Mexence Melo: Mabilionea wajao Tanzania watatokana na Teknolojia

Regent

JF-Expert Member
Oct 9, 2020
2,306
3,550
Maxence Melo Mkurugenzi wa JamiiForums na Mwanzilishi mwenza akiwa kwenye Interview CloudsTzv amesema:

"Mabilionea wanaokuja sasa hivi Tanzania watatokea kwenye teknolojia, hivyo Serikali iweke mazingira wezeshi"

Je, huu msemo unaendana na wakati? ''Kama munaitaka mali mutaipata shambani''

Una nini cha kuchangia?
 
Wakuu labda jamaa aliongea hivyo kwa lugha ya kibiashara zaidi.

Au kusema mabilionea watatokea kwenye technology haina maana sisi ndo tuwe chanzo cha iyo technology

hayo maneno aliyosema mkuu max yana tafsiri pana..

Mabirionea kutokea kwenye technology inaweza ikamaanisha mabilionea kutumia na kutegemea sana technology kama sehemu ya kazi zao,

Hata kwenye hiko kilimo pia technology inaweza kuwa applied na ikawa kama mbadala kwenye iko kilimo mnachokiita cha kisasa na hence kikaleta mabilionea lakini kwa kutumia technology
 
Kauli yake ali trace kutokea kwa mabilionea wakubwa Duniani Bill nawenzie So far amemaanisha DOTCOM VERSION OF BILLIONAIRE masuala mazima ya INFOTECH.
 
Maxence Melo Mkurugenzi wa JamiiForums na Mwanzilishi mwenza akiwa kwenye Interview CloudsTzv amesema:

"Mabilionea wanaokuja sasa hivi Tanzania watatokea kwenye teknolojia, hivyo Serikali iweke mazingira wezeshi"

Je, huu msemo unaendana na wakati? ''Kama munaitaka mali mutaipata shambani''

Una nini cha kuchangia?
Hii serikali inayoweka vpn?
 
Kilimo cha kutegemea jembe la mkono na mvua hakilipi especially when you take into consideration of global warming.
Kwa nchi za africa kama kweli tunataka ubilionea Basi tupambane kwenye kilimo cha kisasa tuuze nje. Kuhusu technology kwa africa mazingira si rafiki sana
 
Maxence Melo kauli uliyotoa ni sahihi lakini Afrika tuko nyuma sana kwenye issue ya science na technology
Kwa nchi za africa kama kweli tunataka ubilionea Basi tupambane kwenye kilimo cha kisasa tuuze nje. Kuhusu technology kwa africa mazingira si rafiki sana
Na tunarudishwa nyuma zaidi , kutokana na syllabus tunazotumia plus mbinu za kusoma

Hadi leo watu wanahangaika na kusolve past papers ili wafaulu mitihani , innovations itatoka wapi?
 
Mabilionea wanatokea kwenye siasa na wataendelea kutokea kwenye siasa. Hakuna kada inayolipa bongo kama siasa.
 
Kwa nchi za africa kama kweli tunataka ubilionea Basi tupambane kwenye kilimo cha kisasa tuuze nje. Kuhusu technology kwa africa mazingira si rafiki sana
Ngumu sana kilimo kututoa kwenye umaskini na kutengeneza mabilionea.
 
Teknolojia ni akili pana na wakati mwingine akili ndogo tu ya kubadili kilichotumika zamani kukiweka kuwa cha kisasa.

Kwa kimombo innovation. Mfano majiko ya mkaa na kupikia mkaa mtu akaongeza akili akatengeneza jiko la gesi na umeme kwa kupikia na kubanika kisasa huku ukiokoa muda, nyumba za cement zikageuka kuwa tailizi, makochi ya mito yakageuka kuwa sofa.

Hivyo teknolojia inawezekana sana tu hata sisi tukiamua na tusipoamua hata hicho kilimo tunachojifusi nacho na wakati hatulimi kisasa kitachukuliwa na wajanja alafu watuletee chakula kilicho tayari na kupakiwa vizuri na sisi tununue.
 
Back
Top Bottom