Meya (CCM) jiji la Mbeya kitanzini

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
Madiwani Mbeya wamweka Meya njia panda

Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga, amewekwa njia panda na Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, baada ya kutakiwa kujibu tuhuma nane zinazomkabili ndani ya siku saba, ikiwemo ya matumizi mabaya ya fedha za halmashauri.

Meya huyo anatuhumiwa kutumia Sh. 5, 760,000 kama nauli ya ndege kwenda na kurudi nchini China kwa safari isiyokuwa rasmi ya kikazi.

Alidai sababu nyingine zinazoonyesha kuwa Meya wa Jiji la Mbeya, alihusika katika vurugu hizo ni kwamba, siku Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Mr. Sugu alipokwenda kuzungumza na wananchi kuwatuliza akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Evance Balama na Mkurugenzi wa Jiji, Idd Juma katika hali ya kushangaza Meya huyo ambaye alikuwa katika msafara huo aliingia mitini.

Mwabulanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Madiwani wa Chadema, alisema Meya huyo bila idhini ya Baraza la Halmashauri ya Mbeya Mjini, aliidhinisha matumizi ya mamilioni ya fedha za halmashauri kwa ajili ya matumizi ya tume aliyoiunda kuchunguza madiwani wawili kinyume cha kanuni za kudumu za halmashauri ya jiji hilo za mwaka 2004 sehemu ya nne kifungu Na.40, 2 (C) ..........

Meya huyo pia anadaiwa kutumia madaraka yake vibaya kwa kuwaahidi watu viwanja na hivyo kujipatia mamilioni ya fedha, huku akishindwa kuwapatia viwanja hivyo, na kwamba pia ameamuru Diwani wa Kata ya Itende kuvunja daraja lililojengwa kwa fedha za Mbunge wa Mbeya Mjini, Mbilinyi ......

Mara baada ya kusomwa kwa tuhuma hizo, Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Juma, alitoa ufafanunuzi kuwa, Meya huyo hawezi akazijibu tuhuma katika kikao hicho na badala yake zinatakiwa ziwasilishwe kwa Mkurugenzi ili Meya akabidhiwe na kuzijibu ndani ya siku saba na baadaye zijadiliwe katika kikao cha Baraza la Madiwani kitakachopangwa.........​
 
Tunahitaji kuendelea kuona mapinduzi everywhere. Mbeya is among the regions I am proud of in this country.Watanzania wanahitaji kuhoji Magamba wametufisidi vya kutosha. CDM ndilo tumaini letu kwa sasa.
 
Huyu Meya aliupata huyo Umeya kwa njia za rushwa hasa baada ya kuwalipia fomu za kuapa mahakamani karibu madiwani wote wa CCM Sh 8,000 kila mmoja baada ya uchaguzi wa Madiwani mwaka jana hivyo kufanya jumla ya fedha alizolipa kuwa zaidi ya laki mbili! CCM ilifanya kila juhudi asifikishwe mahakamani na ndivyo ilivyotokea. Katika uchaguzi wa Meya huyu Mheshimiwa alipita ili kurudisha fadhila kwa Madiwani wenzake!
Sasa Madiwani wa CCM kumtaka Kapunga (Meya) kutoa maelezo sio unafiki? Wao walifikiri angeacha kula rushwa baada ya kuwa Meya? Angerudishaje LAKI MBILI na zaidi alizotumia kuhonga?
Magamba acheni unafiki, mnavuna mlichopanda!
Afadhali Madiwani wa CDM wangempa Kapunga hizo siku 7 kuliko Magamba ambao hawana kabisa moral authority ya kufanya hivyo!
 
Huyu jamaa bogus mno, tena nasikia mtumiaji mzuri wa mitishamba. Kwenye kikako hiki cha Madiwani wanadai alijaribu kujitetea kwa kusema:
"Hapa jamani lazima niseme ukweli ile hali ya vurugu za machinga ilikuwa ya hatari, siwezi kupoteza maisha yangu kwa ajili ya umeya, mimi nikifa mtachagua meya mwingine, hali ile ilikuwa ya kutisha …jamani hakuna mtu asiyeogopa kifo, siwezi kufa eti kwa kuwa ni meya, niliondoka kweli baada ya kuona hali mbaya,"
 
Wezi tu hawa ccm. kila mahali hakuna walichoweza, hakuna walichosubutu, sasa wanasonga mbele kuelekea wapi?
 
Niliwahi kugonga naye Castle Lager pale Kirumba resort Mwanza... Sijui alitia timu kutokea wapi but ni mchangamfu sana hasa kukiwa na Totoz. Ahukumiwe kwa haki katika hayo makosa
 
Mafisadi wa nji hii Magamba mnatisha lakn muda wenu umefikia mwisho,subirini muda wenu umekaribia sana
 
Back
Top Bottom