Mexico: Watu 73 wamefariki na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa vibaya, walikuwa wanakinga mafuta ya bomba lililopasuka

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,643
2,000
Tlahuelilpan, Mexico. Idadi ya watu 21 waliofariki kutokana na mlipuko wa bomba la mafuta nchini Mexico yafikia 73, na wengine zaidi ya 70 wamejeruhiwa vibaya baada ya bomba la mafuta kulipuka na kushika moto nchini Mexico.

Inaaminika kuwa mlipuko huo ulitokea baada ya bomba hilo kuharibiwa na watu wanaodaiwa kuwa wezi wa mafuta katika mji wa Tlahuelilpan, jimbo la Hidalgo.

Maofisa wanasema mamia ya watu walikuwa waking'angania kuchota mafuta kabla ya moto kuwaka ghafla.

Wezi wa mafuta, wanaofahamika kwa jina ‘huachicoleo’ wameongezeka katika baadhi ya jamii ya Wamexico.

Serikali imesema wizi huo uliligharimu taifa hilo takriban Dola 3 bilioni mwaka jana.
Rais Andrés Manuel López Obrador, ambaye aliingia madarakani Desemba amezindua msako mkali dhidi ya wahalifu hao

Picha za televisheni zilionyesha moto mkubwa na watu walioungua vibaya kutokana na moto huo.
 
titimunda

JF-Expert Member
Nov 26, 2014
7,607
2,000
Dah haya majanga yangekua yanatokea bongo , sijui nini kingekua kinatokea !

Poleni wafiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Bongo mbona yanatokea sana.miaka ya nyuma kuna wanakijiji walienda kuiba mafuta kwenye Tipa lililooinduka,msela mmoja akaenda kuchomoa betri gari likawaka moto maraia wakadedi wakutosha,wizi wa mafuta pale kurasinu unafanyika sana tu tena kuna cartel kabisa.sijui kwa sikuhizi za karibuni kama umedhibitiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
34,454
2,000
Tlahuelilpan, Mexico. Idadi ya watu 21 waliofariki kutokana na mlipuko wa bomba la mafuta nchini Mexico yafikia 73, na wengine zaidi ya 70 wamejeruhiwa vibaya baada ya bomba la mafuta kulipuka na kushika moto nchini Mexico.

Inaaminika kuwa mlipuko huo ulitokea baada ya bomba hilo kuharibiwa na watu wanaodaiwa kuwa wezi wa mafuta katika mji wa Tlahuelilpan, jimbo la Hidalgo.

Maofisa wanasema mamia ya watu walikuwa waking'angania kuchota mafuta kabla ya moto kuwaka ghafla.

Wezi wa mafuta, wanaofahamika kwa jina ‘huachicoleo’ wameongezeka katika baadhi ya jamii ya Wamexico.

Serikali imesema wizi huo uliligharimu taifa hilo takriban Dola 3 bilioni mwaka jana.
Rais Andrés Manuel López Obrador, ambaye aliingia madarakani Desemba amezindua msako mkali dhidi ya wahalifu hao

Picha za televisheni zilionyesha moto mkubwa na watu walioungua vibaya kutokana na moto huo.
Vyuma vimekaza hadi Mexico City.
 
Top Bottom