MeTL wakanusha kukamatwa kwa sukari iliyofichwa

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL), leo imekanusha taarifa zilizoripotiwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari siku ya jana na leo kwa baadhi ya Magazeti kuwa imeficha sukari ambayo inatakiwa kwa matumizi ya kawaida majumbani.

MeTL wamedai taarifa za aina hiy hazikuzingatia ukweli na zinachochea hasira za wananchi katika kipindi hiki kigumu cha kupungua kwa sukari ya majumbani katika soko la hapa nchini.

"Mohamed Enterprises pamoja na kuwa kampuni ya biashara kimataifa ikiuza bidhaa za kilimo na kununua, pia inajishughulisha na utengenezaji wa bidhaa ambazo zinahitaji sukari ya kiwandani." ilisema taarifa yao.

"Bidhaa hizo ni pamoja na vinywaji baridi. Ndio kusema katika muda wowote ule tunahitaji kuwa na akiba ya kutosha ya sukari hiyo kwa ajili ya matumizi ya viwandani" iliongeza sehemu ya taarifa yao.

Katika kufafanua zaidi, MeTL walisema:

Tunapoagiza sukari ama kwa mahitaji ya viwanda vyetu kampuni ya Mohamed Enterprises hufuata taratibu zote za Nchi.

Aidha sukari tani 2,990 zilizokutwa Bandari Kavu (ICD) ya PMM iliyopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam, si mali ya MeTL bali ni mali ya kampuni ya Tanzania Commodities Trading inayomilikiwa na Murtaza Dewji.

Sisi tunachoelewa ni kwamba mzigo ulikuwa njiani kuelekea Uganda, lakini kutokana na uhaba wa sukari hapa nchini, Serikali iliruhusu mzigo huo kubaki nchini na ili kuingiza sokoni mara moja kati ya Mei 12 na Mei 13.

Tulifuata taratibu zote ikiwemo Mamlaka husika za Nchi Bodi ya Sukari, Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), na vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama.

Kwa mantiki hiyo, si sahihi kusema sukari tunayoiagiza nchini ni ya kiwango duni wakati hukaguliwa na mamlaka zote husika za kiserikali ikiwemo TFDA na TBS.

Pia kauli kuhusu sukari kuagizwa toka Brazil na kufanyiwa ‘repackaging; Nchini Dubai suala hilo ni jambi la kawaida

Kampuni yetu huagiza sukari kutoka kwa wauzaji wa sukari wa Dubai kutokana na lojistiki zinavyoruhusu.

Kuagiza sukari kutoka Brazil na kuisafirisha hadi Tanzania ni siku 50 hadi 60 kwa njia ya meli, lakini kutoka Dubai ni siku 7 tu, kwa mtu anayefanya biashara lazima ataagiza sukari kutoka Dubai, kuna maslahi zaidi katika hesabu za kibiashara.

Wafanyabiashara wote wanaojua biashara walioko karibu na Dubai hufanya hivyo na sisi si wa kwanza kuagiza sukari kutoka kwa wauzaji wa Dubai.

Ofisi zetu zipo Dar Es Salaam Tanzania, na uongozi upo wazi, laiti kama tungelitafutwa na kuulizwa tungeliweza kutoa maelezo yaliyojitosheleza, kuepusha mikanganyiko na kuweka habari katika mizania inayostahili.

Tunazo nyaraka zote zinazothibitisha uhalali wake ikiwemo TRA, TFDA na Bodi ya Sukari, hivyo hakukuwa na haja kufichwa sukari hiyo kwa sababu zozote zile.

Pia, ieleweke tatizo hilo la sukari ilishaagizwa ya kutosha na itafurika nchi nzima ndani ya wiki mbili zijazo, hivyo Watanzania hawapaswi kuwa na hofu hiyo ya uhaba wa sukari.

TFDA - METL_Page_1.png

TFDA - METL_Page_2.png
 
Na bado za matumizi ya kawaida nyumbani tutapangiwa kiwango cha kuwa nacho.
 
Vibali vimetolewa tarehe 7 May 2016 lakini sukari imekuwa kwenye magodauni kwa miezi.

Kwa nini walichukua muda mrefu kupata vibali vya TFDA?

Waliomba lini vibali vya TFDA?

Je, nani mmiliki wa Bandari Kavu (ICD) ya PMM? Kama wamiliki siyo Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL), kwa nini Press release inawasemea kampuni ya Tanzania Commodities Trading inayomilikiwa na Murtaza Dewji

Kama suala ni uharaka wa kupata mzigo kutoka Dubai, kwa nini sukari inakuja haraka halafu inakaa kwenye magodauni kwa miezi bila kutumika? Nini msingi wa uharaka?

Kwa nini upeleke sukari Uganda wakati nchi ya uganda inazalisha sukari ambayo mpaka inakosa soko la ndani kiasi kwamba imepelekea kuwepo na marumbano na Kenya ambayo imezuia sukari kutoka Uganda kuingia Kenya.

Habari ipo hapa;
Uganda produces enough sugar for its citizens and some surplus for export

Kuna maswali mengi ukisoma vizuri hii press release!
 
Kuna ubaya wa kiwanda kununua stock kwa ajili ya matumizi yake? Kiwanda sio kama family ambayo hufanya manunuzi kwa wiki ama siku. . Kiwanda ni kitu kinachofanya manunuzi kwa awamu na kwa mpangilio maalumu
Mchezo wanaofanya ni kuagiza sukari kwa kigezo cha kutumika kwenye viwanda vyao vya kutengeneza juice. Aina hii ya sukari huwa hailipwi kodi. Kisha huigeuza na kuiuza kama sukari ya biashara. Magufuli alishayajua haya yote.
 
Hapo kuna ukakasi, vyombo vya habari/mitandao haijafafanua uzuri juu ya hili sakata.

1. Jana tuliambiwa ni sukari iliyotunzwa kwa ajili ya shughuli za viwandani
2. Magazeti ya leo yanasema ni sukari iliyotakiwa kusafirishwa kwenda Uganda
3. Jamaa nao wanakuja na taarifa kwamba kweli ilikuwa isafirishwe lakini kwa sababu ya uhaba wa sukari nchini imebidi ibakizwe.

Hapa ufafanuzi wa kina unahitajika.
 
Safi Sana.Nilitahadharisha hapahapa siku tatu zilizopita. Na serikali ijiandae kwa kesi nyingi kwa sababu ya kufanya maamuzi ya pupa.

Watu wanatoa matamko barabarani kwa kutafuta sifa za ajabu ajabu tu halafu taifa linaingia hasara

By the way aliyetoa tamko la kukamata sukari na kugawa bure ni mzoefu wa kugawa Samaki za watu Bure kisha serikali kushtakiwa na kulipa fidia

Ni mzoefu wa kugawa nyumba za Serikali kiholela.

Hili la Sukari nilitahadharisha. Wako wapi wale waliotoa mapovu niliposema watu watasema ni za viwandani halafu wataumbuka kwa kukurupuka?
 
Magufuli karusha jiwe gizani ukisikia ng'weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee fahamu tayari kaumia mtu
Hivi mnadhani serikali yenye vyombo vya kuipatia taarifa utalinganisha na wakesha mtandaoni??? acheni hizo hakuna kesi wala hukumu hapa.mbona swala la kuagiza sukari ya kuchanganyia juzi hatimaye ikipakuliwa inafanyiwa rebagging ni issue ya kawaida sana na ya muda mrefu.Huo ni uhujumu uchumi tuuu, huwezi kufanya biashara za kihuni na kuifanya serikali eti zezeta.imekula kwenu
 
Nilisema hapa na narudia kusema MeTL hawajaficha sukari ambayo ilitakiwa kuuzwa sokoni. Kwa taarifa isio rasmi kuanzia Leo sukari inaanza kupokelewa bandarini takribani container 390. Wiki ijayo sukari itakuwa imejaa nchi nzima.
 
Vibali vimetolewa tarehe 7 May 2016 lakini sukari imekuwa kwenye magodauni kwa miezi.

Kwa nini walichukua muda mrefu kupata vibali vya TFDA?

Waliomba lini vibali vya TFDA?

Je, nani mmiliki wa Bandari Kavu (ICD) ya PMM? Kama wamiliki siyo Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL), kwa nini Press release inawasemea kampuni ya Tanzania Commodities Trading inayomilikiwa na Murtaza Dewji

Kama suala ni uharaka wa kupata mzigo kutoka Dubai, kwa nini sukari inakuja haraka halafu inakaa kwenye magodauni kwa miezi bila kutumika? Nini msingi wa uharaka?

Kuna maswali mengi ukisoma press release!


Kwani kuna Deadline ya kufanya hayo?Kuna sheria gani wamevunja? Watu wazima wamevuliwa nguo .Tuliwaonya lakini hamkusikia.
 
vyombo vyetu vya habari navyo ni tatizo kuuu,hawajishughulishi kutafuta ukweli wa jambo husika wao ni kukumbilia tu kuandika.jana star tv waliandika kwenye ukurasa wao wao facebook kua daraja la mwalimu nyerere liko kinondoni.ni mizuka tuu si weredi tena
 
Wambie watoto wako wasibakize sukar , mkikamatwa na ziada ya sukari mtatumbuliwa!!
 
Back
Top Bottom