Meya Boniface: Namuombea msamaha DC wa ubungo kwa wananchi.

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
NAMUOMBEA MSAMAHA DC WA UBUNGO KWA WANANCHI

Baada ya kupata wasaa na Muda wa kutosha wa kutafakari, ni muda sahihi wa kuongelea tukio hili la kijinga na Maudhi.

Ni dhahiri kuanzia Jumatano nitoke Mahabusu ya POLISI mpaka leo jumamosi ni kweli hasira zimeisha na busara imetamalaki kichwani kwangu.

Nimeona kupitia vyombo mbalimbali vya Habari na mitandao ya kijamii kila mtu akilaani na kukasirishwa na Matumizi mabaya dhidi ya vyombo vya Dola, hata kupelekea mimi kushikiliwa kituo cha polisi Mbezi(w).

Kwa Masaa 48 mahabusu hata mimi nilikuwa na hasira sana, kwanza nilijiona ninamkosi kwakuwa nilihisi anayafanya haya sababu ya Maswahibu yaliyomkuta ya kuondolewa kuwa Boss ikulu mpaka kuletwa kuwa Dc Ubungo.

Msameheni Dc Ubungo, kwa sababu tatu:

1. Nimepata ujumbe wake kwa walio nifikishia kuwa, anakiri tukio la namna ile si Zuri, na ametoa pole na masikitiko yake kutoka Moyoni.

2. Kwa sababu hao walio na Mamlaka juu yake walitaka afanye vile, asinge fanya kama alivyo agizwa ni dhahiri ingekula kwake Mazima, hivyo alikuwa anatetea Kitumbua chake.

3.Kaonyesha Uungwana mkubwa sana, ingawa amekosa uthubutu wa kuyasema hayo Hadharani, lakini tunapaswa kuyajua mazimgira ya kazi yake na kibarua chake.

Kw sababu tatu nilizo taja hapo juu ADUI wa wana Ubungo siyo DC ni hao waliomuagiza kufanya aliyoyafanya,na waliotoa Amri hiyo sina sababu ya kuwa taja,
Mimi ninawajua...
Wewe unawajua....
Watanzania wanawajua....
Dunia inawajua......

Kulumbana na Dc ni kupoteza lengo katika Halmashauri yetu mpya na nzuri tuliyopewa na Wananchi wakati wa uchaguzi 2015.

Wakati Ubungo kuna kampeni ovu inayoitwa KOMBOA UBUNGO Inayo ongozwa na DSO UBUNGO kwa maana ya kuwarudisha CCM majimboni na kwenye kata.....
Mimii ninawaomba kumpatia ushirikiano DC kwakuwa ni mtu mwelewa kwakiwango fulani, ni jambo hili tu Mabosi zake walilenga kumfitinisha na Viongozi wa Halmashauri.

Aidha nimepokea pole na Hongera za Watanzania nje na ndani ya Ubungo

Masaa 48 polisi Mbezi, yamenifanya nikamilishe "kukaa ndani" Mahabusu zote za Dar, nilisha kaa mahabusu 15 na Magereza manne(4), ilikuwa imebakia mahabusu 1 ya Mbezi polisi, tena kwa makosa ya kisiasa, hivyo nimemuhaidi OCD MBEZI POLISI kupeleka vifaa vya usafi.

MWISHO
Ninapenda kuutarifu Umma wa Watanzania ndani na nje ya Ubungo kuwa Nimeanza safari rasmi ya kutafuta haki dhidi ya sheria hii kandimizi ya ma Dc na ma Rc, haijalishi nitafika au la.
Moyoni nimeweka Nadhiri ya kuwa kiongozi wa Mwisho wa kisiasa aliyechaguliwa kutendewa sivyo kwa kisingizio cha sheria kandamizi na hata kama safari hii kuna nitakao wagusa, basi ni kwa sababu itahitajika mifano tu. Lakini nia ni mimi kuwa muhanga wa mwisho.

Na Boniface Jacob
Mstahiki Meya
Halmashauri ya ubungo

Senior councilor
 
-Masaa 48 polisi Mbezi, yamenifanya nikamilishe "kukaa ndani" Mahabusu zote za Dar, nilisha kaa mahabusu 15 na Magereza manne(4), ilikuwa imebakia mahabusu 1 ya Mbezi polisi, tena kwa makosa ya kisiasa, hivyo nimemuhaidi OCD MBEZI POLISI kupeleka vifaa vya usafi
 
Hivi mpaka sasa ni ' Wanaharakati ' wangapi ' wameshapotea ' nchini Tanzania?
 
Forgiveness is not something we do for other people, We do it for ourselves so that we can move forward
 
IMG-20170624-WA0025.jpg

Baada ya kupata wasaa na Muda wa kutosha wa kutafakari, ni muda sahihi wa kuongelea tukio hili la kijinga na Maudhi.

Ni dhahiri kuanzia Jumatano nitoke Mahabusu ya POLISI mpaka leo jumamosi ni kweli hasira zimeisha na busara imetamalaki kichwani kwangu.

Nimeona kupitia vyombo mbalimbali vya Habari na mitandao ya kijamii kila mtu akilaani na kukasirishwa na Matumizi mabaya dhidi ya vyombo vya Dola, hata kupelekea mimi kushikiliwa kituo cha polisi Mbezi(w).

Kwa Masaa 48 mahabusu hata mimi nilikuwa na hasira sana, kwanza nilijiona ninamkosi kwakuwa nilihisi anayafanya haya sababu ya *Maswahibu yaliyomkuta ya kuondolewa kuwa Boss ikulu mpaka kuletwa kuwa Dc Ubungo.*

Msameheni Dc Ubungo, kwa sababu tatu:

1. Nimepata ujumbe wake kwa walio nifikishia kuwa, anakiri tukio la namna ile si Zuri, na ametoa pole na masikitiko yake kutoka Moyoni.

2. Kwa sababu hao walio na Mamlaka juu yake walitaka afanye vile, asinge fanya kama alivyo agizwa ni dhahiri ingekula kwake Mazima, hivyo alikuwa anatetea Kitumbua chake.

3.Kaonyesha Uungwana mkubwa sana, ingawa amekosa uthubutu wa kuyasema hayo Hadharani, lakini tunapaswa kuyajua mazimgira ya kazi yake na kibarua chake.

Kw sababu tatu nilizo taja hapo juu ADUI wa wana Ubungo siyo DC ni hao waliomuagiza kufanya aliyoyafanya,na waliotoa Amri hiyo sina sababu ya kuwa taja,
Mimi ninawajua...
Wewe unawajua....
Watanzania wanawajua....
Dunia inawajua......

Kulumbana na Dc ni kupoteza lengo katika Halmashauri yetu mpya na nzuri tuliyopewa na Wananchi wakati wa uchaguzi 2015.

Wakati Ubungo kuna kampeni ovu Inayo ongozwa na DSO UBUNGO kwa maana ya kuwarudisha CCM majimboni na kwenye kata.....
Mimii ninawaomba kumpatia ushirikiano DC kwakuwa ni mtu mwelewa kwakiwango fulani, ni jambo hili tu Mabosi zake walilenga kumfitinisha na Viongozi wa Halmashauri.

Aidha nimepokea pole na Hongera za Watanzania nje na ndani ya Ubungo

Masaa 48 polisi Mbezi, yamenifanya nikamilishe "kukaa ndani" Mahabusu zote za Dar, nilisha kaa mahabusu 15 na Magereza manne(4), ilikuwa imebakia mahabusu 1 ya Mbezi polisi, tena kwa makosa ya kisiasa, hivyo nimemuhaidi OCD MBEZI POLISI kupeleka vifaa vya usafi.

*MWISHO*
Ninapenda kuutarifu Umma wa Watanzania ndani na nje ya Ubungo kuwa Nimeanza safari rasmi ya kutafuta haki dhidi ya sheria hii kandimizi ya ma Dc na ma Rc, haijalishi nitafika au la.
*Moyoni nimeweka Nadhiri ya kuwa kiongozi wa Mwisho wa kisiasa aliyechaguliwa kutendewa sivyo kwa kisingizio cha sheria kandamizi* na hata kama safari hii kuna nitakao wagusa, basi ni kwa sababu itahitajika mifano tu. Lakini nia ni mimi kuwa muhanga wa mwisho.

Na Boniface Jacob
Mstahiki Meya
Halmashauri ya ubungo
 
Everybody knew for sure, that the DC could not have acted that way on his own will! Mniombee, watanzania mniombee! Anayekuweka jela ni kuwa anakutakia kifo! --- "Akwendele ekomelo, akwendela warumbe" methali ya kiganda
 
Mmmmmmh

Huyu meya anayejifanya gangwe akubali kiurahisi hivi:eek:

Kuna jambo, aweke na proof basi tuone.

Awamu hii hata ambaye yupo upinzani atabadilika tu. Eeeeeeh hongera kwake kwa kuelewa kuwa kuna sheria.

Magufuli oyeeeee
 
1. Nimepata ujumbe wake kwa walio nifikishia kuwa, anakiri tukio la namna ile si Zuri, na ametoa pole na masikitiko yake kutoka Moyoni.

2. Kwa sababu hao walio na Mamlaka juu yake walitaka afanye vile, asinge fanya kama alivyo agizwa ni dhahiri ingekula kwake Mazima, hivyo alikuwa anatetea Kitumbua chake.

mleta mada inaonyesha kuna kama kichaa kinamuanza hivi.mwenye namba ya mirembe hospital aweke hapa.yaweza msaidia just in case kinawaka
 
Hakuna kitu kigumu kama kumsamehe aliyekupora haki yako, basi kwa kuwa umemsamehe kutoka moyoni kwa kweli ubarikiwe sana Kiongozi. Kama sisi waumini wa Kikristo tumefundishwa kusamehe mara saba sabini.
 
Meya Wa Ubungo Unachosema Ni Upumbavu, Kama ingekuwa ni Tukio la siku moja au Kiongozi Mmoja Ningekuelewa, Unachofanya hapa ni wapa cover wanaotumika Kuwahujumu. Hii Tabia, Unataka Uwaatangazie Wanaofanya haya na Watanzani kuwa Its not a big deal!

Kumbe sisi tunahatarisha Maisha Yetu kutetea Uhuru haki na Demokrasia yenu, Tumeumbuka eh! Forgive, kwenye siasa za hujuma? What a foolish strategy! Na Walioharibu Shamba Mbowe wasamehe, Na waliomweka Lema ndani kwa kuota ndoto na Kuzuia dhamana Wasamehe! Na waliowakamata Maya wa Arusha kwa Kwenda kutoa Pole wasamehe, Na Waliovuruga mazishi ya Ndesamburo wasamehe! Hiki Ndicho CCM wanachokitaka kuona asiyejali akichukuliwa inchi, Ndio maana Wanachukua Maili nzima.

Naona sasa Kutetea Wapinzani Tanzania ni Kupoteza Muda! May be wako hapo tu kutaka sifa na Mashangingi na Mimi nipoteze Muda Kuwatetea! Si wazimu huo?
Umesema Kuna Waliomtuma, Kuna waliomtuma, kama dhana ni kusamehe, The hell Kama wewe ni bingwa wa Kusamehe na sio Mnafiki, Ulitakiwa Ufocus Kuwasamehe na Kuwaombea Msamaha waliomtuma huyu mkuu wa wilaya.

Unaongea Kama hayo Masaa 48 walikufukizia Moshi wa Mwenge wa, "Uhuru" usiku kucha wow! Masikini wa Shetani.

The hell am out of here!
 
Back
Top Bottom