Uchaguzi 2020 Meya Boniface Jacob asimamishwa kufanya kampeni kwa siku 7 baada ya kuzidisha dk 5 kwenye mkutano wa kampeni

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,480
9,241
MGOMBEA ubunge Jimbo la Ubungo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amesimamishwa kuendelea na kampeni, akidaiwa kukiuka kanuni za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Mgombea huyo, kwa mujibu wa Msimamizi wa Jimbo la Uchaguzi Ubungo, Beatrice Dominic, amesimamishwa kwa kipindi cha siku saba.

Beatrice amesema jana kuwa mgombea huyo amesimamishwa baada ya uamuzi huo kutolewa na kamati ya maadili: “Nilikuwa kwenye kikao tangu asubuhi, kamati ndiyo iliyotoa maamuzi, hivyo namsainia barua sasa hivi mjumbe wa mgombea nimpatie,” alisema Beatrice.

Akifanya mahojiano na Kipindi cha Front Page cha +255 Global Radio, leo asubuhi, Boniface amesema: “Nimesimamishwa kufanya kampeni kwa siku saba na NEC kwa madai ya kuzidisha dakika tano za kuzungumza baada ya muda wa kampeni (saa 12 jioni). Kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi kosa hilo sipaswi kuzuiliwa, labda kuonywa na kuomba radhi.

“Wanaosema mimi ni kinara wa figisu ndani ya Chadema ni waoga, ninasimamia taratibu na misingi ya chama, ukienda kinyume na chama lazima nitasimama kukitetea chama, kwa hiyo lazima tu utasema nina figisu lakini siyo kweli.

“Mimi ninashirikiana sana na viongozi wa CCM, Waziri Mkuu alikuja Kilungule, Mheshimiwa Kigwangalla, Ummy Mwalimu, Mheshimiwa Dkt. Magufuli kwenye kusaini mkataba wa Ujenzi wa Ubungo Interchange alinipa nafasi ya kuzungumza kwenye jukwaa.

“Viongozi wanaoleta dharau kwenye kazi kwa kweli tumekuwa wakali kulinda heshima zetu, wanaokuja kwa nidhamu tunafanya nao vizuri, amekuja naibu Waziri wa Maji tumezunguka naye kwenye miradi yote. Hata kama ingeachwa siku moja, bado wananchi wa Ubungo wananihitaji tu kujua nagombea basi. Kwa hiyo ‘issue’ ya kampeni sio kitu.

“Wakinichagua miradi niliyoianza tutaimalizia, vitu ambavyo nimefanya katika jimbo hilo kama shule, zahanati na barabara ni alama ambazo nimeziacha,” alisema Boniface ambaye aliwahi kuwa meya wa Ubungo na kuongeza kuwa wananchi wa jimbo hilo wanafahamu utendaji kazi wake tangu akiwa diwani na hatimaye mbunge.

Agosti 29, mwaka huu, Boniface alipokea barua ya Msimamizi wa Uchaguzi kumuengua kugombea ubunge jimbo hilo, kwa maelezo ya kushindwa kukidhi masharti. Boniface alirejea kwenye mchakato wa kugombea ubunge jimbo hilo, Septemba, mwaka huu, baada ya NEC kukubali rufani 13 na kuwarejesha katika orodha ya wagombea ubunge 13 baada ya kupitia nyaraka walizowasilisha.

Kati ya rufani hizo ni kutoka majimbo ya Singida Magharibi, Madaba, Ilemela, Namtumbo, Bagamoyo, Liwale, Tunduma, Bukene, Ubungo na Kigamboni. Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Charles Mahera, ilisema kuwa tume imechambua vielelezo, nyaraka na maelezo ya warufani na warufaniwa vilivyowasilishwa ili kuhakikisha inatenda haki wa mujibu wa sheria.
 
Why always Boniface Jacob and the Returning Officer of Ubungo Municipality? Is there any hiding issue between the two that we don't know? I guess...
 
Tulisha shauri muda mrefu. Chadema huyo mama hana nia nzuri na nyie. Hata mkishinda hata watangaza... Watch out!!!!
 
watu wakisema NEC ni tawi la CCM wananuna, angekuwa mgombea wa CCM angethubutu hata kutoa onyo? yale yale ya ndoa ya CCM na TLP.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom