradi wa maji Vingunguti

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Katika kuonyesha dhamira ya kutatua kero sugu za wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na viunga vyake, Leo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Mhe. Kuyeko amezindua mradi wa Maji na vyoo viwili katika Kata ya Vingunguti.

Miradi hiyo miwili iliyojengwa katika Kata ya Vingunguti, mtaa wa Mtakuja na mtaa wa Mtambani imejengwa na CIUP chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia.

Awali akizungumza katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Mtakuja, ndugu Sharifu Abdallah Mbulu alisema kuwa miradi hiyo ilikuwa ijengwe na kukamiliki toka mwaka 2013 lakini kutokana ubadhirifu na usimamizi mbovu wa uongozi uliopita (CCM) walishindwa kusimamia ujenzi wa miradi hiyo. Uongozi mpya wa mtaa wa mtakuja uliongia mwaka 2014 kwa kushirikiana na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Vingunguti, Mhe. Omary Kumbilamoto kwa muda mfupi wamefanikiwa kuikamilisha miradi hiyo.

Mhe. Kumbilamoto akizungumza katika uzinduzi huo amesema mradi huo utakuwa na faida tatu. Faida ya kwanza ni kuwa mradi wa Maji umelenga kuwaondolea wananchi wa mitaa adha ya Maji. Faida ya pili ni usafi wa mazingira kwani wananchi hasa wafanyabiashara walikuwa wanakojoa hadharani na kuelekea kuchafua mazingira. Naibu Meya alitumia nafasi hiyo kupiga marufuku kukojoa hadharani maana hakuna kisingizio tena. Naibu Meya alisema faida ya tatu ni kwa mtaa na Kata kupata mapato kwa choo mile kitakuwa kinalipiwa.

Mhe. Kumbilamoto pia alimwelezea Mstahiki Meya wa Ilala kuwa Kata ya Vingunguti pia inakabiliwa na changamoto ya baadhi ya mitaa kutokuwa na maafisa watendaji. Kata inamitaa Sita lakini mitaa mitatu ndiyo ina maafisa watendaji na mitaa mitatu haina watendaji hali ambayo inarudisha nyuma utendaji kazi. Lakini changamoto nyingine ni kufufua visima vya Maji katika mitaa minne iliyobakia ya Kata hiyo.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ndiye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo Mhe. Charles Kuyeko akizungumza katika uzinduzi huo amempongeza Diwani wa Kata ya Vingunguti na viongozi wenzake wa mitaa yote ya Kata hiyo. Mhe. Kuyeko amewapongeza pia wananchi wa Kata ya Vingunguti kwa kuchagua viongozi wachapakazi na wenye shauku ya kuwaletea maendeleo wananchi wao. Mhe Kuyeko alisema faida ya kutumia vizuri haki ya kupiga kura ni kuchagua kiongozi bora ambaye ni mwakilishi wa wananchi na mwenye uwezo wa kutatua kero za wananchi wake ambapo Vingunguti mmefanikiwa. Vingunguti ninaijua vizuri sana, lakini Vingunguti ninayoijua siku zote siyo hii ya Leo, imebadilika sana imekuwa safi na hata nyuso za watu wake zimebadilika, zinaonyesha matumaini mazuri tofauti na zamani, alisema Kuyeko.

Aidha, Kuyeko aliwataka wananchi wa Kata ya Vingunguti bila kujali itikadi zao watoe ushirikiano wa dhati kwa Diwani kwani nimchapakazi na mpenda maendeleo. Diwani wenu ni Naibu Meya wa Ilala hivyo kiitifaki ni msaidizi wangu mkuu kwa nafasi hiyo nimepata fursa ya kumfamu vizuri ni mchapakazi, mpenda maendeleo kwa hiyo mkimpa ushirikiano mzuri maendeleo mnayoyataka mtayapata, alisema Kuyeko.

Meya pia ametumia nafasi kuwataka Madiwani wote wa Ilala kuiga mfano wa Diwani wa Vingunguti kuwa karibu na wananchi wao ili kujua changamoto zinazowakabili. Mhe. Kuyeko amewataka Madiwani kushirikiana na wananchi wa Kata zao kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi wao. Wapiga kura wanamatumaini na sisi, maana wakati tunaomba kura tuliahidi Mabadiliko, Mabadiliko hayo ni kuleta maendeleo kwa wananchi wetu, alisema Kuyeko. Kuyeko pia alisema kwa nafasi yake ya kuwa Meya wa Ilala kwa kushirikiana na Madiwani wote miradi ya maendeleo itafanikiwa.

Mstahiki Meya amechangia Tshs. 5,000,000/ ili zisaidie kusukuma miradi ya maendeleo kwa Kata ya Vingunguti hasa kufufua visima vya Maji kwa mitaa iliyobakia.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa pia na viongozi wa chama vya UKAWA; Katibu Mwenezi wa Chadema kata ya vingunguti Kamanda Masiaga, Katibu wa Cuf Kata, afisa mtendaji wa mtaa Mtakuja Lilian James.

Imetolewa Leo 28/06/2016
Na Alex Massaba
Katibu wa Meya Manispaa Ilala.
0656 568256
 

Attachments

  • IMG-20160628-WA0089.jpg
    IMG-20160628-WA0089.jpg
    76.6 KB · Views: 48
  • IMG-20160628-WA0085.jpg
    IMG-20160628-WA0085.jpg
    71.2 KB · Views: 52
  • IMG-20160628-WA0086.jpg
    IMG-20160628-WA0086.jpg
    82.5 KB · Views: 56
  • IMG-20160628-WA0087.jpg
    IMG-20160628-WA0087.jpg
    77.4 KB · Views: 59
Safi sana fanyeni kwa kasi zaidi yale yaliyoshindikana kwa miaka 50 japo yapo ndani ya uwezo wetu hasa suala la usafi wa mazingira hasa kwenye masoko.
 
Back
Top Bottom