Message ya kuomba kunywa chupa moja ya wine ilivyo mpagawisha hadi akanitunuku bikira yake

Hazard CFC

JF-Expert Member
Apr 7, 2015
16,615
38,589
Story ya kweli inanihusu kwa 100%

Ni mrembo niliyetokea kumkubali toka tukiwa watoto wadogo,malkia huyu jina lake linaanza na "H" yale majina pendwa uchagani na kwingineko alikuwa na sifa zote zakuitwa mlimbwende, ni mrefu, mweupe, alikuwa na shingo ndefu kiasi na macho yake meupe hakika kwa wakati ule alikuwa msichana mkali sana (hakuwa na chura).

kwenye vijiji vyote vitatu vilivyotuzunguka (Kondeni, Karoro na Kirosha) naweza kusema yeye ndio alikuwa anakimbiza. H alikuwa na akili za darasani sana nilikuwa nampita kwenye somo moja tu la hesabu mengine yote alikuwa ananichia vumbi, hata masomo ya dini pia alinigaragaza vibaya kwani alikuwa mwanafunzi bora wa mafundisho (kipaimara) mimi nikiambulia nafasi ya tatu.

H alikuwa mpole, mwenye aibu na mpenda dini sana.

Wote tulifaulu darasa la saba na kupangwa shule moja lakini mimi nikapelekwa Agape Seminary yeye akaenda shule aliyopangwa, baada ya miezi kama sita nikatimuliwa shule kwa kosa la kwenda kuwapiga chabo watumishi wa kike wakioga, wazazi wakaamua niwe karibu yao wakanirudisha ile shule niliyopangwa awali ndipo nikakutana tena na mrembo H.

Kufika kidato cha tatu H alihamishwa shule na kupelekwa Julius Nyerere Moshi Mjini ndio ukawa mwanzo wa kupotezana.chanzo cha yeye kuhama ni kuwa mama yake alitengana na baba yake mtoto akamfuata mama.

Sikubahatika kuonana tena na H mpaka tulivyofika kidato cha tano nikiwa shule nikakutana na wanafunzi waliomaliza na H pale JK wakawa wananipa story zake jinsi alivyo,alivyoshikilia dini na wakasema hata advance karudi pale pale JK, tulivyoenda likizo nikawaomba wakirudi waje na namba yake ya simu na kweli mshikaji wangu mmoja akaniletea baharia namba chatting zikaanza rasmi.

Tulivyomaliza form six H alipangwa UDOM mimi nilipangwa UDSM tukawa tunawasiliana kama kawaida, mwaka wa pili nikatimuliwa UDSM miongoni mwa wale 46, baadae tukasamehewa lakini wazazi wakaniambia nibadili chuo nikaapply IFM nikabahitika kuchaguliwa.nikiwa mwaka wa kwanza H kaingia mwaka wa tatu UDOM ila nilimficha, mpaka anamaliza chuo alijua wote tumemaliza pamoja kumbe ndio kwanza naingia mwaka wa pili.

Niliweza kumaintain uongo huo na hukujua kitu. Mpaka kufika stage hiyo sikuwahi kumtongoza mtoto H, baada ya yeye kumaliza chuo alifanya kazi Moshi pale kwa kujitolea kwa kipindi kifupi tu akabahatika kupata ajira yake ya kwanza Dar kanisa la Msasani pale, palikuwa sijui na shirika lisilo la kiserikali la kusaidia watoto wasio na uwezo wakupata elimu na bla blaa blaa.

H akatua jiji la wahuni Dasilamu mzee baba nikasema sasa huyu malikia twiga wangu lazima nitavunja ukimya kashasogea karibu na mimi.

Kweli nikajitahidi kutupa ndoano mtoto hakatai na pia hakubali, madai ananichunguza. H alikuwa hapendi walevi na kwa kipindi kile mimi nilikuwa nakunywa pombe kuliko kitu chochote yaani ilifika stage naamka asubuhi nakunywa safari na chapati mbili, ila nilijitahidi kuficha tabia hiyo na hakujua, outing zetu mzee baba nilikuwa nagonga Sparletta kama mwinjilisti vile, tukaenda wee ukatokea msiba wa ndugu yangu Moshi na mimi nikasafiri nao kufika Moshi ndipo nilipojizolea macredit, mapoint yote kwa mtoto H akajiona hapa kapata mtu sahihi baada ya kumtumia ujumbe uliosomeka hivi:

"H TUMEFIKA SALAMA NINA UCHOVU SANA NA MAJONZI WENZANGU NAONA WANAPUNGUZA MAJONZI KWA KUNYWA POMBE NAOMBA UNIRUHUSU NINYWE HATA CHUPA MOJA YA WINE" daaaa huwezi kuamini msg hii ikanipa demu aisee ndani ya miaka zaidi ya 15 kaujumbe ka kinafki kakanipa mtoto mkalii na nilituma huo ujumbe nikiwa nakunywa konyagi.

Kurudi Dar sasa mtoto ndiyo kashakolea kwa muhuni haelewi chochote, siku moja tukiwa tunachat akaniambia kuna zawadi anataka kunipa na sitoisahau maisha yote nikawa najiuliza ni zawadi gani au huyu kachanganyikiwa.

Tukapanga siku yakwenda kulizindua penzi letu rasmi, tumefika tumekaa H kaniruhusu ninywe St. Anna nikasema kimoyomoyo hivi huyu anafikiri mimi ni wakunywa hii juice kweli?

Katika kupiga piga stor hatuna haraka tunao usiku mzima ndio akanimbia zawadi niliyotaka kukupa ni BIKIRA yangu,akaongeza najua huamini kama msichana wa zaidi ya miaka 25 ninatunza bikra yangu hadi leo kwa ajili ya mtu sahihi,nimesoma shule ya mixture,nimemaliza udom lakini hakuna aliefanikiwa kuitoa japo nimeshakua kwenye mahusiano na watu wawili lakin wote walifeli vigezo na masharti.

Nikamwangalia nikachekaa nikasema hiii huyu karuka majivu kakanyaga moto, ni kweli baada ya tendo mtoto alikuwa bikra kweli na alinipa tabu sana na ndio siku hiyo na yeye akagonga wine pia kwa furaha.

Itaendelea part 2

Jinsi alivyokuja kuujua ukweli kua mimi ni mlevi na pili bado sija graduate akaniacha kwa msg moja tu, akili yake ikawa kama haipo sawa akapata mimba, akapata cheo cha usingo maza n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom