Meya apiga marufuku watu kufa kwenye mji wake

BigBaba

JF-Expert Member
Feb 7, 2017
1,908
9,040
Ni marufuku na ni kosa kisheria kwa mtu yeyote kufa kwenye mji wa Le Lavandou, Ufaransa
Mwaka 2000 meya wa mji wa Lavandou nchini Ufaransa Mayor Gil Bernardi alilazimika kupitisha sheria ndogo yenye lengo la kupiga marufuku watu kufa katika mji huo. Na yeyote atakayevunja sheria hiyo (atakayefariki) atapata adhabu kali. Sababu za meya huyo kupitisha sheria hiyo ni kutokana na kukataliwa ombi lake la kupewa sehemu mpya ya kuzikia wafu baada ya kujaa kwa sehemu ya makaburi iliyokuwa ikitumika awali.

Sasa ole wako ufie kwenye mji huo, utakiona cha mtema kuni!

1d6227a30f931b31adc5fa4b68ddac28.jpg
 
Attachments

  • FB_IMG_1493230924206.jpg
    FB_IMG_1493230924206.jpg
    19.6 KB · Views: 36
Hahaha...meya ameomba eneo la kuzikia akanyimwa....sasa hapo haijakaa vzr nani amemnyima?nadhani walikengeuka ktk hiyo sheria ingesema hakuna kuzikwa.....suala la kufa halipingiki.
 
Hiyo meya ingekuwa bongo angekuwa meya kutokea chama gani na meya wa wapi??
 
Wazungu wana uwezo mzuri wa kufikiri
Huwa wanajiuliza maswali tata sana na kisha kuyatafutia majibu sasa haya majibu yakipatikana ndio ugunduzi wenyewe sasa

Hapa kuna habari ya meya kukataa watu kufarikia jimboni,meya kajipanga ila kama utawaza juujuu utaona kama meya ni wazimu

Maeneo yamejaa na serikali imegoma kutoa eneo sasa ni marufuku kufia hapa na atakayefia hapa atakiona cha mtema kuni maana yake nini??

Meya hatarusu shughuli yoyote ya maazishi jimboni kwake, kwa wale watakaofiwa na wapendwa wao watafute mahala pa kuwazikia nje ya hili jimbo!!
Hii lazima itazua tafrani kubwa sana kwenye hili jimbo na matokeo yake ni kwamba meya atapewa eneo na serikali kwa ajili ya kuzikia na kesi itakuwa imeisha
huyu jamaa ana akili nyingi
 
Walete hiyo sharia tanzagiza ili ccm wakome kuua wapinzani (Mawazo nk) vinginevyo wakiua tu mpinzani,wavunje mijengo yao ya ccm isiyo lipiwa kodi, wapate viwanja vya kuzikia.
Manake kila balaa ccm inaelekeza kwa wapinzani.hata wanayosababisha ccm wanasema,chadema,mbowe,kama ni kweli kwanini wanakataa mzungu kumtafuta Ben ? Ccm mleteni Ben,mnajua alipo,hamuwezi kupinga msaada wa kumtafuta bila kujua mnahusika kwa upotevu wake,mnaogopa /mnakwepa kuumbuka.
 
hatari sana
 
Dah!
Kupatwa kwa Kifo!
Hapo ukiugua tu hata homa, unasafirishwa nje ya Mji.
Shikamoo Meya wa Le Lavandou.
 
Back
Top Bottom