Meseji yazua utata kwa wanandoa

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,778
MWANAMKE mmoja [32] [jina kapuni] mkazi wa Ukonga Mombasa jijini Dar es Salaam,anamlazimisha mume wake ampe talaka kinguvu kwa kushindwa kuvumilia baada ya kukuta meseji ya kimapenzi kwenye simu ya mume wake.

MWanamke huyo alimtaka mume wake huyo ampe talaka kwa kukuta meseji ambayo inamfanya akose raha kwenye nyumba yake hiyo na kudai kuwa anaweza akamfanya kitu kibaya mume wake huyo na kuomba bora apewe talaka kwa kuepusha matatizo.

MWanamke huyo alikuta ujumbe wa simu kutoka kwa hawara wa mumeme huyo, uliomfanya akose raha na baada ya kumuuliza mume wake huyo alimjibu kuwa huyo dada wakikuwa wakitaniana mara kwa mara na kumsihi mkewe huyo kuwa haikuwa kweli.

Ujumbe alioufuma dada huyo kutoka kwenye simu hiyo ulisema kuwa “ nimekumisi sana mpenzi wangu, penzi lako la jana lilikuwa zuri sana sitaweza kulisahau, naomba tuoanane kesho jioni” ulisema ujumbe huo

Baada ya kukuta meseji hiyo dada huyo alihamisha ujumbe huo kwenye simu yake na kuhamisha kwenye line nyingine ya simu ya ziada na kisha kumuuliza mumewe huyo kama alikuwa na uhusiano na mwanamke mwingine.

ALidai kuwa, mumewe huyo alikana kuwa na mahusiano na mwanamke mwingine bila kutambua kuwa mke wake huyo aliangalia ujumbe uliohifandiwa katika simu yake hiyo.

Alidai alimuuliza mara ya pili na kumwambia kuwa alikuwa anahitaji talaka yake kwa kuwa alibaini ana mahusiano na mwanamke mwingine alipoendelea kubisha alichukua simu na kumuonyesha ujumbe huo na baba huyo kukosa jibu kwa muda huo na kumwambia kuwa huyo dada walikuwa wakitaniana mara kwa mara.


Baba huyo alianza kumsihi mke wake asiwe na jazba kwa kuwa haikuwa kweli ila ni utani ambao walikuwa wakitaniana na huyo dada mara kwa mara.

Maelezo yake hayo hakuweza kuyaelewa na kumuamuru ampe talaka ili kila mtu aweze kuishi kwa amani kwa kuwa alishamuudhi kupita kiasi.

HAdi nifahamishe inaandika habari hii ilipofanya mawasiliano na dada huyo alikuwa hajapata talaka hiyo na ameondoka nyumbani kwake hapo na kwenda kupumzika kwa rafiki yake ili aweze kupata talaka hiyo.
 
Mwizi anaingia ndani ya nyumba yako...Unachoamua ni kukimbia kuiacha nyumba yako ili mwizi aishi humo, iwe yake...! huh!

Mwambie huyo mama akomae afanya uchunguzi wa ziada kwa huyo mume na huyo mwizi kwa kupitia namba hiyo ya simu ya mwizi...kukimbia atakuwa amechukua maamuz ya kiuwoga sana...au hana watoto nini?
 
hii kasheshe ..utani wa hivyo jamani ..imagine mwanamme ndo akute message hiyo kwenye simu ya mkewe ..patakuwa hapatoshi
 
Saa nyingine wanawake wa ajabu sana!!! hapo anaomba talaka naye akishakua huko ananyakua wa mwingine, naye yule akiwa kama yeye naye ananyakua wa mwingine. Kwani hao wanawake wanaoandika hizo message au wanaotembea na waume za watu kwani na wao si wake za watu? Kwa ujumla uozo uko kotekote!
 
Huyo dada hampendi huyo mwanaume au? Haina maana kukimbia ndoa kwa sababu ya sms. Ndoa zina mambo mengi zaidi ya sms kama hiyo. Aite watu wampe onyo kali mumewe waendelee kula maisha. Kuna wanawake wengine wanafanya kusudi ili ususe wao wale...think twice!
 
huyo dada hampendi huyo mwanaume au? Haina maana kukimbia ndoa kwa sababu ya sms. Ndoa zina mambo mengi zaidi ya sms kama hiyo. Aite watu wampe onyo kali mumewe waendelee kula maisha. Kuna wanawake wengine wanafanya kusudi ili ususe wao wale...think twice!


tema mate chini usiombe mkeo adili na simu zenu weeeeee
 
Huyo dada hampendi huyo mwanaume au? Haina maana kukimbia ndoa kwa sababu ya sms. Ndoa zina mambo mengi zaidi ya sms kama hiyo. Aite watu wampe onyo kali mumewe waendelee kula maisha. Kuna wanawake wengine wanafanya kusudi ili ususe wao wale...think twice!
Mkuu ustake ncheke!!
Mambo haya yanongelewa na wahusika
sio yakwenda kwenye vikao!
 
Nadhani hapo linakuja suala la mapenzi! Huyo mama ajiulize, je anampenda mumewe kweli (whether they have kids or not!!!)
Then ataweza kutoa maamuzi yake!
Halafu pia akumbuke ahadi yao ya ndoa.....!!!!!
 
tema mate chini usiombe mkeo adili na simu zenu weeeeee
..Mimi kuondoa matatizo nyumbani kuanzia januari 2010 tumekubaliana kuacha kabisa kutumia simu za mkononi...Mambo safi sana hakuna kuulizana uko wapi mbona unachelewa kurudi? sijui nimekutana sms za mahawala zako.....Kimya. Ni maisha ya ujima lakini matamu sana!!
 
Alichokosea huyo Mwanamke ni kuwa na mchecheto, alitakiwa kusubiri na kuchunguza taratibu ili awakute, kwa sababu ana ushahidi wa sms...
 
Mwizi anaingia ndani ya nyumba yako...Unachoamua ni kukimbia kuiacha nyumba yako ili mwizi aishi humo, iwe yake...! huh!

Mwambie huyo mama akomae afanya uchunguzi wa ziada kwa huyo mume na huyo mwizi kwa kupitia namba hiyo ya simu ya mwizi...kukimbia atakuwa amechukua maamuz ya kiuwoga sana...au hana watoto nini?
Agreed that will be the stupidest thing to do.
The lady should fight it on while in the house and im sure the guy will have learnt his lesson and in future he will either stop meandering or will be more discreet.
 
Back
Top Bottom