Meya Dar aamuru polisi wenye silaha kutoka ukumbini

M

mashakani

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2018
Messages
354
Likes
424
Points
80
M

mashakani

JF-Expert Member
Joined Aug 15, 2018
354 424 80
Meya Dar aamuru polisi wenye silaha kutoka ukumbini

pic+meya.jpg

Kwa ufupi
  • Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani la Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amewaamuru polisi wenye silaha za moto waliokuwa ndani ya ukumbi wa mkutano kutoka nje kwa madai uwapo wao unawatisha wajumbe.

Dar es Salaam. Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amewataka polisi wenye silaha za moto kutoka nje ya ukumbi wa Baraza la Madiwani wa jiji hilo kwa madai kuwa uwapo wao unawatisha wajumbe wa baraza hilo.

Mwita alitoa amri hiyo leo baada ya mmoja wa wajumbe wa baraza hilo, Saed Kubenea kuomba utaratibu kuhusu uwapo wa askari na uhuru wa kutoa maoni.

Ilivyokuwa
Baada ya dua ya kuliombea baraza hilo lenye ajenda ya uchaguzi wa Naibu Meya wa jiji ili kuziba nafasi ya Mussa Kafana aliyejiuzulu na kuhamia CCM, Kubenea alisema: “leo mkutano huu una wageni wengi hasa askari polisi wenye silaha za moto tena ndani ya ukumbi lakini siyo utaratibu mwenyekiti.”

"Hatukatai vyombo vya usalama kuwapo humu ndani lakini hizi silaha za moto si sahihi. Tunaomba watoke nje ili tuendelee na kikao.”

Baada ya maelezo hayo, Mwita alimpa nafasi katibu wa baraza hilo, Sipora Liana kutoa ufafanuzi kuhusu hatua ya polisi wenye silaha kuwapo ndani ya kikao hicho.

"Mimi ndiye nimeandaa mkutano huu, nimeamua kuweka ulinzi kutokana na historia ya vikao vya nyuma kuwa na vurugu. Nataka mkutano uwe na ulinzi na utulivu.”

"Nimewahakikishia ulinzi wajumbe wangu ndiyo maana ulinzi upo hapa nami ndio muandaaji wa kikao hiki,” alisema Liana.
Baada ya maelezo hayo, Mwita alimpa nafasi tena Kubenea ambaye alsisitiza polisi hao watoke nje na kama vurugu zitatokea wataitwa ndani.

“Hata kule bungeni vurugu zikitokea Spika ana agiza askari waingie ndani," alisema Kubenea.

Maelezo hayo ya Kubenea yalimfanya Mwita kuagiza askari waliokuwa na silaha watoke nje ya ukumbi jambo ambalo lilitekelezwa.

Wakati Meya wa Ubungo akisikika akisema hatoweza kutoa maoni huku askari hao wakiwa ukumbini na silaha, mjumbe mwingine wa CCM, Mussa Ntinika alisikika akisema siyo jambo jema na halileti tafsiri nzuri kwa vyombo vya ulinzi kutolewa nje ya ukumbi.

Chanzo: Mwananchi
 
Kurzweil

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Messages
5,627
Likes
6,195
Points
280
Kurzweil

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined May 25, 2011
5,627 6,195 280
Dar es Salaam.

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amewataka polisi wenye silaha za moto kutoka nje ya ukumbi wa Baraza la Madiwani wa jiji hilo kwa madai kuwa uwapo wao unawatisha wajumbe wa baraza hilo.

Mwita alitoa amri hiyo leo baada ya mmoja wa wajumbe wa baraza hilo, Saed Kubenea kuomba utaratibu kuhusu uwapo wa askari na uhuru wa kutoa maoni.

Ilivyokuwa

Baada ya dua ya kuliombea baraza hilo lenye ajenda ya uchaguzi wa Naibu Meya wa jiji ili kuziba nafasi ya Mussa Kafana aliyejiuzulu na kuhamia CCM, Kubenea alisema: “leo mkutano huu una wageni wengi hasa askari polisi wenye silaha za moto tena ndani ya ukumbi lakini siyo utaratibu mwenyekiti.”

"Hatukatai vyombo vya usalama kuwapo humu ndani lakini hizi silaha za moto si sahihi. Tunaomba watoke nje ili tuendelee na kikao.”

Baada ya maelezo hayo, Mwita alimpa nafasi katibu wa baraza hilo, Sipora Liana kutoa ufafanuzi kuhusu hatua ya polisi wenye silaha kuwapo ndani ya kikao hicho.

"Mimi ndiye nimeandaa mkutano huu, nimeamua kuweka ulinzi kutokana na historia ya vikao vya nyuma kuwa na vurugu. Nataka mkutano uwe na ulinzi na utulivu.”

"Nimewahakikishia ulinzi wajumbe wangu ndiyo maana ulinzi upo hapa nami ndio muandaaji wa kikao hiki,” alisema Liana.

Baada ya maelezo hayo, Mwita alimpa nafasi tena Kubenea ambaye alsisitiza polisi hao watoke nje na kama vurugu zitatokea wataitwa ndani.

“Hata kule bungeni vurugu zikitokea Spika ana agiza askari waingie ndani," alisema Kubenea.
Maelezo hayo ya Kubenea yalimfanya Mwita kuagiza askari waliokuwa na silaha watoke nje ya ukumbi jambo ambalo lilitekelezwa.

Wakati Meya wa Ubungo akisikika akisema hatoweza kutoa maoni huku askari hao wakiwa ukumbini na silaha, mjumbe mwingine wa CCM, Mussa Ntinika alisikika akisema siyo jambo jema na halileti tafsiri nzuri kwa vyombo vya ulinzi kutolewa nje ya ukumbi
 
P

Pohamba

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2015
Messages
18,242
Likes
29,927
Points
280
P

Pohamba

JF-Expert Member
Joined Jun 2, 2015
18,242 29,927 280
Kubenea hapendi Polisi Kwa Kuwa amekubuhu Kwenye uhalifu

Huyu anatuhumiwa kutaka Kumteka Mwenyekti wa Taifa wa Chadema hali iliyopelekea mpaka Mh. Mbowe kuamua kukiuka Masharti ya dhamana ili tu arudishwe rumande Kwa usalama wake kuepuka vitisho vya Saeed
 
Akasankara

Akasankara

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2015
Messages
2,058
Likes
2,149
Points
280
Akasankara

Akasankara

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2015
2,058 2,149 280
Kubenea hapendi Polisi Kwa Kuwa amekubuhu Kwenye uhalifu

Huyu anatuhumiwa kutaka Kumteka Mwenyekti wa Taifa wa Chadema hali iliyopelekea mpaka Mh. Mbowe kuamua kukiuka Masharti ya dhamana ili tu arudishwe rumande Kwa usalama wake kuepuka vitisho vya Saeed
Baada ya Lumumba na magogoni kumteka Mo, je walifanikiwa kupata fedha?
 
Bila bila

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Messages
5,601
Likes
7,909
Points
280
Age
40
Bila bila

Bila bila

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2016
5,601 7,909 280
Kubenea hapendi Polisi Kwa Kuwa amekubuhu Kwenye uhalifu

Huyu anatuhumiwa kutaka Kumteka Mwenyekti wa Taifa wa Chadema hali iliyopelekea mpaka Mh. Mbowe kuamua kukiuka Masharti ya dhamana ili tu arudishwe rumande Kwa usalama wake kuepuka vitisho vya Saeed
Kwa akili yako umeona Polisi ni wajumbe wa Baraza la Madiwani?
 
marxlups

marxlups

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Messages
10,023
Likes
4,489
Points
280
marxlups

marxlups

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2011
10,023 4,489 280
Mussa Ntinika alisikika akisema siyo jambo jema na halileti tafsiri nzuri kwa vyombo vya ulinzi kutolewa nje ya ukumbi

Yangejirudia ya Kinondoni ya risasi kukata kona na kumfuata yeye labda angeelewa wenzake wanamaanisha nini
 
Forum statistics

Threads 1,235,679
Members 474,712
Posts 29,230,348