Meremeta & TANGOLD Revealed!

Una assume kwamba Usalama wa Taifa wao sio mafisadi.

Ukiangalia viongozi wa juu wa Usalama, hususana waliotoka kustaafu (hawa wa sasa hivi sifahamu kwa sana) wanavyo ishi na mali waliyojilimbikizia, sidhani kama mishahara yao ingetosha kufanya mavitu yao.

Tusi assume kwamba ukiwapa wao ulinzi wa mali ya Umma basi itakuwa poa.

Hata Plato ali spin alipoulizwa "nani atalinda walinzi"?
Unayosema ni kweli kabisa!!!!! Wengi ni matajiri na hatujui walipata wapi mali hawa. Kila walichonacho ni siri kwa sababu ndivyo mwana usalama Pinda alivyosema.
 
Labda anataka kufikisha post 30,000 kisha tumtumie pongezi

Usiidharau RESOLVE YANGU KWA MANENO YAKO YA KIPUUZI!
NCHI IMEUZWA!
Maswali ni mengi!
Na kama wewe uko comfortable..Well i dont know how!
Unless unajua kitakachofanyika!
TAIFA LIMEOZA!
 
Misconception of Law.

Alichokisema Zitto ni vague. Sheria hazisemi hiyo ni kazi yao Usalama. Na Wabunge wamepiga makofi bila kujijua, kama kawaida yao. Wanadhani kwamba kila kitu kinacho sound muhimu muhimu kama nishati basi ni kazi ya Usalama wa Taifa. Dead wrong.

Kama kina Zitto wanataka mabadiliko ya sheria lazima wachonge hoja zao ziwe sharper. Ningekuwa mimi Mbunge fisadi hapa ningewatoa nishai kina Zitto na hiyo pointi yao hapo. Mikataba ya Tanesco sio mikataba ya Usalama, kwa mujibu wa Sheria.

Hawa wabunge kila siku kabla ya kusema kitu inabidi wamuulize Sitta kama it's ok, as if Sitta ndio arbiter wa sheria za immunity za Wabunge. Huyo Phillip Marmo mwenyewe hajui anachokifanya. Kamwambia Slaa, Slaa unafanya jinai kutoa siri za Meremeta Bungeni. Slaa akamwambia 'nikamate.' Marmo akafyata. Alikuwa kakurupuka tu. Hawajui sheria hawa watunga sheria hawa. So pathetic!

imagine na wewe ungekuwa mbunge, halafu ukawaback up kina Zitto kusharpen hoja zao, mambo yangenyooka in a little while. Kagombee ubunge (jimbo la chenge,lowassa au karamagi) 2010. Tunahitaji michango yenu vijana (excluding vijana mafisadi maana nick names nazo zinafcha mengi).
 
Misconception of Law.

Alichokisema Zitto ni vague. Sheria hazisemi hiyo ni kazi yao Usalama. Na Wabunge wamepiga makofi bila kujijua, kama kawaida yao. Wanadhani kwamba kila kitu kinacho sound muhimu muhimu kama nishati basi ni kazi ya Usalama wa Taifa. Dead wrong!

Kama kina Zitto wanataka mabadiliko ya sheria lazima wachonge hoja zao ziwe sharper. Ningekuwa mimi Mbunge fisadi hapa ningewatoa nishai kina Zitto na hiyo pointi yao hapo. Mikataba ya Tanesco sio mikataba ya Usalama, kwa mujibu wa Sheria.

Hawa wabunge kila siku kabla ya kusema kitu inabidi wamuulize Sitta kama it's ok, as if Sitta ndio arbiter wa sheria za immunity za Wabunge. Huyo Phillip Marmo mwenyewe hajui anachokifanya. Kamwambia Slaa, "Slaa unafanya jinai kutoa siri" za Meremeta Bungeni. Slaa akamwambia "nikamateni." Marmo akafyata. Alikuwa kakurupuka tu. Hawajui sheria hawa watunga sheria hawa. So pathetic!

Sikubaliani na wewe..
Madini na nishati ni rasilimali za TAIFA!
Na kama nchi ikivamiwa leo...Watakaovamia watayachukua hayo madini na pamoja na kulipua vyanzo vya umeme ili kutupa giza watuvamie vizuri...Sasa unasema si usalama wa Taifa huo?
 
Kama ni kweli wanasema Mkapa alichukua maamuzi hayo ili kulilinda TAIFA...BASI WATUWEKEE WAZI NI KIVIPI MIKATABA HIYO YA MEREMETA ILIKUWA IKILINDA TAIFA LISIVAMIWE KAMA WANAVYOTAKA KU IMPLY.
 
Misconception of Law.

Alichokisema Zitto ni vague. Sheria hazisemi hiyo ni kazi yao Usalama. Na Wabunge wamepiga makofi bila kujijua, kama kawaida yao. Wanadhani kwamba kila kitu kinacho sound muhimu muhimu kama nishati basi ni kazi ya Usalama wa Taifa. Dead wrong!

Kama kina Zitto wanataka mabadiliko ya sheria lazima wachonge hoja zao ziwe sharper. Ningekuwa mimi Mbunge fisadi hapa ningewatoa nishai kina Zitto na hiyo pointi yao hapo. Mikataba ya Tanesco sio mikataba ya Usalama, kwa mujibu wa Sheria.

Hawa wabunge kila siku kabla ya kusema kitu inabidi wamuulize Sitta kama it's ok, as if Sitta ndio arbiter wa sheria za immunity za Wabunge. Huyo Phillip Marmo mwenyewe hajui anachokifanya. Kamwambia Slaa, "Slaa unafanya jinai kutoa siri" za Meremeta Bungeni. Slaa akamwambia "nikamateni." Marmo akafyata. Alikuwa kakurupuka tu. Hawajui sheria hawa watunga sheria hawa. So pathetic!

Kuhani,

Mara nyingi tuna confuse that which is with that which it ought to be.Sheria zenyewe nyingi ziko vague.Si zetu tu, bali hata za hao tunaowaita walioendelea. Nilikuwa nasoma kuhusu an awkward comma in the wording of the US Constitution's second amendment making big stories now, kuna sehemu wamesema wamarekani wote wanahaki ya kuwa na silaha halafu kuna sehemu nyingine wanasema wanatakiwa kuwa kwenye militia, halafu kuna vi comma viwili vitatu vimekaa katikati hapo vinaleta ambiguity kwamba wenye haki ya kuwa na silaha ni wamarekani wote au wamarekani wote walio katika militia?

Pengine muheshimiwa ndiyo anatunga au anapalilia kutungwa kwa sheria mpya zitakazokuwa sharper zaidi.

Kwani sheria yetu inasemaje na/ au inaweza kutafsiriwaje kuhusu masuala ya usalama wa taifa?
 
Sikubaliani na wewe..
Madini na nishati ni rasilimali za TAIFA!
Na kama nchi ikivamiwa leo...Watakaovamia watayachukua hayo madini na pamoja na kulipua vyanzo vya umeme ili kutupa giza watuvamie vizuri...Sasa unasema si usalama wa Taifa huo?

Angalau sasa hivi hauongelei mambo ya Mwinyi kuruhusu watanzania kula vyura na kitimoto, baba una mambo wewe yaani sikuwezi kabisa.

Na hao wanaotaka kuvamia nchi na kuzima umeme ili kuleta giza ni kina nani?
 
Huu ndio mchango wa maandishi lakini pia nimeyaongea mengi ya humu. Nikipata ule mchango wa sauti nitawaletea baada ya watu wa hansard kukamilisha kazi yao.
Mheshimiwa Spika, Katika kikao hiki na vilivyotangulia tumekuwa tukirudia kukumbushana juu ya wajibu wa Bunge lako hili tukufu, wajibu ambao kikatiba unatajwa kuwa ni pamoja na kuishauri na kuisimamia serikali. Lakini zaidi pia ambacho hatujakumbushana kwa uzito wake ni kuwa sisi ndio watunga sheria wa nchi hii; ndio wenye wajibu wa pekee wa kusema chombo gani kifanye kazi vipi, nini kiwepo, nini kisiwepo n.k Tuna nguvu ya Kikatiba ya kutunga sheria ambazo nyingi kati ya hizo zinaathiri maishi ya kila Mtanzania. Nguvu hii hii wanayo ndugu zetu wa Baraza la Wawakilishi kwa mambo yale yasiyo ya Muungano au ambayo yanahitaji ridhaa yao.


Ni kwa sababu hii Mhe. Spika naweza kusema kuwa changamoto kubwa inayotukabili kama watunga sheria, washauri na wasimamizi wa serikali yetu ni nafasi ya Taasisi na sera yetu ya Usalama wa Taifa katika kujenga na kuhakikisha uwepo wa Taifa lililo huru, lenye watu walio sawa na ambalo lina nafasi ya kufanikiwa katika jumuiya ya Mataifa ya ulimwengu. Katika kufanya hayo, Taasisi ya Usalama wa Taifa inasimama katika uwanja wa peke yake.


Ninafahamu Mhe. Spika kwamba hatujawahi kuwa na mjadala wa kina na mzito kuhusu sera na sheria zetu za usalama wa Taifa. Jambo hili limekuwa kama mwiko. Mara nyingi tumefanyia mabadiliko vipengele mbalimbali vya sheria zetu za usalama wa Taifa hasa ile ya 1970 na ile iliyounda TISS ya 1996. Karibu mara zote tumefanya hivyo pasipo mjadala mkubwa wa kuangalia athari na matokeo ya mabadiliko ya sheria hizo katika usalama wa nchi yetu. Umekuwa ni mwiko mkubwa wa kutokugusa katika sakafu hii suala la Usalama wa Taifa. Yawezekana hiyo ni kwa sababu ya unyeti wake, na hasa kutokana na sifa ya taasisi hiyo ambayo kwa baadhi ya watu yawezekana kuwa si sifa nzuri. Mhe. Spika, kwa heshima kubwa kwa Taifa letu, kwa Bunge lako tukufu, na kwa vyombo vyetu vya Usalama na hasa Usalama wa Taifa, naomba leo hii nivunje mwiko huo.


Matukio ya hivi karibuni, yametuthibitishia kuwa Taasisi yetu ya Usalama wa Taifa imelega lega, ni dhaifu, na kama tukiendelea nayo jinsi ilivyo, tutafika mahali ambapo kamwe hatukutaka kufika, tutakuwa hatuna tena Usalama wa Taifa. Tukiendelea jinsi ilivyo, pasipo kufanya mabadiliko ya haraka na ya lazima, tutakuja kujuta kwani tumeshaziona dalili za nini kinatungojea mbeleni.


Mheshimiwa Spika usalama wa Taifa umelegalega ndio maana tuko hapa tulipo leo. Leo tunazungumzia mambo ya mikataba mibovu, tunazungumzia wizi kama wa kutoboa gunia la sukari kwa panga, katika taasisi zetu hasa Benki Kuu, tunazungumzia uundwaji wa makampuni feki mengine yakiwa na viwanja si umbali mrefu kutoka maslahi ya Taasisi hii. Leo hii tunazungumzia jinsi gani watu wachache wameweza kutengeneza mtandao wa uhalifu wa fedha na ukashamiri, mtandao ambao kama Usalama wetu wa Taifa wangekuwa wanajua uwepo wake tusingefika hapa tulipofika. Mlolongo wa matukio ya kitapeli, msururu wa matukio ya kilaghai ambayo yamesababisha upotevu wa mabilioni ya shilingi zetu, ni ushahidi dhahiri kuwa Usalama wetu kama Taifa, uko matatani.


Leo hii Mheshimiwa spika, tunalazimishwa kupiga magoti na kuchuchumaa mbele ya wezi. Tunaambiwa kwamba waliohusika na upotevu wa fedha za EPA pale Benki Kuu ni kama watu waliotuteka nyara na wameshikilia bomu mkononi. Ati tukiwasukuma sana kuwadai wanaweza kulilipua. Hivyo leo hii kuna baadhi yetu wanalazimika kuzungumza nao kwa “upole” ili tusiwaudhi hao mafisadi. Tunalazimika kufanya vikao na watu waliochota fedha zetu, na tunalazimika kuficha hata majina yao. Mheshimiwa Spika, Usalama wa Taifa letu uko matatani.


Mheshimiwa Spika leo hii tunalipia mamilioni ya shilingi kila siku kwa kampuni ambayo imeichukua mkataba wa kampuni ambayo haikuweza kuingia mkataba wa awali kwani kampuni hiyo ya awal haikuwepo kisheria. Tunawalipa Dowans mamilioni ya shilingi, fedha ambazo zingeweza kutumika kumalizia miradi kadhaa ya mabwawa ya kuzalishia umeme. Tunawalipa kwa sababu Taifa letu liliacha kuingia mkataba na kampuni ambayo haikuwa na uwezo, haikuwa na historia, na haikuwa na vifaa vya kutufulia umeme wa dharura. Kampuni ambayo kama Usalama wetu wa Taifa wangekuwa makini isingepewa hata nafasi kuangika pendekezo lao la biashara.


Kwa kuangalia unyeti wa sekta ya nishati, ni jinsi gani ina athari katika shughuli za uchumi, kitendo cha Taifa kuruhusu mkataba ule kuingiwa pasipo uchunguzi wakina na taarifa ya clearance kutoka Usalama wa Taifa ni upungufu mkubwa kabisa wa sheria yetu ya Usalama wa Taifa. Na kwa vile bado tunaendelea kufanya kazi katika sheria hiyo hiyo ni wazi kuwa tusijekuombea tunapatwa tatizo jingine kubwa la nishati, kwani taratibu na sheria bado hazijabadilika na makosa kama ya Richmond yanaweza kurudiwa tena. Mheshimiwa Spika, Usalama wa Taifa letu uko matatani.


Mheshimiwa Spika kuna wawekezaji wanakuja kutoka kila kona duniani. Kuna wale ambao tumewapa eneo kubwa la ardhi yetu kiasi kwamba wanafikiri wana ubia na nchi yetu. Kuna wale ambao kutokana na sababu wanazozijua wao wenyewe wanafikiri wanaweza kuwanyanyasa Watanzania katika Taifa lao wenyewe kwa sababu tu “wamewekeza fedha nyingi”. Wengine wamefikia kuwa na kiburi wakiamini kuwa wamewaweka baadhi ya viongozi mifukoni mwao. Tukiacha hali hii iendelee siyo tu tunawapa kibali cha ufisadi bali pia tunahatarisha usalama wa Taifa letu.


Mheshimiwa spika, tumefikia mahali kwamba mambo muhimu ya Taifa yanafichwa kwa kisingizio cha Usalama wa Taifa. Tumeshuhudia wote siku ya Ijumaa wakati Mheshimiwa Waziri Mkuu alipozungumzia suala la Meremeta na makampuni mengine yanayodaiwa kuhusika na ufisadi Benki Kuu. Tumetakiwa kukubali kuwa uchimbaji wa madini wa Meremeta ulifanywa kwa ajili ya Usalama wa Taifa letu. Kwamba makampuni ya Deep Green, Mwananchi Gold, Tangold na Meremeta yote yaligawiwa mabilioni ya Shilingi bila kukaguliwa na mtu yeyote kwa ajili ya Usalama wa Taifa. Kwamba tumetakiwa kukubali kuwa Meremeta haijakaguliwa na Mkaguzi Mkuu kwa vile kuchimba kwake madini, kuyauza na kupata fedha vyote ni kwa ajili ya Usalama wa Taifa.


Mheshimiwa Spika huo Usalama wa Deep Green, huo Usalama wa Mwananchi Gold, huo usalama wa Tangold, huo usalama wa Meremeta, ni usalama wa Taifa gani?! Ni usalama na ulinzi wa watu wa nchi gani!? Mbona sisi wawakilishi wa wananchi wa Taifa hili ambalo Meremeta na wenzake wanatulinda, hatuna taarifa ya walinzi hao? Kama ni Usalama wa Taifa letu hawa wakurugenzi wa Afrika ya Kusini wanafanya nini humo? Je kwa kuhusisha wageni siyo kwamba tunacompromise national security?


Mheshimiwa Spika, tukikubali hilo itakuwa ni sawa na kumruhusu mtu aje shambani kwako, alime, apande, vikue na avune, kisha aende kuuza na faida kuiweka mkononi, na ukimuuliza akuambie amekuja kukutunzia shamba. Ukimwambia uone mapato aliyoyapata anasema “ni siri yake kwa ajili ya usalama wako”! Ukimwambia nani alimtuma anasema “ni siri yake kwa ajili ya usalama wako”. Usalama huu wa Taifa wa Meremeta ni usalama wa nani?


Sasa Mheshimiwa Spika, kama ni usalama wa CCM, kama ni usalama wa baadhi ya watu katika serikali, kama ni Usalama wa watu fulani kwenye jeshi letu basi tuambiwe kwanini ni usalama wao!? Lakini kama kweli ni Usalama wa Taifa hili na kama kweli Jeshi letu ambalo linaitwa “la wananchi” linahusika kwa namna yoyote na mambo ya Meremeta, Tangold, Deep Green na Mwananchi Gold basi sisi wawakilishi halali wa wananchi hao tunataka kujua na tujue sasa.


Mheshimiwa Spika, wakati umefika wa kusema “enough is enough”. Sasa imetosha, tunaitaka nchi yetu irudishwe. Tunataka sheria zetu zifuatwe na wavunjaji sheria hizo kuadhibiwa pasipo upendeleo, woga, hofu, au aina yoyote ile ya utwana. Tunataka Usalama wa Taifa ambao kweli utahakikisha usalama wa fedha yetu, usalama wa mali na raslimali zetu, na kwa hakika usalama wa kila kitu kiitwacho cha Mtanzania. Hatuwezi tena kuendelea kuitikia kibwagizo cha mafisadi na kuimba wimbo wa lele mama mbele yao. Umefika wakati Bunge lako tukufu Mheshimiwa Spika lichukue msimamo, Msimamo ambao utaimarisha, utaisafisha, na kwa hakika kabisa utaipa uhai mpya idara yetu ya Usalama wa Taifa, ili iwe ya kisasa zaidi, wazi zaidi, na inayowajibika zaidi kwa Taifa lake. Hilo lazima tufanye.


Mhe. Spika, Tunahitaji mabadiliko katika sehemu kubwa mbili. Tunahitaji mabadiliko ya kisheria na tunahitaji mabadiliko ya kifikra linapokuja suala la idara ya Usalama wa Taifa. Hilo la pili ni gumu zaidi, lakini hilo la kwanza ni rahisi na liko ndani ya uwezo wetu. Nimesema hapo nyuma kuwa tunajukumu la kuishauri na kuisimamia serikali, lakini jukumu letu la kwanza kabisa kama wabunge ni kutunga sheria. Hivyo hili la kufanyia mabadiliko upande wa sheria kuhusu Usalama wa Taifa limo ndani ya uwezo wetu.


Kwenye upande wa sheria, hatuna kuandika upya sheria yetu ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1970. Sheria ile ilitungwa wakati dunia imegawanyika katika pande mbili, nchi za kisoshalist na zile za Kibepari, iliandikwa wakati wa Vita Baridi ambako sera yetu ya nje ilikuwa ni ya kutofungamana na upande wowote. Iliandikiwa miaka tisa tu tangu Tanganyika iwe huru na miaka sita tu tangu tuungane. Ni kweli kuna mabadiliko ya hapa na pale tuliyoyafanya, lakini naamini ipo haja ya kukaa chini na kuangalia hali ya ulimwengu leo hii, hali ya kiuchumi na kisiasa barani mwetu na duniani na hivyo kuangika sheria mpya itakayoakisi hali halisi duniani sasa hivi. Sheria hiyo mpya lazima izingatie uelewa wetu wa haki za raia na binadamu na dhana nzima ya utawala bora.


Lakini mabadiliko makubwa Mhe. Spika yanahitajika katika Taasisi yetu ya Usalama wa Taifa. Nimekuwa nikijiuliza kwa muda sasa ni jinsi gani Bunge hili liliweza kupitisha sheria iliyounda TISS ya mwaka 1996. Kwa yeyote anayeweza kuisoma sheria hiyo anaweza kushtushwa na jinsi taasisi hiyo ilipoundwa na wakati huo huo kufungwa mikono kufanya kazi yake ya Usalama wa Taifa. Inawezekana vipi tuwe na Taasisi ya Usalama wa Taifa ambayo haina nguvu ya kumkamata mtu?


Ibara ya tano ya sheria hiyo inafanya kazi ya TISS kuwa butu. Kwamba TISS wana jukumu la kukusanya habari za kijasusi lakini chochote wanachokipata inabidi wapeleke kwa mtu mwingine akifanyie kazi. Kipengele cha pili cha ibara hiyo hiyo kinaikataza TISS na ninaomba ni nukuu “(2) It shall not be a function of the Service-

to enforce measures for security;” Yaani, TISS inakatazwa kuchukua hatua za kiusalama kama vile kumweka mtu kizuizini, kukamata vitu n.k! Halafu leo tunashangaa fedha zimekombwa Benki Kuu!


Lakini zaidi pia tunahitaji kuondoa mawazo kuwa Usalama wa Taifa lengo lake ni kufuatilia watu hasa wale wanaoonekana kuikosa serikali, kuipinga au kwa njia halali kukataa utendaji wake. Leo hii bado kuna hofu miongoni mwa watu wetu kuwa ukifanya jambo fulani basi Usalama wa Taifa wanakufuatilia wanataka kujua wewe ni nani.


Usalama wa Taifa lazima iwe ni taasisi ya wananchi wa Taifa hili. Utaratibu wake wa ajira uwekwe wazi ili watu wajue na kama kuna mtu anataka ajira basi ijulikane. Mheshimiwa Spika leo kijana wa nchi kama Marekani au wa Uingereza anayetaka kutumikia Taifa lake katika maeneo ya Usalama wa Taifa haitaji kwenda mbali vigezo vyote na fomu zinapatikana kiurahisi tu kwenye mtandao. Sijui ni wangapi kati yetu humu wanajua mtumishi wa Usalama wa Taifa wa Tanzania. Sijui ni wangapi wanajua kuwa kutokana na Sheria hii ya 1996 Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa anaajiriwa kwa makubaliano tu kati yake na Rais (Ibara 6:2). Ni wangapi hapa wanajua kuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa anaweza kumuajiri mtu yeyote kwa shughuli za Usalama kama anavyoona inafaa (ibara 7:2 a, b).


Hivi kwa mtindo huu wa ajira ambapo Bunge halina uamuzi wa mtu muhimu kama Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa kweli tunashangazwa na yote yanayotokea? Ni jukumu letu kusahihisha makosa yetu wenyewe, ili hatimaye tuwe na Usalama wa Taifa ambacho kitakuwa kweli ni chombo kilichowazi, chenye taratibu zinazoeleweka, na ambacho kiko mikononi mwa wananchi wenyewe na hivyo kuepukana na haya maneno ya kutumia jina la Usalama wa Taifa.


Nimalizie kwa kusema hivi. Wakati matukio ya Septemba 11 yametokea kule Marekani serikali ya nchi hiyo haikuacha mambo hayo yapite tu hivi hivi. Rais Bush kwa kufuata maagizo ya Bunge lao aliunda Kamati ya Kuangalia matukio ya Septemba 11 na kutoa mapendekezo yake. Kati ya vitu walivyoangalia ni suala zima la jinsi gani jumuiya yao ya Intelligencia licha ya kuwa na vifaa vingi vya kisasa na mtandao mkubwa duniani walishindwa kutabiri kwa uhakika na hatimaye kuzuia matukio yale. Tume ile ilipomaliza kazi yake ilipendekeza mabadiliko makubwa katika Usalama wa Taifa la Marekani kwa kuunda Kurugenzi mpya ya Usalama wa Taifa na kulazimisha idara ambazo zilikuwa hazitakiwa kuwasiliana kisheria zianze kushikiriana na kupashana habari. Kosa la kushindwa katika mambo ya kijasusi wenzeti wa Marekani hawakuliacha lipite tu kama mapenzi ya Mungu.


Sisi leo hii tuna matukio mengi ambayo yamedhihirisha kuwa Jumuiya yetu ya mambo ya Intelligensia haijaenda na wakati na bado hakuna legal framework ambayo inalazimisha taasisi zetu za Usalama kuwasiliana na kupashana habari. Ni matumaini yangu kuwa serikali itakaa chini na kuja na kufanya utafiti na upembuzi yakinifu wa jinsi gani tunaweza kuiboresha idara yetu ya Usalama wa Taifa ili kweli tujiandae na ushindani katika nyanja zote za maendeleo na tusiachwe nyuma tena. Tunao watanzania wengi ambao wako nje ya nchi na ambao wako kwenye taasisi mbalimbali ni wakati wa kuanza kuwatumia hawa na nina uhakika kama tungekuwa makini suala la Richmond lingekwepeka mapema sana kwani baadhi ya ndugu zetu walioko Marekani walishatuambia tangu siku ya kwanza kwamba kampuni hiyo ni feki.

Safi sana zito. Nashauri kila njia ifanyike tukurudishe 2010. Mbona umesema yote kweli? Wajifanye hawasikii lakini masikioni mwao limegusa na ukweli wameujua.
 
Angalau sasa hivi hauongelei mambo ya Mwinyi kuruhusu watanzania kula vyura na kitimoto, baba una mambo wewe yaani sikuwezi kabisa.

Na hao wanaotaka kuvamia nchi na kuzima umeme ili kuleta giza ni kina nani?[/quote]

Waulize hao waliodai kuwa mikataba ya KIWIRA,RICHMOND NA MEREMETA NI YA USALAMA WA TAIFA!
NB:USALAMA GANI WA TAIFA HUO AMBAO AUHUSIANI NA KULINDA TUSIVAMIWE?
AMA KULINDA MASLAHI YA MNYONGE?
Kuona kuwa ana pata mahitaji yake muhimu na hata chakula kwa kuutumia UTAJIRI ALIOPEWA BURE NA MUNGU?
NI MPAKA LINI TUTAKAA NA KUANGALIA WATOTO WETU WAKIFA KWA NJAA NA KUISHI KAMA WAKIMBIZI?
 
Usiidharau RESOLVE YANGU KWA MANENO YAKO YA KIPUUZI!
NCHI IMEUZWA!
Maswali ni mengi!
Na kama wewe uko comfortable..Well i dont know how!
Unless unajua kitakachofanyika!
TAIFA LIMEOZA!
Mhhhhhhhhhh jm hivi wewe ndiye mwenye uchungu kuliko wana jf wote kweli kiasi kwamba wengine si tunaonekana wapuuzi?.
Sorry mie sina ubavu wa kubishana na wewe kama mwanamke mwafirika.
Naheshimu kauli zako mkuu na kuzikubali hata kama zina kaarufu ka matusi:(
 
Safi sana zito. Nashauri kila njia ifanyike tukurudishe 2010. Mbona umesema yote kweli? Wajifanye hawasikii lakini masikioni mwao limegusa na ukweli wameujua.

Mkuu samahani sana kwani ndiyo maana hata OLE alisema kitu!
Ila HII HOTUBA YA ZITTO HAPO JUU NDIYO IMENIPAGAWISHA!
HUYU JAMAA ATAKUWA SHUJAA KWA AWAMU NYINGINE!
MARK MA WORDS!
Kama kweli akisimamia hapo!
Basi ukombozi ni lazima!
 
Good job Bw.Zitto lakini experience inaonyesha speech hizi zinaishia hewani tuu na hakuna chochote kitakacho badilika,sasa kuna bill yeyote mezani umetayarisha unayotaka kuweka bungeni ili kubadilisha hayo mambo uliyozungumzia? action plseee!

Hapo ndipo anapopatikana mtu ,maana kuna kila aina ya upingaji hapo Bungeni ,lakini woote utawasikia wakitema eti cheche lakini hatuoni action yeyote ,hakuna cha kuweka shilingi wala kuweka bili ni makelele na wananchi kupewa tamaa kuwa sasa bungeni kuna waka moto ,lakini kikao kikimaliza palipounguwa hapaonekaniki .hapo ndipo wengi wetu tunapoachwa kwenye mshangao.
Sasa kuna wengine wamezuka hawa wamikuja na neno ...tusubiri...!
 
Sijui ni wangapi wanajua kuwa kutokana na Sheria hii ya 1996 Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa anaajiriwa kwa makubaliano tu kati yake na Rais (Ibara 6:2). Ni wangapi hapa wanajua kuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa anaweza kumuajiri mtu yeyote kwa shughuli za Usalama kama anavyoona inafaa (ibara 7:2 a, b).

Halafu wakuu...Rejea hiyo quote hapo juu...

Naomba kama kuna anayejuwa anijibu hili.
Rais huchagua mkurugenzi wa Idara ya Usalama ambaye ndiye mwajiri wa wanausalama.
Je...Mkurugenzi wa usalama wa MKAPA NA KIKWETE NI MMOJA AMA TOFAUTI?
NA KAMA NI TOFAUTI...BASI LAZIMA MMOJAWAPO NDIO WA KUSIKILIZWA
 
Waulize hao waliodai kuwa mikataba ya KIWIRA,RICHMOND NA MEREMETA NI YA USALAMA WA TAIFA!
NB:USALAMA GANI WA TAIFA HUO AMBAO AUHUSIANI NA KULINDA TUSIVAMIWE?

Mambo ya kuvamiwa yanahusiana vipi na mikataba? Au ndio yale yale ya kuandika chochote ili uonekane umechangia. Nani anavamia nchi ya Tanzania?

Hata hivyo sikushangai sana maana muda mfupi uliopita ulianza kumlaumu Raisi mstaafu kuwa aliruhusu watu kula vyura na kitimoto kwenye hii thread wakati ukijua kabisa hayo yote hayana uhusiano wowote na hii thread.
 
Mara nyingi tuna confuse that which is with that which it ought to be.

Hiyo confusion hiyo, unayoisema ndio Mushi anaifanya hapa:

Sikubaliani na wewe..
Madini na nishati ni rasilimali za TAIFA!
Na kama nchi ikivamiwa leo...Watakaovamia watayachukua hayo madini na pamoja na kulipua vyanzo vya umeme ili kutupa giza watuvamie vizuri...Sasa unasema si usalama wa Taifa huo?

Ulichokisema hapo, Mushi, ni kile wewe unadhani kina make sense kiwe ni sheria. Lakini sio existing law.

Kwa hiyo, reformers lazima kwanza mkubali kwamba under existing law, Rashid Othman sio mzuia wezi. Wa mikufu ya dhahabu au migodi ya dhahabu.

Halafu ndio uanze ku argue kwamba hiyo hai make sense. Lakini mnachokisema sasa hivi, Mushi, pamoja na Zitto (Mh.) na reformers wengine, ni kwamba Usalama umeshindwa kufanya kazi yao. Sasa hilo, kama ni kweli, halihitaji mabadiko ya sheria. Kwa maneno mengine mnasema utendaji ndio mbaya. Ndio maana nikasema watetea ufisadi Bungeni wangeweza kuwazimilia mbali na hizo hoja ambazo hazija pikwa vizuri. Bahati nzuri kwa reformers, CCM ya kina Pinda na Waziri Marmo nao sio wazuri sana katika ku cover mafisadi, as hard as they appear to try.

Unaona how that reform effort is being stymied by being vague in the conception and presentation of existing law?
 
Hiyo confusion hiyo, unayoisema ndio Mushi anaifanya hapa:



Ulichokisema hapo, Mushi, ni kile wewe unadhani kina make sense kiwe ni sheria. Lakini sio existing law.

Kwa hiyo, reformers lazima kwanza mkubaki kwamba under existing law, Rashid Othman sio mzuia wezi. Wa mikufu ya dhahabu au migodi ya dhahabu.

Halafu ndio uanze ku argue kwamba hiyo hai make sense. Lakini mnachokisema sasa hivi, Mushi, pamoja na Zitto (Mh.) na reformers wengine, ni kwamba Usalama umeshindwa kufanya kazi yao. Sasa hilo, kama ni kweli, halihitaji mabadiko ya sheria. Kwa maneno mengine mnasema utendaji ndio mbaya. Ndio maana nikasema watetea ufisadi Bungeni wangeweza kuwazimilia mbali na hizo hoja ambazo hazija pikwa vizuri. Bahati nzuri kwa reformers, CCM ya kina Pinda na Waziri Marmo nao sio wazuri sana katika ku cover mafisadi, as hard as they appear to try.

Unaona how that reform effort is being stymied by being vague in the conception and presentation of existing law?

HIVI UKIIWEKA MIGODI MIKONONI MWA WATU BINAFSI BILA KUHAKIKISHA MKATABA NI WA MANUFAA kwa MWANANCHI MNYONGE
JE HUJAUZA UHURU?

Kama mtu anamiliki mgodi kuna tofauti gani na mtu anayeitwa RHODESIA alivyokuwa akiimiliki ZIMBABWE kwa msaada wa MALIKIA na hata kukufuru na kuliita TAIFA kwa jina lake?

KAMA MIGODI YETU NI MOJAWAPO YA RASILIMALI ZETU ZA KUTULISHA NA KUTULETEA MAENDELEO...THEN SI USALAMA WA MWANANCHI NA KIZAZI KIJACHO?

Wamarekani wenyewe walipovamia IRAQ walilinda visima vya mafuta.

Ni lazima hiyo mikataba ipitiwe na usalama wa TAIFA ili kutathmini kama bado inaruhusu UHURU WETU KUWA VALID!

Kwamba uamuzi wa mwisho kuhusu mikataba hiyo uzingatie sheria mpya zitakazo preserve UHURU WETU! Na kunufaika na MALI ZETU.

Sasa hiyo mikataba yenu ni sawa na kumwuzia MKABURU UHURU halafu unasema tuko huru?
 
Hiyo confusion hiyo, unayoisema ndio Mushi anaifanya hapa:



Ulichokisema hapo, Mushi, ni kile wewe unadhani kina make sense kiwe ni sheria. Lakini sio existing law.

Kwa hiyo, reformers lazima kwanza mkubaki kwamba under existing law, Rashid Othman sio mzuia wezi. Wa mikufu ya dhahabu au migodi ya dhahabu.

Halafu ndio uanze ku argue kwamba hiyo hai make sense. Lakini mnachokisema sasa hivi, Mushi, pamoja na Zitto (Mh.) na reformers wengine, ni kwamba Usalama umeshindwa kufanya kazi yao. Sasa hilo, kama ni kweli, halihitaji mabadiko ya sheria. Kwa maneno mengine mnasema utendaji ndio mbaya. Ndio maana nikasema watetea ufisadi Bungeni wangeweza kuwazimilia mbali na hizo hoja ambazo hazija pikwa vizuri. Bahati nzuri kwa reformers, CCM ya kina Pinda na Waziri Marmo nao sio wazuri sana katika ku cover mafisadi, as hard as they appear to try.

Unaona how that reform effort is being stymied by being vague in the conception and presentation of existing law?

kuhani.. umeshindwa kuona jambo moja dhahiri katika hoja ya zitto, TISS wameshindwa kufanya kazi zao si kwa sababu ya utendaji bali kutokana na sheria iliyopo. Sheria iliyopo na sera ya usalama wa Taifa (ambayo sijui nani anayo) inafanya vigumu sana kwa usalama wa Taifa kufanya kazi ambayo tunaamini inapaswa kuwepo katika ajenda yao.

Ukiangalia sheria ya Usalama wa Taifa utaona majukumu ya Idara hiyo, majukumu ambayo kimsingi hayasimamii usalama wa Taifa bali kukusanya habari tu.

Hivyo suala la kubadili sheria ni msingi mkubwa wa kuleta mabadiliko katika utendaji.
 
Hivyo suala la kubadili sheria ni msingi mkubwa wa kuleta mabadiliko katika utendaji.

Mkulu Heshima mbele,

Haya ndio maneno tunatakiwa wananchi wote wa Tanzania na wabunge kuwa tunayaimba kila siku, kwa sababu hawa wezi wetu wa bongo siku zote wanazitumia sheria zetu mbovu kutuibia kwenye taifa, the name of the game ni mabadiliko ya katiba kwanza!

Hapa tupo ukurasa mmoja!
 
Jiwe na Hollo, madhabahuni ni mahali patakatifu, mafisadi wa CCM hawasitahili kukanyaga hapo. Wao wanasatahili kupelekwa msalabani kusulubishwa kwa sababu ya ufisadi wao.
 
... katika hoja ya zitto, TISS wameshindwa kufanya kazi zao si kwa sababu ya utendaji bali kutokana na sheria iliyopo. Sheria iliyopo na sera ya usalama wa Taifa (ambayo sijui nani anayo) inafanya vigumu sana kwa usalama wa Taifa kufanya kazi ambayo tunaamini inapaswa kuwepo katika ajenda yao.

Ukiangalia sheria ya Usalama wa Taifa utaona majukumu ya Idara hiyo, majukumu ambayo kimsingi hayasimamii usalama wa Taifa bali kukusanya habari tu.

Hivyo suala la kubadili sheria ni msingi mkubwa wa kuleta mabadiliko katika utendaji.

Tena na tena, mnajichanganya.

"Tunaamini Inapaswa," inapaswa kwa mujibu wa nini, sheria au busara?

"Kukusanya habari," habari zipi, za wezi? Na majambazi wa kuvunja benki pia? Na wapokonya pochi?

"Kuleta mabadiliko katika utendaji," kwani umeshawapa majukumu ya huo utendaji?

Hicho kitu "tunaamini inapaswa iwe ajenda yao" ni kuotea otea kuliko vague. Kama inapaswa kwa kujibu wa mawazo yenu, ina maana mnapendekeza iwe kazi yao. Kama "inapaswa" kwa mujibu wa sheria, tuonyeshe!

Sio kazi yao. Sheria haijipingi na haijawahi kuwapa Usalama kazi ya kuzui au kukusanya habari za wezi wa migodo au wa pochi. Hakuna hicho kitu. Wewe ndio "unaamini" inapaswa iwe kazi yao.

Sema kwanza, "hewala, sio kazi yao." Halafu hatua ya pili ndio sema "sasa tunataka iwe kazi yao."
 
Back
Top Bottom