Messi njoo England angalau wiki tu...

Afrika Furaha

JF-Expert Member
Dec 16, 2010
329
9
Messi kwa kweli anaitafuna La Liga kama vile ni Ligi Kuu ya Shangazi yake, kila mwisho wa wiki ana mabao mawili au matatu, na Barca hawapitishi wiki bila kupiga mtu 4 au zaidi. Nadhani Messi aende kucheza England ajaribu kukabwa na mabeki wenye ROHO MBAYA wa English Premier League, tuone kama kweli anaweza kuchomoza na mabao kila wiki akicheza viwanja vya White Hart Lane, Old Trafford, Goodson Park, Stamford Brigde n.k. Mwenzie Ronaldo ameshakomazwa na Ligi hiyo kiboko duniani
 
Kashacheza na Arsenal, Man U na Chelsea na kapiga bao sana, yote hiyo haitoshi?
 
Ishu sio kucheza nao mechi moja mbili halafu unaachana nao, hapa nasemea aje EPL afunge magoli kama anavyofunga La Liga tuone . . . dogo ana kipaji lakin nadhan akacheze pia England na aonyeshe makeke kama anavyofanya Spain
 
England kuna timu moja tu inayocheza mpira wa aina ya Messi...

Sio lazima kucheza England kuwa mkali - mbona hawa hamkuwauliza: Ronaldinho, Zidane, Ronaldo wa Ukweli...
 
Messi ni noma hata akila Engalnd. Tofauti ya ligi hizi ni: Spain-more technocal, Italy-more tactical, England-more physical. Hata hivyo Spain kuna timu kama Getafe na Espanyol ambazo ni very physical and intimidating kuliko hata timu za England na bado Messi anawapiga goli. waulizi Madrid majuzi, baada ya kuona mambo magumu wakaamua kuwa very physical na bado aliwafanya kitu mbaya sana!
 
Messi ni noma hata akija England. Tofauti ya ligi hizi ni: Spain-more technocal, Italy-more tactical, England-more physical. Hata hivyo Spain kuna timu kama Getafe na Espanyol ambazo ni very physical and intimidating kuliko hata timu za England na bado Messi anawapiga goli. waulizi Madrid majuzi, baada ya kuona mambo magumu wakaamua kuwa very physical na bado aliwafanya kitu mbaya sana!
 
naona kama vile arsenal wameanza kumtafuta mchawi!mechi muhimu kama hiyo ya barca navuta pumzi!
 
Messi ni noma hata akija England. Tofauti ya ligi hizi ni: Spain-more technocal, Italy-more tactical, England-more physical. Hata hivyo Spain kuna timu kama Getafe na Espanyol ambazo ni very physical and intimidating kuliko hata timu za England na bado Messi anawapiga goli. waulizi Madrid majuzi, baada ya kuona mambo magumu wakaamua kuwa very physical na bado aliwafanya kitu mbaya sana!

Kwa physical game, timu za Spain ni nyanya sana, huwezi fananisha timu yoyote ya Spain kwa timu za England kwa physical game . . . na isitoshe Messi haonekani uwanjani mechi zote walizocheza Barca na Chelsea. R. Madrid haiwezi kucheza physical game wakati huo sio mpira wao, walikuwa wanajaribu tu kitu wasichokijua. Pengine Mourinho sasa ndo atajaribu kuwafundisha physical game, na itawachukua muda sana kuiweza. Messi hawezi kuonekana ukicheza 60% physical game plus 40% brain-Use game, hii inatokana na umbile lake pia. Anakipaji sawa hatukatai, ila ana mapungufu yake pia. Jaribu kuangalia game ya Argentina vs Ujeruman ktk WC 2010 au Chelsea vs Barcelona pale darajani ambapo ngoma iliisha 1 - 1 ndo utajua Messi unamkabaje
 
aende kucheza italy uone kama anachacharika kama anavofanya sasa
 
England kuna timu moja tu inayocheza mpira wa aina ya Messi...

Sio lazima kucheza England kuwa mkali - mbona hawa hamkuwauliza: Ronaldinho, Zidane, Ronaldo wa Ukweli...

Hao uliowataja kwa blue colour ukiwaangalia physically utaona wasingeweza kupata tabu sana kui-fit ligi ya England, na Ronaldo wa Ukweli ndo nani?? Unatumia vigezo vipi kusema huyo ndo Ronaldo wa ukweli??
 
Kuna masuala ambayo hayana mjadala, Ronaldo wa kweli katika soka ni El Fenomeno...

Hata Ronaldo de Assis Moreira alilitambua hilo ndio maana akaitwa Ronaldinho Gaucho...
 
Kwa physical game, timu za Spain ni nyanya sana, huwezi fananisha timu yoyote ya Spain kwa timu za England kwa physical game . . . na isitoshe Messi haonekani uwanjani mechi zote walizocheza Barca na Chelsea. R. Madrid haiwezi kucheza physical game wakati huo sio mpira wao, walikuwa wanajaribu tu kitu wasichokijua. Pengine Mourinho sasa ndo atajaribu kuwafundisha physical game, na itawachukua muda sana kuiweza. Messi hawezi kuonekana ukicheza 60% physical game plus 40% brain-Use game, hii inatokana na umbile lake pia. Anakipaji sawa hatukatai, ila ana mapungufu yake pia. Jaribu kuangalia game ya Argentina vs Ujeruman ktk WC 2010 au Chelsea vs Barcelona pale darajani ambapo ngoma iliisha 1 - 1 ndo utajua Messi unamkabaje

Messi ni mchezaji aliyekamilika (complete player). Hana mapungufu. Hakabiki. Hazuiliki. Subiri akutane na timu yako ya Man U.
 
Kuna masuala ambayo hayana mjadala, Ronaldo wa kweli katika soka ni El Fenomeno...

Hata Ronaldo de Assis Moreira alilitambua hilo ndio maana akaitwa Ronaldinho Gaucho...

Kwa taarifa tu ni kwamba Ronaldinho alikubali kubadili muonekano wa jina lake kwa nia ya kutojichanganya jina tu na Ronaldo de Lima kwa vile wote wanatoka taifa moja, na wala si vinginevyo. Hayo hayana mjadala kwa mtazamo wako, lakin si kwa kivigezo. Naanza kupata picha labda wewe ni Man Utd ndio maana ile Ronaldo kuondoka inakuuma mpaka leo . . . pole sana
 
[SIZE=4 said:
Jabulani: Aisee, kumbe na wewe upo England !

Aisee ktk jibu lako, kuna kitu kimoja tu kimenigusa . . . nimewaza kwa nini umejiita jina hilo? Unajua maana yake?? Umewahi kusikia wimbo wenye title ya hilo neno??
 
Messi ni wa kawaida mno hafikii hata robo ya Cristiano Ronaldo. Akienda England halafu akutane na time kama Stoke City, Bolton, Blackburn na Fulham week in week out hawezi kumaliza mwaka ataishia kuwa kama Reyes aliekuwa Arsenal. Timu nyingi za EPL zinaweza kumpoteza. Kwenye mechi na Germany WC 2010 alipotezwa kabisa na akina Bastian na Khedira. Kule Spain at the moment anafanya vizuri kwa sababu ya mpira wa kule na wachezaji wa Barca wamemaster passing game na pia mabeki pinzani hawana tough game kama EPL. Sidhani kama ataweza kufanya dribblings zake akikutana na hizo time nilizozitaja hapo juu, akijaribu ataishia kuwa majeruhi three quarters of the season.
 
Humu kuna watu wabishi sana. Yaani watu wanabishana mpaka na makocha wa timu wanazozishabikia. Rejeeni wanayoyasema Maurinho, Fergusson, Wenger na wengineo kuhusu Messi. Halafu kuna wengine wanataka kumfananisha Ronaldo wa ukweli na Ronaldo wa kuchakachuliwa!
 
Messi ni mchezaji aliyekamilika (complete player). Hana mapungufu. Hakabiki. Hazuiliki. Subiri akutane na timu yako ya Man U.
Kwa nini Messi anaperform vizuri akicheza na XAVI/INIESTA/SERGIO akiwa kwao Argentina mchovu tofauti na kina Zidane,Ronaldo,KAKA &Ronaldinho?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom