Messi vs Ronaldo: Nani zaidi?

Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,257
353
Messi better than Ronaldo - Cole


Chelsea's Joe Cole says Barcelona's Lionel Messi is ahead of Manchester United star Cristiano Ronaldo as the best player in the world.

Source: BBC Sport|Football

Mimi binafsi nakubaliana kabisa na maneno ya Joe Cole hapo juu, Messi anatisha!

Nakumbuka wakati wa Euro 2000, kulikuwa na maswali na malumbano mengi sana kati ya wadau wa soka waliokuwa wanajiuliza Zinedine Zidane na Louis Figo ni nani mkali zaidi. Hawa wachezaji enzi hizo walikuwa katika kiwango cha juu mno. Niliwafanyia wadau uchambuzi yakinifu kuwaelezea hawa wafalme wawili wa enzi hizo na kuonekana dhahiri kuwa nani alikuwa zaidi.

Moja ya kitu ninachokumbuka, vyombo mbalimbali vya kimataifa baada ya ile michuano walikuwa wanacomment kuwa Louis Figo ni mchezaji bora kabisa katika Euro 2000, ILA UKIMUWEKA ZIDANE PEMBENI. Maana yake ilikuwa ni kwamba, wakati Figo ndio alikuwa The world best footballer, Zidane alikuwa katika level nyingine baada ya ubest, sasa kwa kiingereza hakuna neno linalomchambua mtu aliye zaid ya best. Maana kuna good, better na best. Labda extremely best !!! Ilikuwa kila Zizzou alipokuwa anacheza, commentators walikuwa wanatafuta maneno ya kumfit km, wonderful, classic, excellent, extraordinaly na mengineyo ya mfano huu…

Sasa, nirudi kwenye mada kuu. Wakati dunia nzima saizi ya wapenzi wa kandanda aka soka ikiwa inajiuliza ni nani mkali kati ya Crhistiano Ronaldo na Leonel Messi, mimi nikiwa kama mchambuzi niliyebobea katika soka la kimataifa nakuletea kwa kina uwezo wa hawa mastar wawili wanaoishika dunia ya soka kwa sasa.

Nitafanya outlining ili nieleweke vizuri. Hapa nitaweka point kumi na mbili muhimu za kuwalinganisha halafu mwisho nitaconclude. Nikianza na Christiano Ronaldo,

CR ana sifa zifuatazo,


  1. Physical appearance (urefu 1.86m au 6.1ft) inampa advantage kama mchezaji katika position yoyote.
  2. Anaweza kutumia miguu yote miwili vizuri kabisa, hii inamfanya amudu kucheza nafasi nyingi bila tabu yoyote.
  3. Ana uwezo mkubwa wa kutumia kichwa. Hii inamfanya aweze vizuri kufunga magoli ya kichwa hapa pointi ya kwanza (urefu) pia inamwongezea hii advantage.
  4. Ana uwezo mkubwa wa kupiga faulo. Ikiwa ni pamoja na kuwa ni mpiga penati mzuri achilia mbali penati kadhaa muhimu ambazo ashawahi kukosa.
  5. Ana uwezo mkubwa wa kuipasua ngome ya wapinzani, hii nikiwa namaanisha ni mwepesi wa kupiga chenga na pia ana spidi kali inayomfanya awe tishio kubwa kwa wapinzani
  6. Anauwezo mkubwa sana wa kufunga magoli akitokea upande wowote wa uwanja na kwa mguu wowote. So far ashafunga goli 22 za Laliga katika mechi 19, msimu uliopita alifunga magoli 26 katika Laliga pia 4 za champ ligi. Mpaka sasa Ronaldo ashafunga magoli 65 katika mechi 64 akiwa Madrid.
  7. Ana uwezo wa kucheza kama kiungo wa pembeni, pia anauwezo mkubwa wa kucheza km mshambuliaji wa kati. Pia CR anaweza akacheza nyuma ya mshambuliaji wa mwisho. Hii inamfanya awe flexible sana na formation nyingi za kiuchezaji.
  8. Ni mzuri sana wa kupiga pasi za mwisho. Kwenye statistics so far kwenye Laliga ametoa pasi 6 na pia kwenye UCL ametoa pasi 2.
  9. Ni mwepesi wa kuflustrate timu yake inapokuwa down, hii inamfanya asiweze kuwika katika mechi ngumu. Hii inamfanya awe amefunga mara chache sana anapocheza mechi ngumu.
  10. Hajaonyesha kiwango chochote cha ajabu akiwa na timu yake ya taifa.
  11. Pamoja na kuwa anatumia miguu yote, CR si mzuri sana akiwa anashambulia akitokea kushoto.
  12. Hana uwezo kabisa wa kusaidia defence ya timu yake.

Nikija kwa Leonel Messi.


  1. Physical appearance yake (urefu 1.69m au 5.58 ft) haimpi advantage kubwa ya kucheza namba nyingi uwanjani na ndio maana alivyoanza soka na Barca alitumika zaidi kama winga wa kulia.
  2. Anauwezo mkubwa sana wa kutumia mguu wa kushoto, ni mwepesi sana, hii inamfanya kutoonekana udhaifu wake wa kuwa na uwezo mdogo sana wa kutumia mguu wa kulia.
  3. Uwezo wake wa kutumia kichwa ni mdogo kwa sababu ya kimo chake, ila kutokana na wepesi wake mara chache amekuwa akifunga magoli makali sana kwa kichwa, km goli la 2 na Man U fainali ya UCL 2009 aliweza kuruka juu na kuwaacha magiant Vidic na Ferdinand na pia alishafunga goli kwa kuruka juu na kuusindikiza mpira kwa mkono katika mechi na Espanyol, ni goli sawa kabisa na alilofunga Maradona maarufu kama mkono wa mungu.
  4. Si mpigaji wa mara kwa mara wa faulo, ila mara kadhaa amekuwa akifunga kwa faulo. Pia si mpigaji wa penati, imetokea mara chache sana kwa Messi kupiga penati.
  5. Ni extremely dangerous anapokuwa na mpira, anauwezo mkubwa sana wa kupiga chenga, ni mwepesi sana na pia anapokuwa na mpira ni vigumu sana kwa mabeki kujua anachotaka kukifanya, kama kutoa pasi, kupiga shuti au kupiga chenga. Hii inafanya awe hatari mno hata anapobaki na mabeki hata kama ni wawili au watatu.
  6. Ana uwezo mkubwa sana wa kufunga akitokea upande wowote wa uwanja, ila kwa kutumia mguu wa kushoto. Ana goli 18 za Laliga katika mechi 19, msimu ulioisha alifunga magoli 34 katika mechi 34 za LaLiga, alifunga magoli 48 katika michuano yote na Barca na pia ameshafunga magoli 6 ya UCL ktk mechi 6 msimu huu.
  7. Japokuwa Messi anatumia sana mguu wa kushoto, ila anauwezo wa kucheza namba zote za mbele. Anauwezo wa kucheza kama kiungo wa pembeni, ni hatari sana anapokuwa anashambulia tokea kulia, pia anauwezo wa kucheza nyuma ya mshambuliaji, mshambuliaji wa mwisho au kama attacking midfielder. Ni hatari sana anapokuwa anacheza kama kiungo wa kushambulia, nyuma ya mchambuliaji mmoja au wawili.
  8. Ni mpiga pasi za mwisho bora kabisa katika ulimwengu wa sasa. So far ana pasi za mwisho 13 katika Laliga.
  9. Messi yupo humble, ni mchezaji aliyetulia asiye na makeke, na hata timu yake inapozidiwa si rahisi kumuona ameflustrate.
  10. Messi pia bado hajaonyesha uwezo mkubwa kwenye timu ya taifa.
  11. Japokuwa hatumii kabisa mguu wa kulia, Messi ni hatari sana anaposhambulia kutokea kulia. Hii imefanya udhaifu wake wa kutotumia mguu wa kulia usionekane.
  12. Si mzuri kabisa kwenye kusaidia defence.

Kwa kufuatilia hizo pointi 12, naamini utakuwa umeweza kupata picha halisi ya hawa wanasoka wawili wanaowika sasa katika medani ya soka. Katika maeneo mengi uwezo wao unaelekeana, na kama ni kuzidiana ni katika kiwango kidogo.

Pamoja na hayo, Messi ni bora zaidi kwa sababu anaskills ya hali ya juu sana ukilinganisha Ronaldo. Kwakiwango kikubwa, Ronaldo kasi yake ndiyo humfanya awe hatari anapokuwa na mpira, lakini Messi skills yake ndiyo inayomfanya awe hatari sana, maana anapokuwa na mpira huwezi jua anataka kufanya nini, na ndio maana ukiangalia katika upigaji wa pasi za mwisho Messi anatisha mno. Kuna vigezo vingine vingi tu vinavyowahusu, ila kwa kuwa maelezo yanakuwa marefu nimeamua kuishia hapo maana hili si gazeti.

Hapa ni sawa comparing Ferrari na Porsche....kwanza Ronaldo ni mchezaji ghali sana duniani akiwa ameuzwa toka man u kwa mkwanja mnyamwezi mil 131....
wote wameshachukua kiatu cha uchezaji bora wa FIFA....

Tukianza na finishing kwa kutumia maguu....Messi ni mkali wa kumalizia hasa kwa guu lake ma mavi na mara nyingi amekuwa akishambulia tokea upande wa kulia nafasi ambayo alianza kuitumia tangu pep achukue timu...mara nyingi messi umaliziaji wake hauna makosa hata chembe na hasa timu ikiwa ina shine naweza kumpa rate ya 9/10..

Lakini wakai messi ni mtumiaji mzuri wa akili analikaribia lango Ronaldo yeye ni mtumiaji wa nguvu sana na ni mmaliziaji mzuri wa guu lake la kulia na kwa matumizi yake ya nguvu amekuwa si mfungaji mmaliziaji mzuri na nampa rate ya 8/10

Umaliziaji kwa kichwa...
Messi yawezekana akawa ni mbovu kinoma noma katika umaziliaji kwa kichwa na mpoja ya magoli yake bora ambayo alibahatisha kumalizia kwa kichwa ni lile la final na man u nampa rate ya 6/10

Ronaldo ni mkali wa vichwa na haogopi kutia kichwa na hufunga kwa kichwa hata kwa umbali mrefu na ukizingatia ni mtumiaji mzuri wa nguvu..nampa 8/10(kumbuka kuna wakali wa vichwa kama patrick kluivet ambao wana rate ya 10/10 na yazidu zidane mwenye rate ya 9/10)

Kwenye free-kicks...
wote ni wakali wamipira mfu messi kama kawaida yake anatumia akili sana kwenye upigaji wa mipira mfu na ana kawaida ya kupiga kwenye nyavu ndogo mfano mzuri angalia el-classico ya juzi....nampa messi 8/10
Ronaldo ni mkali wa powerfull freekicks na amekuwa mkali tangu alipokuwa man u na hata real madrid hapa ronaldo nampa rate ya 9/10

Dribbling na kontrol
Messi ni guru wa ku dribble hapana shaka kwa hili ni mkali wa kukimbia na mpira uku akikatiza kati kati ya misiutu ya mabeki nampa 10/10
Ronaldo ni mkali lakini sio kivileeeee yeye mar nyingi anatumia ile chenga ya tangulia twende na kukimbiza na ana luzi controll sana anapokuwa yupo katika eneo la hatari nampa 9/10


Skills na teknic
Messi ni magic wa skill japo hajamfikia dinho umaarufu wa skills zake ni kwamba huwa zinaleta madhara kwenye timu pinzani nampa 10/10 unlike ronaldo ambae ni show man anapiga skills nyuma ya mstari wa nusu uwanja ambapo haendi popote ni mzuri kumuangalia lakini hana impact kwa timu kwa hizo skills zake...nampa 9/10

team play
messi amnekuwa maarufu hasa akiwa na viungo bora kabisa kwa kipindi hiki xavi na iniesta kombinenga hii huwa ni ya kuogopewa na ndio maana watu wengi wanasema messi si bora kwa sababu anacheza na watu kama hao..nampa 9/10

ronaldo kama kawaida ni selfish anjulikana hivyo na mara nyingi amekuwa hata akipigiwa boo na mashabiki bernabeu nampa 6/10

phsical
messi ni kadogo kadogo hakana nguvu kivilee na kama mnavyojua alizaliwa akiwa njiti..ni mzuri sana ukiwa nae ana kwa ana...ndio maana defenders always wanambwaga chini..nampa 7/10
Ronaldo ni fiziki anaonekana ni mtu anaenyanyua vitu vizito na kula vizuri na inamsaidia kupiga mprikwa kwa mbali nampa 9/10


kitakwimu tangu ronaldo aende real 2009

Messi

2009-10
Games: 64
Goals: 49
Assists: 11

2010-11
Games: 61
Goals: 51
Assists: 22

2011-12
Games: 68
Goals: 74
Assists: 27

Ronaldo

2009-10
Games: 39
Goals: 33
Assists: 7

2010-11
Games: 65
Goals: 56
Assists: 16

2011-12
Games: 73
Goals: 77
Assists: 16



hitimisho
messi ni mkali tena kwa kila game iwe ngumu au laini..messi hakabiki anabadilika badilika anaweza kucheza kati kama namba 8 anaweza kurudi mpaka nyuma anachukua mpira na kusambaza kwa winga na mido wa kati na anaweza pia kukimbia na mpira toka nyuma mpak akafunga..lakini ronaldo ni mkali wa mechi zake..zikija meschi muhimu haonekani....

jumla
messi 69/70
ronaldo 68/70
Unajua, ushabiki wa msimu mmoja utawatoa nishai. Msiwe mnaongea bila stats jamani...........

International Appearances and goals (Hapa hatuangalii Messi kafanya nini akiwa under 21/20);

Ronaldo 53 matches 16 goals (1 goal in 3.3 matches)
Messi 18 Matches 10 goals (1 in 1.8 matches)

Ndio maana nasema Ronaldo anaweza UK tu, subiri tuone kama atafurukuta euro 2008 mwezi ujao tu!!

Umeangalia stats za magoli ya timu msimu huu tu, angalia hayo magoli Ronaldo kafunga timu gani mbovu za UK. Halafu angalia record ya Ronaldo na Messi tangu waingie first team tuone nani ana return nzuri zaidi;

Ronaldo 238 matches 91 goals (average return 1 in 2.615 games)
Messi 102 matches 39 goals (average return 1 in 2.615 games)
Hapo return yao sawa. Ila average ya Ronaldo imepanda msimu huu tu kwasababu kacheza na timu mbuzi za UK. Na kumbuka Messi mechi nyingi kaingia substitute. Nakupeni homework mtafute wakati Ronaldo ana mechi 100 au 102 hapo Manu je alikuwa na magoli mangapi?

CL msimu huu (Messi akiwa injured)
R 11 7 (1.57)
M 9 6 (1.5)

I could go on and on, ila kama we kweli unajua mpira, utaelewa kwamba Ronaldo anatamba ligi ya UK tu ambapo madefender wengi ni wachovu wa butua butua.....very average hawana skill (defender usipokuwa skillfull utazuiaje mchezaji skillfull? Tofauti na Europe au world football. We umeshawahi kumwona Ronaldo anamsumbua Glichy? Ashley Cole unaweza kusema 50/50, ila madefender wengine anawasumbua). Nje ya UK Ronaldo is an average player. Yaani mara mia hata Torres yuko proven.

Halafu tafuteni mechi ya Barca vs Getafe muone mambo Messi alifanya.....Ronaldo hawezi hiyo hata siku moja.

Mkitaka assists;

http://www.fcbarcelona.com/web/engl...07-08/estadistiques/jugadors/Messi/fitxa.html

Messi kamfanya hata Thierry Henry aonekane mbovu. Na hapo ndio utajua ukiwa Uingereza sio kwamba uta-guarantee ufanikishe Europe. Hata wakati Thenry yuko Arsenal, Europe alikuwa anachemsha.....na ameonekana average Barcelona, alikuwa average Juventus. Ndo maana nasema Messi can fit any league comfortably.

Angalia statistics award

CHRISTIANO RONALDO

TEAM HONOURS WITH MAN UNITED
Barclays Premier League: 2006-2007, 2007-2008
Runner Up: 2005-06
FA Cup: 2004
Runners Up: 2005, 2007
Carling Cup: 2006
FA Community Shield: 2007
UEFA Champions League: 2008

HONOURS WITH PORTUGAL
UEFA European Championship 2004: Runner-up
2006 FIFA World Cup: 4th place

INDIVIDUAL HONOURS AND AWARD
Professional Footballers' Association
PFA Players' Player of the Year: 2007, 2008
PFA Young Player of the Year: 2007
PFA Fans' Player of the Year: 2007, 2008
PFA Premier League Team of the Year: 2005-2006, 2006-2007, 2007-2008
PFA Fans' Player of the Month: October 2006, February 2007, November 2007, January 2008

BARCLAYS PREMIER LEAGUE
Barclays Player of the Season: 2006-2007, 2007-2008
Barclays Player of the Month: November 2006, December 2006, January 2008, March 2008
Barclays Golden Boot: 2007–08
Barclays Merit Award: 2008
Football Writers' Association Award: 2007, 2008

MANCHESTER UNITED FC
Sir Matt Busby Player of the Year: 2003-2004, 2006-2007, 2007-2008
Manchester United Players' Player of the Year: 2006-2007, 2007-2008
Manchester United Goal of the Season: 2007-2008

PORTUGAL
Portuguese Sports Personality: 2006
Portuguese Footballer of the Year: 2007

EUROPE
UEFA Team of the Year: 2004, 2007
UEFA Champions League Top Scorer: 2007-08
UEFA European Championship 2004: Team of the Tournament
European Golden Shoe - Soulier d'Or: 2007-2008
European Footballer of the Year - Ballon d'Or:
2nd place: 2007
Onze d'Or
2nd place: 2007
Bravo Award: 2004

WORLD
FIFA World Player of the Year
3rd place: 2007
World Soccer Player of the Year
3rd place: 2007
FIFPro Special Young Player of the Year: 2005, 2006
FIFPro World XI: 2006-2007

LEO MESSI

ARGENTINA NATIONAL TEAM

FIFA U-20 World Cup: 2005
Copa América 2007 second place

WITH FC BARCELONA
La Liga:2004-05, 2005-06
Supercopa de España: 2005, 2006
UEFA Champions League: 2005-2006

PERSONAL HONOURS
Golden Ball: FIFA U-20 World Cup: 2005
Golden Boot: FIFA U-20 World Cup: 2005
Golden Boy: 2005
Bravo Award: 2007[42]
World Soccer Young Player of the Year: 2006[43], 2007[44]
Olimpia de Plata: Argentinian Player of the Year: 2005
FIFPro World Young Player of the Year: 2006
FIFPro World XI: 2007
EFE Trophy: Best Ibero-American Player in La Liga: 2006-2007[45]
Best foreign player in La Liga: 2007[46]
Copa America Best Young Player: 2007[47]
France Football Player of the Year:
3rd place: 2007
World Soccer Footballer of the Year:
2nd place: 2007[48]
FIFA World Player of the Year:
2nd place: 2007[49]
SI Latino's 2007 Sportsman of the Year: 2007[50]

Messi award nyingi kazipata akiwa Junior Player
Hata Barca walivyochukua CHAMPS LEAGUE alicheza game 6 na kufunga goli 1 but Ronaldo kacheza game 11 na kafunga magoli 8 na assist 1 na ndio TOP SCORER
 
Messi better than Ronaldo - Cole

Messi and Ronaldo went head-to-head in the Champions League
Chelsea's Joe Cole says Barcelona's Lionel Messi is ahead of Manchester United star Cristiano Ronaldo as the best player in the world.

Cole said Messi's form in Barca's Champions League semi-final defeat by United settled the debate.

"Ronaldo's been fantastic but in the semi-final Messi showed he's the top man," said Cole, who will face Ronaldo in next week's Champions League final.

"He is only 20 as well, imagine how good he will be in the next 10 years."

Messi has been linked with a £80m move to Chelsea, and Cole admitted he would be delighted if the speculation proved to be true.

"If we could sign him, I'd love to play alongside him," he added.

Cole's comments will help to crank up the atmosphere ahead of Wednesday's final between United and Chelsea in Moscow.


Source:bbc.co.uk

Mimi binafsi nakubaliana kabisa na maneno ya Joe Cole hapo juu, Messi anatisha!

hicho ni kizazi kipya cha soccer
 
hawa jamaa wote wanatandaza soka.ila tukija katika fair play,lionel mess ni zaidi.huyu jamaa ronaldo ana hasira sana,pia vimajivuno kwa mabli,ila huyu dogo mess yeye ni fair play tu.mess zaidi
 
For the TEAM PERFORMANCE RONALDO NI ZAIDI BUT KWA KUMILIKI MPIRA MESSI ZAIDI
Labda kwa kuwa bado mdogo MESSI anapenda kupiga chenga/kumiliki mpira badala ya kufunga au kutengeneza nafasi kwa wenzake
RONALDO-Ana kasi,anapiga freekick kali,anatengeneza nafasi nyingi kwa wenzie
 
Messi better than Ronaldo - Cole

Messi and Ronaldo went head-to-head in the Champions League
Chelsea's Joe Cole says Barcelona's Lionel Messi is ahead of Manchester United star Cristiano Ronaldo as the best player in the world.

Cole said Messi's form in Barca's Champions League semi-final defeat by United settled the debate.

"Ronaldo's been fantastic but in the semi-final Messi showed he's the top man," said Cole, who will face Ronaldo in next week's Champions League final.

"He is only 20 as well, imagine how good he will be in the next 10 years."

Messi has been linked with a £80m move to Chelsea, and Cole admitted he would be delighted if the speculation proved to be true.

"If we could sign him, I'd love to play alongside him," he added.

Cole's comments will help to crank up the atmosphere ahead of Wednesday's final between United and Chelsea in Moscow.


Source:bbc.co.uk

Mimi binafsi nakubaliana kabisa na maneno ya Joe Cole hapo juu, Messi anatisha!

Mkubwa UNANISIKITISHA sana unavyochukua mawazo ya CASHLEY na kuyakubali.
Cole amepewa shida sana na Ronaldo akiwa ARSENAL na alikuwa anampania sana Ronaldo ,sifikirii kama Cole anaweza kumkubali RONALDO
Watu kama MESSI,KAKA,SCOLARI,CAPELO,LIPI,TORES,CARVARLO wanamkubali RONALDO kwa wakati huu
 
Mkubwa UNANISIKITISHA sana unavyochukua mawazo ya CASHLEY na kuyakubali.
Cole amepewa shida sana na Ronaldo akiwa sana na alikuwa anampania sana Ronaldo ,sifikirii kama Cole anaweza kumkubali RONALDO
Watu kama MESSI,KAKA,SCOLARI,CAPELO,LIPI,TORES,CARVARLO wanamkubali RONALDO kwa wakati huu

Cashley Cole sio Joe Cole, ni Ashley Cole. Anyway, ninaposema Messi zaidi ni kwa mtazamo wangu, kila mtu anaweza kuwa na chaguo lake.
 
ni sawa na kufananisha usingizi na kifo....messi ni maestro.
diego armando maradona hakuwa mjinga kusema messi ndo mrithi wangu katika soka.
sasa kama mnamkubali maradona basi myakubali na maneno yake.

un messi que club
 
tena ni dhambi kwa mungu kumfananisha ronaldo na messi...
baada ya mechi ya manchester na barca ile ya old trafold washabiki wa manchester waliingia uwanjani kwenda kumlaki messi kama masiya, je kwa nini hawakwenda kwa ronaldo?
 
For the TEAM PERFORMANCE RONALDO NI ZAIDI BUT KWA KUMILIKI MPIRA MESSI ZAIDI
Labda kwa kuwa bado mdogo MESSI anapenda kupiga chenga/kumiliki mpira badala ya kufunga au kutengeneza nafasi kwa wenzake
RONALDO-Ana kasi,anapiga freekick kali,anatengeneza nafasi nyingi kwa wenzie

Nakubaliana nawe mimi kama mchezaji enzi zangu ingawa bado mara moja moja hapa uwa nipo mchezoni tena,kuna mpira wa collective(teamwork) na individual skills.Katika individual skills both wako sawa katika kumiliki mpira ingawa ukiwachunguza sana utagundua kwamba Ronaldo ni muoga wa kuumia hivo yuko tayari muda wote kukuachia mpira kwa maana nyingine enzi yetu asingecheza kwani watu wanapiga tiktak kichwani kwako,Messi akubali kuachia mpira kiraisi na ndio waajentina walivo(usikubali kuachia mpira wako)lakini wareno ni usiniguse(dont touch me)ingawa wapo wareno waliokua wanang'ang'ania mpira kama Figo.
Katiaka collective(teamwork)hapa ndio Ronaldo anakua bora sasa,kwa sababu za uoga wake basi anakua anawahi kutoa mpira ili achukue nafasi nyingine asiyobana apige chenga adui akiwa mbali hivo anaonekana anashiriki katika majukumu pamoja ya kitimu.Here now,you can separate boys from men!Na ndio hicho kinachowatofautisha kati ya Messi na Ronaldo.Asanteni
 
Tunawalinganisha vipi...? I.e Wamezisaidia vipi timu zao both Clubs na National Teams...au mnaangalia nani anapiga chenga nyingi na kumiliki mpira?
 
hapa tunaangalia uwezo binafsi pindi wanapokuwa uwanjani,hilo suala la kufanikisha klabu au national timu kufanya vizuri mie naona mchango wake ni mdogo sana,mfano hata mchezaji aliyecheza mechi chache lkn kwa kuwa alikuwepo katika hiyo club au national team na ikafanikiwa kutwaa taji basi utaambiwa kuwa huyo mchezaji nae alisaidia hiyo timu kutwaa hilo taji.so what we discuss here ni uwezo binafsi.
 
hapa tunaangalia uwezo binafsi pindi wanapokuwa uwanjani,hilo suala la kufanikisha klabu au national timu kufanya vizuri mie naona mchango wake ni mdogo sana,mfano hata mchezaji aliyecheza mechi chache lkn kwa kuwa alikuwepo katika hiyo club au national team na ikafanikiwa kutwaa taji basi utaambiwa kuwa huyo mchezaji nae alisaidia hiyo timu kutwaa hilo taji.so what we discuss here ni uwezo binafsi.

Mfano mzuri angalia jinsi Ronaldo alivyoisaidia Manchester kufika hapa ilipo Season hii na season iliyopita...kati ya magoli yote timu iliyofunga season hii amefunga magoli 41...now huo ni mchango mdogo?
 
wote wana skills zinazo fanana na uwezo wao wa kupenya ngome unafanana, tofauti ni Ronaldo muoga na Messi ni shoka......si rahisi kumnyang'anya mpira Messi, as a team player Ronaldo anamzidi Messi
 
ebwana kana-naka-nsungu ebu nisaidie,huyu jamaa icadon ni mshabiki wa manchester au vipi?halafu yaonekana hajaelewa maelezo yangu
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom