Meru: Vijana Wasiofanya kazi kuchapwa viboko 70 kila mmoja

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Wazee wa mila wakisema hayo katika sherehe zao za jadi Vijana wasiofanya kazi,Walevi,wagomvi watakutana na adhabu ya viboko 70 na alienda mbali zaidi na kusema kama kijana hana afya nzuri atakopeshwa idadi ya viboko vyake mpaka amalize dozi yake.

Kukopeshwa akimaanisha wiki hii unaweza kula viboko vitano wiki ijayo vitano tena mpaka idadi itimie ila kama una ufya yako unapokea 70 vyote kwa mpigo lengo kubwa haswa ni kumuunga rais na sera yake ya hapa kazi tu na kuhakikisha jamii inaishi kwa Amani.

Source ITV news

Unaonaje kama adhabu hii ingekua sheria ya nchi na kutumika kila sehemu?
 
Hao ndiyo wazee wa siku hizi, wana yao, yawezekana wanataka vijana wakimbie kijiji ili wao wachukue nafasi zao si mnajua ng'ombe hawazeeki maini
 
Wazee wamekosa kazi za kufanya au shida ni nini?

Hii nchi mbona kadri siku zinavyozidi kwenda kunakuwa na vituko sana.
 
Wanaunga mkono juhudi za rais kwa kuwachapa viboko vijana wasiofanya kazi
 
Kwa ambao tuko Arusha hiyo sio ajabu sababu ni sheria ya siku nyingi sana kwao, ukilewa mchana unapata Sabin I, ukipigana na mwenzio nyote mnapata kwanza sabini kisha ndio chanzo kijulikane na nimeshashuhudia wengi wakichapwa.
Kinachowezesha hilo huku mkubwa wako lazima umuheshimu sasa akiwa mzee wa mila ndio kabisaa yaani anachosema harudii mara mbili means kama wewe uko rika la miaka ishirini ukifanya kosa kubwa mnaweza adhibiwa vijana wote kijijini wa rika la miaka yako mkapewa adhabu hiyo na wale wa juu yenu mfano wa miaka 30 hiyo inafanya rika moja likiona mwenzao kafanya kosa anaadhibiwa kabla taharifa haijafika rika la juu, sasa wazee wa mila wao wakiongea inamaana sio wao watawatafuta kuwachapa ila ni rika zitachapana.
Huku imezoeleka na iko hivyo ukitembea sijui mara matusi barabarani, mara umeelewa, mara umeamua kuwapiga nyumban mke na watoto jua huna bahati kijiji kitakufundisha ukikomaa wewe mkorofi utahama mchana kweupee.
Wageni hawatuingilii labda ufanye kosa kubwa au wewe uwachokoze mbali na hapo mila zao hazikugusi wewe
 
Jamii za wafugaji ndio mila zao, yan wote ni mboko tu, kosa dogo ndo viboko 21
 
Hivi haiwezekani wakamchukua Godbless Lema na Sugu wakakae nao huko.Wangekaa nao hata mwezi ingepeneza.Utukutu wao ungefikia tamati
 
Back
Top Bottom