Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
MEYA AZINDUA UKARABATI NA UCHONGAJI WA BARABARA MANISPAA YA KINONDONI LEO
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Boniface Jacob leo Alhamisi 19/05/2016, amezindua mkakati wa ukarabati na uchongaji wa barabara za Manispaa ya Kinondoni.
Baada ya mvua kunyesha na kuharibu Miundombinu ya barabara katika maeneo mbalimbali katika Manispaa ya Kinondoni, Mstahiki Meya ametoa greda la Manispaa ya Kinondoni kwa ajili ya kuanza operesheni maalum ya ukarabati na uchongaji wa barabara zilizoharibika.
Ukarabati na uchongaji wa barabara hizo umeanza leo Alhamisi 19/05/2016 katika Kata ya Mbezi.
Mstahiki Meya amesema ili kupata greda hilo inatakiwa Waheshimiwa Madiwani na Wenyeviti wa Serikali za mitaa kuchukua jukumu la kuwahamasisha wananchi wao waweze kuchangia fedha kwa ajili ya mafuta kwa ajili ya kuweka kwenye greda ili kufanya zoezi hilo la ukarabati na uchongaji wa barabara.
Greda kwa siku 1 linatumia lita 100 za mafuta (diesel) kiwango ambacho ni Shilingi 160,000/=.
"Mwananchi yeyote au Kamati inaweza kulipata greda baada ya kulipia kiasi hiko cha pesa, greda linapatikana muda wowote kwa mtu yeyote, ni kufanya malipo kwanza kisha unapata greda" ameongeza Meya Boniface.
Wananchi wanatakiwa kuhakikisha wanaandika barua na ipitishwe na diwani au Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa eneo husika.
Kwa kuanza leo Alhamisi 18/05/2016, Mhe. John Mnyika (MB) Madiwani na wananchi wake wa Goba wameomba greda lianze ukarabati na uchongaji wa barabara kwenye jimbo la Kibamba, litakuwepo huko kwa siku 10.
Leo tarehe 19/05 ni Mbezi, tarehe 20/05/ - 22/05/2016 ni Msigani, tarehe 22/05 - 24/05/2016 ni Kwembe, tarehe 26/05 - 28/05/2016 ni Goba na tarehe 28/05 - 2/06/2016 ni Saranga na Kimara.
Baada ya hapo Majimbo yatakayofuatia ni Majimbo ya Kawe, Ubungo na Kinondoni pamoja na Kata zake.

- Ukarabati na uchongaji huu maalum wa barabara za Manispaa ya Kinondoni hazihusiani na miradi ya Maendeleo ya matengenezo ya barabara kwa bajeti iliyotengwa 2016/17 kama njia ya kudumu ya Uboreshaji wa barabara zote za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.