Khalidoun
JF-Expert Member
- Feb 12, 2013
- 2,833
- 4,458
5. 3D printing technology
Dunia ipo kasi mno, na hii kasi sijui kama itamuacha mtu salama. Si ajabu tukawa tunakata lile shina la mti tulilokalia, ni jambo la kuhuzunisha lakini hatuna jinsi ndio tumeshafika huko. Miaka ya nyuma kidogo kabla teknolojia haijakuwa ilimhitaji mtu aandike kila kitu kwa kutumia mkono na peni, leo hii unaweza kuchapisha hata vitabu 1000 ndani ya saa moja. Hii ni 1D printing, dunia sasa imefika kwenye 3D printing, ambapo mtoto akivunja kikombe mama anawasha printer anachapisha kikombe kingine anakoroga uji.
Tumeona 3D bioprinters zimefika uwezo wa kuprint viungo bandia, mifupa, ngozi, pua, maskio, mapafu na vitu vingine vingi sana. Viwanda vingi sana sasa wanatumia 3D printer, Google imetoa takwimu kuwa zaidi ya 11% ya viwanda wamehamia kwenye 3D printing. Hapa ndugu zangu wengi watakosa ajira miaka 20 ijayo ambapo karibia 95% ya viwanda watakua wanatumia 3D printers.
Dunia tumefika hatua ambayo tunaweza sasa kutengeneza vitu kama drones,viatu,urembo,vifaa vya muziki,vifaa vya magari na ndege, nguo.Yani utashangaa unaposhangaa kuona 3D printer inaprint 3D printer mwenzake, tayari zipo Printers zinazoprint printer.
Wakati kila mtu anawaza kuunda driverless car mzee baba Kevin Cringer kaamua kutuletea 3D printed car kupitia kampuni yake ya Divergent 3D. Makampuni makubwa kama KIA, BMW, Strati tayari nao wameanza kuprint magari, yani gari unalichapisha kama gazeti.
Mwaka jana tumeshangazwa baada ya nyumba ya kwanza kuwa printed na 3D printers, start up company moja huko San fransisco wameweza kujenga nyumba nyumba nzima kwa 3D printer ndani ya masaa 24.
Hivi majuzi China na Dubai wamejenga maghorofa marefu zaidi duniani yenye floor 5 ndani ya siku 17. AUE tayari wameanza mpango wa kuprint sky scraper ndefu zaidi kuwahi kuwa 3D printed. Ndugu zangu wahandisi watu wa michoro, quantitative survey, wabeba zege watakuwa na hali ngumu sana miaka 10-20 ijayo. Wazalishaji wa simenti, mbao, mabati na wafyatua matofali sijui watasurvive vipi.nyumba iliyojengwa kwa teknolojia ya 3D printing