Meremeta, Randgold,Tangold & The Jersey Connection: Jeshi liliingizwaje hapa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Meremeta, Randgold,Tangold & The Jersey Connection: Jeshi liliingizwaje hapa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bill, Jun 25, 2009.

 1. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,167
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Kwa Uchache: Ya Meremeta, Tangold, JWTZ na Signatories

  Waziri akizima hoja ya Slaa kuhusu Ukaguzi wa Meremeta/Tangold alisema haiwezi kujadiliwa hadharani kwa kuwa inahusu mambo nyeti ya usalama wa Taifa na Jeshi la Wananchi Tanzania - JWTZ.

  Ilishadhihirika kuwa Meremeta ilirithisha shughuli zake kwa Tangold, na kwamba Serikali kupitia BOT iliilipia deni kubwa kupitia benki ya SA zaidi ya TZS 155 bn. Tangold ikachukua kazi za Meremeta.

  Kwa maana hiyo Tangold ni mali ya usalama wa Taifa kupitia JWTZ. Na kwa maana hiyo pia CHENGE mtia saini mkuu wa akaunti za Tangold ndiye Signatories wa JWTZ.

  Ni akaunti ngapi za JWTZ ambazo Chenge na wenzake ni lazima waanguke sahihi zao ndio hela zitoke.

  Kwa nini jeshi la nchi yetu linadhalilishwa katika wizi huu limekaa kimya, linatakiwa kuja na kutoa ufafanuzi ikibidi kuichukulia hatua za kinidhamu Serikali.

  Leteni michango yenu kwa ufupi
   
 2. M

  Masatu JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  How do u define "singatories?"
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  He/she meant Signatories ....!
   
 4. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,167
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  that was the meaning,
   
 5. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kama hatua ipi kwa mfano?
   
 6. A

  African Member

  #6
  Jun 25, 2009
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu mjadala unazimwa kwa lipi haswa ? Je ni kwa maslahi ya watawala au maslahi ya taifa? Je usalama wa taifa upo kwa ajili ya nani kama si raia ????
   
 7. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,920
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kuna jamaa hapo juu wanaanza kudiscuss the spelings! Nadhani nao wana nia ya kuuzima huu mjadala hapa JF. So wapo wengi pia hapa JF wenye nia hiyo.

  Otherwise Bill umetoa mchanganuo mzuri sana. Ni kitu ambacho tunahitaji majibu na si majibu OVYO OVYO.
   
 8. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2009
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mzee Bill, nadhani ulimaanisha "Signatories".

  Wenye jukumu la kutia saini ktk cheki za kampuni ya Tangold, ili bank inayoweka fedha zake iweze kumlipa mteja yeyote, waliteuliwa, kama ilivyo kawaida, na bodi ya kampuni. Andrew Chenge, akiwa Attorney General wa Tanzania wakati wa kampuni kuundwa alikuwa Member wa Bodi. Kwa usahihi kabisa akateuliwa ni mmoja wa signatories.

  ULAJI ulipoamza kwa nguvu miongoni mwa watumishi wa umma, (baada ya Muasisi wa Taifa kuondoka) inaonekana Chenge aliruhusiwa "kununua" hisa ktk hii kampuni, kwa bei tusiyofahamu.

  Sina hakika kama ni wakati huo alipofungua akaunti ktk Bank ya kule Jersey Islands, Uingereza, na kuanza kulundika "vijisenti" huko. Waingereza wametuarifu kwamba ktk mgao wa ile commission ya 30 percent ya ununuzi wa Radar, US$ 600,000 zilizolipwa bwana Vijisenti, ziliwekwa huko.

  Waingereza wanajua. Sisi Tanzania tumearifiwa. Pia tunajua kwamba ile bei ya radar ilikuwa ya kuruka sana, kiasi cha Waziri mmoja wa Uingereza (?Judith Short) kutusemea ktk Bunge lao kwamba kampuni yao ilitudanganya. Sisi wenyewe tunatambua commission ya 30 percent ni kufuru na wizi wa hadharani. Lakini "Uchunguzi" wetu bado haujakamilika, licha ya madokezo na madondoo yote hayo.

  Viongozi wazalendo jasiri, wakiongozwa na Dk. Willibrod Slaa Bungeni, wakauliza "kulikoni?". Mheshimiwa Jeremiah Sumari, Naibu Waziri wetu wa Fedha tunayemlipa mshahara, akasema maswali hayo yanahusu viongozi wa JWTZ na kwamba hayazungumzwi! Hapa akiimanisha kwamba ukiteuliwa kiongozi ktk Jeshi, basi hata aliyekuteuwa, yaani Serikali inayosimamiwa na Bunge, haiwezi kukuhoji unapokwiba fedha za umma.

  Swali lilikuwa Controller and Auditor General aanze kazi mapema kukagua makampuni haya yenye hisa nyingi za Serikali ili Bunge lijue ni nini kilifanyika. Ni jukumu lao.

  Mhe. Sumari sio tu alijibu utumbo, bali alimalizia kumwambia Mhe. Slaa abuni hoja nyingine kuleta Bungeni!

  Siku iliyofuata, Mhe. Zitto Kabwe akielezea masikitiko yake kuhusu majibu ya Mhe. Sumari, ambayo kwa kila muelewa aliyeyasikia aliona ni ya "hovyo hovyo" akaamuriwa na kiongozi wa Bunge eti ayafute maneno hayo. Sasa tujiulize "Je Tutafika?"

  Mimi naona Bunge hili la sasa likiwa na majority ya wana-CCM, limefikia kikomo ktk kupuuza maslahi halisi ya WaTz. Na Serikali yenyewe inaonekana kuwa ni jumuiya ya watu wasioelewa au wasiojali maovu yanayofanyiwa nchi yao, yanayosababisha kutokufikia malengo ya kujikwamua ktk ujinga, umaskini na maradhi yanayotuangamiza.
   
 9. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hili wazo la kwanini JWTZ haitoi tamko hata mimi limenijia wakati kazaa kichwani, serikali inalipaka matope jeshi hapa, na sisi wananchi tutalichukia jeshi kwa namna hii...mana kumbe hata lenyewe linajihusisha na ufisadi...kama sio kweli, JWTZ mko wapi mkipakwa matope...??
   
 10. R

  RACH Member

  #10
  Jun 25, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JWTZ wote ni makada wa CCM! kwa hiyo ni wale wale
   
 11. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Bill,
  Hao askari wanaoifahamu hiyo Meremeta ni asilimia ndogo sana ya jeshi letu. Hapo ndipo utakubali kuwa ile kauli ya Chiligati kule Busanda kuhusu uwezo wa wananchi kusoma magazeti na vyombo vya habari kwa ujumla haikutoka kwa bahati mbaya. Kwao hizi ni kelele za mlango!
   
 12. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #12
  Jun 26, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,167
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280

  Hakika kwa bunge la majority ya wana CCM hakuna uzingatiaji wa maslahi ya nchi. Hayo yanaongelewa hadharani tena LIVE kila mTZ anasikia, watu wanapuuzwa na kuambiwa wafute hoja, wabunge wamenyamaza tuu, Je inakuwaje kwenye vikao vya ndani vya wabunge wa CCM?

  Nadhani huwa wanashaauriana "Msiwastue hawa walala bongo ili tuendelee kuila nchi"

  Haiingii akili kuona kuwa nchi yenye utajiri wa rasilimali kila pemebe iko taabani kwa umaskini kiasi kwamba wananchi wake wanashindwa kumudu hata mlo mmoja.

  Hatujawahi kutawaliwa na chama kingine zaidi ya CCM, kwa maana hiyo basi umaskini huu umeletwa na CCM. Ili kuuondoa umaskini ni lazima kwanza kwenda kwenye source na kuiondoa. Na source yenyewe ni CCM

  Ondoa CCM ondoa Umaskini
  [​IMG]
   
 13. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #13
  Jun 26, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,675
  Likes Received: 21,907
  Trophy Points: 280
  Bill, Au Jeshi letu limepitiwa usingizi tulizindue?
   
 14. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #14
  Jun 26, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,586
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  JWTZ lenyewe linaendeshwa kisiasa, Hata siku moja usitegemee kwamba watasema chochote. Unadhani wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao ni wanajeshi wastaafu wanateuliwa kwa bahati mbaya???

  JWTZ na CCM ni mtu na Mjomba wake tusitegeme Tamko lolote.
   
 15. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #15
  Jun 26, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  watu waliosomea lugha utawajuatu..!
   
 16. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #16
  Jun 26, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,586
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Wadau tubaki kwenye mada, mambo ya lugha tuachane nayo. Tujadili hii thread...
   
 17. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #17
  Jun 26, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hii ya kusema miradi hii ina uhusiano na usalama wa Nchi naona ni kutishana ,ukiangalia miradi yote ya serikali inaweza kuhatarisha usalama wa Nchi au inahusika moja kwa moja na usalama wa Nchi.
  Au tuseme wanamaanisha bajeti ya vyombo vya ulinzi haimo katika na haijadiliwi katika Vikao vya Bajeti ya Nchi , kwa kuwa vyombo hivyo vina vitega uchumi vyao na mapato na matumizi yanayopatikana huko yanakuwa ni siri kwa walioko au waliomo humo. Hapa panakuja hoja ya mishahara na mafao ya wanaohusika na mapato ya huko ,viwango vya mishahara ya vyombo hivyo havihusiani na viwango vya mishahara ya wafanyakazi wa serikali ,kwa maana hiyo panapojadiliwa viwango vya mishahara pale bungeni vyombo vya ulinzi na usalama vinakuwa havimo ,na ndipo kunakopelekea wafanyakazi wa vyombo hivi kulipana kwa upendeleo na wachini kabisa anakuwa kama mtumwa na hana mtetezi na inaonekana pale wanapopelekwa mstari wa mbele na wengine kufariki na wengine kurudi vilema huwa inakuwa mbinde kulipwa na na mara nyingi huwa hawalipwi kabisa ,nakumbuka nilihangaishwa sana kudai malipo niliporejea kutoka kwenye mapambano ya kumng'oa nduli na sikulipwa ,wisho wake niliambiwa niende kwa Nyerere kwenda kudai kwa kuwa yeye ndie aliesema vijana wajitokeze kulinda Nchi yao sio kitengo cha Jeshi. Sikupata kitu.
  Labda kama mpo mnaofahamu bajeti ya matumizi ya vyombo vya ulinzi kama huwa inajadiliwa bungeni na kujaziwa fedha kutoka serikalini, mtueleze.
   
 18. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #18
  Jun 27, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Wana JF, Randgold inaishia wapi na Tangold inaanzia wapi ? Waendeshaji wa Tangold wana accounts zao Visiwa vya Jersey - zinakofichwa hela zetu walizotuibia. Sasa Serikali imepiga marufuku kuzungumzia Meremeta , Deep Green na Tangold. Hebu tujikumbushe kidogo yaliyotokea 2007:-

  Kweli njia ya mwongo ni fupi - Pinda amekubali kupindishwa na pamoja na kwamba ukipanda mchele huwezi kuvuna chungwa, haya kwa hakika yanasikitisha. Nawasilisha.
   
 19. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #19
  Jun 28, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Halafu kinachotatanisha zaidi - Randgold Resources baadaye walitoa taarifa hii:-

  Hivi JV ilikuwa kati ya Randgold Resources na Serikali ya Tanzania au ilikuwa kati yake na Tangold - kitendawili kinakua. Lakini Kulingana na Mizengo Pinda
  Kaaazi kweli kweli..........maanake na Meremeta hiyo hiyo ilikuwa JV kati ya Trinnex (Pty) Limited ya Afrika Kusini na serikali ya Tanzania !!!
   
 20. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #20
  Jun 28, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Mjadala wa DECI utazimwa kwa maslahi ya "watawala", na mjadala wa Tangold/Meremeta, nao pia utazimwa kwa namna hiyo hiyo.

  Mungu ibariki Tanzania!

  2010 tutajua moja, kama tutaendelea kukuubali ufisadi (kwa staili ile ya zimwi likujualo...) ama tutataka uongozi (si utawala) mbadala.

  Nani anastahili kuongoza? Mtapima wenyewe. Kama kweli demokrasia ipo nchi hii!

  ./Mwana wa Haki
   
Loading...