Methali: mwenzako akinyolewa...!?

Nadhani hata Kenya nao wana msala kama huu. Ile standadi geji yao ishaanza kudaiwa na wachina na dhamana ilikuwa bandari ya Mombasa
 
kiukweli bado hatujafanya kazi vizuri pamoja na angalau kuwa na hali nzuri ya usalama ukilinganisha na kongo na kuwa na fursa zote za uchumi ikiwemo bandari na kumiliki zaidi ya asilimia 20 ya maji baridi na kusifika kuwa afrika tuna mlima mkubwa na binadamu wa kwanza aliishi tanzania.
achilia mbali tanzanite ipo tanzania na zabibu tamu inayolimwa kiasilia ipo dodoma inayouzwa bei mbaya kuliko ya afrika kusini lakini bado hatujafanya vizuri tukizidiwa na swaziland wanaotegemea uchumi wao kwa kutega maji milimani na kuuza afrika kusini.
ili tuweza kwenda vizuri mambo makubwa mawili tunatakiwa kujituma:-
  1. tuipende nchi yetu kwa kuwa tukiipenda nchi yetu tutaweza kuipigania kwa uaminifu na kwa maarifa yote hii ni pamoja na:-
    • kuwaanda na kuchagua viongozi waaminifu na sio watawala watakaokuwa tayari kufanya kazi kwa maslahi ya taifa wakiwa na maono ya kutufikisha tunapokwenda. wakiwa tayari kushughulika na wataalamu waaminifu wasioona maslahi yao kwanza.
    • kuwa tayari kujitoa kutengeneza kizazi kinachopenda kufanya kazi na kujituma kuanzia hatua ya familia mpaka taifa
    • kujenga uaminifu katika kulinda na kusisimamia rasilimali za taifa.
    • kupenda vya kwetu kwanza ili tutengeneze soko la ndani kwa bidhaa zetu na kusaidia kujenga uchumi wa ndani kwa kununua bidhaa zetu.
    • kuthaminiana na kupendana ikiwa ni pamoja na mazingira ya usalama wa raia na mali zao.
  2. kushiriki kikamilifu katika uchumi hii ni pamoja na:-
    • kuongeza pato la taifa kwa kuongeza uuzaji bidhaa nje ya nchi tukitumia fursa zilizopo. bado tantrade hawajafanya vizuri katika eneo hili kwa kuwagusa wazalishaji wa zaidi ya mjini na wenye mitaji midogo na wengi hawajui hata hili shirika linafanya nini.
    • kuwa tayari kuwaelekeza wenzetu nini tunafanya na hasa kwa masoko ya nje mfano miaka ya nyuma nilikutana na msafirishaji mmoja wa alizeti nje ya nchi nikamwomba atusaidie na sisi tuweze kufanya hiyo biashara na yeye kwa mdomo akakubali kwa kuwa wahitaji walikuwa wanataka tani 3000 wakati yeye uwezo wake wa kukusanya haufiki tani 800 lakini hakuonyesha ushirikiano. vilevile nikiwa field katika benki moja nilikutana na mzee mmoja alikuwa amepata soko la kupeleka ngozi india lakini mtaji hana na bado hakuwa tayari kutoa mchango wapi anapeleka. sasa hii imewatokea wengi na watu wanapenda waone kila siku unawalilia shida na sio utoke kwenye shida zako hatuwezi fika vizuri.
    • taifa liweke mazingira mazuri kwa vijana na kushiriki vizuri kwa uchumi si swala la wao kuunda vikundi vya watu kumikumi kisha tunawapa 500,000/- haziwezi kuwafikisha kokote watapiga kalata na ziishe.
tukifanya hivi tunaweza kuwa na utumiaji mzuri wa miundo mbinu iliyowekwa na nchi ikapata mapato yanayoweza kusaidia urejeshaji wa mikopo waliochukua. mfano kama fursa za biashara zitakuwepo utumiaji wa train ya mwendo kazi na barabara zilizojengwa utaleta tija na serikali zitaweza kulipa madeni waliokopa kwa uwekezaji waliofanya.
 
Tatizo sisi watu weusi tumetawaliwa na hofu sana. Kila tukifanyacho hukifanya kwa hofu, kila tujadilipo jambo hata km ni la kujenga asilimia kubwa ya mawazo huegemea kwenye kushindwa.

Hv hii hali hutokana na hofu tuu au kuna chuki na hira ndani yake? Au ndio kusema tunaombea kushindwa ili baadae tuje kujigamba kuwa tulisema watafeli (atafeli)/hafiki mbali?

Badilisha ufikiria & mtazamo wako kuwa positive. Mataifa yaliyo endelea hayakuwa na mitazamo hasi.
 
Tatizo sisi watu weusi tumetawaliwa na hofu sana. Kila tukifanyacho hukifanya kwa hofu, kila tujadilipo jambo hata km ni la kujenga asilimia kubwa ya mawazo huegemea kwenye kushindwa.

Hv hii hali hutokana na hofu tuu au kuna chuki na hira ndani yake? Au ndio kusema tunaombea kushindwa ili baadae tuje kujigamba kuwa tulisema watafeli (atafeli)/hafiki mbali?

Badilisha ufikiria & mtazamo wako kuwa positive. Mataifa yaliyo endelea hayakuwa na mitazamo hasi.
Kwahiyo tuendelee kukopa toka China bado tunakopesheka? Mfano wako wa hofu kwenye hili sio valid.. Angalia hicho kikaragosi utaelewa
IMG-20180910-WA0073.jpg
 
Back
Top Bottom