Messi na Ronaldo, nikiitwa kwa Mungu baba nikafa sijamuona mtoto...

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
Kama sio kombe la dunia basi hakuna kitu ambacho Leo Messi na Cristiano Ronaldo wamekiacha , hawa viumbe wamefanya kila la umuhimu katika soka wala hilo halina mjadala kabisa.

Jamaa wametawala dunia kwa zaidi ya miaka 13 katika jukwaa moja la soka, hawa ndugu wamefanya hata ambao hawafuatilii mpira waanze kuupenda, hata dada zetu ambao hawana muda na mpira wanajadili jinsi Ronaldo anavyovutia kimuonekano mbele ya Leo Messi…

Hawa jamaa wameigawa dunia katika pande mbili kuu hakika walitupa chanzo cha ubishi na stori kwa zaidi ya miaka 10, wametupa namna mbili ya kumtathimini mchezaji kwanza kipaji chake pili kujituma kwake, Messi anaaminika na kipaji chake lakini Ronaldo kipaji kiasi na upambanaji wa kutosha.

El Classico ilikuja kua mechi maarufu zaidii duniani kisa wao , kila rekodi iko upande wao kisoka hakika jamaa wameletwa kwa sababu maalumu….

Kitu kilichobaki kwao ni kombe la dunia pekeee yaani hapa ndio penye uchawi mkubwa, Diego Maradona na wachawi wengine wa soka wa zamani kombe la dunia linawapa jeuri, kina Pele kilichobaki kwao ni kombe la dunia ndio maana mpaka leo tunawajadili katika daraja moja la Messi na Ronaldo.

Kama sio kombela dunia Maradona kamzidi nini Messi ? ni wazi hakuna anazidiwa hadi idadi za mechi timu ya taifa , bahati wa Ronaldo ni kwamba hana presha kubwa sababu taifa lake halijawahi chukua kombe la dunia..

Jamaa wanacheza la mwisho mwaka 2022 pale Qatar wanakwenda kutimiza maandiko kabisa, ni wazi watakua wamechoka kidogo na je kama kipindi wako moto wameshindwa je watachukua wakiwa wakongwe ? hilo linaweza lisiwe shinda kwa maana timu ina wachezaji 11 je ni nani atalibeba kati yao ? atakae lichukua ndiye atamzika mwenzake mazima.

Hawa ndugu walifanya mpaka tuwe tunatukanana wakati wao wanaingiza pesa lakini sote tunaongea lugha moja , umebaki ukweli tu na ushabiki sababu lazima uchague mmoja hata wao saivi wanapendana…

Je itakuaje siku wanatangaza kustaafu hawana kombe la dunia awe mmoja wao au wote kabisa ? , ipo wazi jamaa hawahitaji kombe ili wadhiririshe kwamba wamekuja kwa sababu moja tu na wako peke yao.

Kombe la dunia lina hadhi yake ndio maana mpaka leo Diego Maradona anakelele nyingi lakini alilibeba 1986 , Messi hajachukua Copa America na Argentina lakini hata ukiwauliza wao watataka alete kwanza kombe la dunia hata huko Ureno hawajawahi chukua kombe la dunia ivyo Ronaldo ndio tumaini..

Baada ya kombe la dunia 2022 ndipo kila mtu atatoa mtazamo wake je ni nani bora wa muda wote na katika historia ya mpira kwa ujumla..? Nikiitwa kwa mungu baba nikafa sijamuona mtoto mpeni shahada la msalaba aliweke ubavu wangu wa kushoto ….
 
1-Lion king 🇦🇷💪🏿
2-Yo soy el diego Armando(Golden boy) 🇦🇷💪🏿
3-Pele🇧🇷
4-Cr7 🇧🇫---Zinedine zizzou 🇫🇷
5-Johan cruyff 🇳🇱---Alfredo de stefano 🇦🇷
6-Redondo 🇦🇷
7-Iniesta 🇪🇦
8-Xavi 🇪🇦
9-De lima 🇧🇷
10-Puskas 🇭🇺
 
Back
Top Bottom