Mere prediction about the future: Yajayo yanafurahisha, upo tayari?

5. 3D printing technology

Dunia ipo kasi mno, na hii kasi sijui kama itamuacha mtu salama. Si ajabu tukawa tunakata lile shina la mti tulilokalia, ni jambo la kuhuzunisha lakini hatuna jinsi ndio tumeshafika huko. Miaka ya nyuma kidogo kabla teknolojia haijakuwa ilimhitaji mtu aandike kila kitu kwa kutumia mkono na peni, leo hii unaweza kuchapisha hata vitabu 1000 ndani ya saa moja. Hii ni 1D printing, dunia sasa imefika kwenye 3D printing, ambapo mtoto akivunja kikombe mama anawasha printer anachapisha kikombe kingine anakoroga uji.

Tumeona 3D bioprinters zimefika uwezo wa kuprint viungo bandia, mifupa, ngozi, pua, maskio, mapafu na vitu vingine vingi sana. Viwanda vingi sana sasa wanatumia 3D printer, Google imetoa takwimu kuwa zaidi ya 11% ya viwanda wamehamia kwenye 3D printing. Hapa ndugu zangu wengi watakosa ajira miaka 20 ijayo ambapo karibia 95% ya viwanda watakua wanatumia 3D printers.

Dunia tumefika hatua ambayo tunaweza sasa kutengeneza vitu kama drones,viatu,urembo,vifaa vya muziki,vifaa vya magari na ndege, nguo.Yani utashangaa unaposhangaa kuona 3D printer inaprint 3D printer mwenzake, tayari zipo Printers zinazoprint printer.

Wakati kila mtu anawaza kuunda driverless car mzee baba Kevin Cringer kaamua kutuletea 3D printed car kupitia kampuni yake ya Divergent 3D. Makampuni makubwa kama KIA, BMW, Strati tayari nao wameanza kuprint magari, yani gari unalichapisha kama gazeti.

Mwaka jana tumeshangazwa baada ya nyumba ya kwanza kuwa printed na 3D printers, start up company moja huko San fransisco wameweza kujenga nyumba nyumba nzima kwa 3D printer ndani ya masaa 24.

Hivi majuzi China na Dubai wamejenga maghorofa marefu zaidi duniani yenye floor 5 ndani ya siku 17. AUE tayari wameanza mpango wa kuprint sky scraper ndefu zaidi kuwahi kuwa 3D printed. Ndugu zangu wahandisi watu wa michoro, quantitative survey, wabeba zege watakuwa na hali ngumu sana miaka 10-20 ijayo. Wazalishaji wa simenti, mbao, mabati na wafyatua matofali sijui watasurvive vipi.
8062191dd7be5232c79cbcdd02dcc55b.jpg
nyumba iliyojengwa kwa teknolojia ya 3D printing











 
Mkuu nilikuwa nakusapoti ila nmegundua wewe ni muongo na ni smartest tapeli eti fridge isafiliashwe kama pesa kudadeq acha uongo kuiyo ikitumwa itapaa hewani au tutakuwa tunaenda kutoa fridges m-pesa?

Kwa waliosema kazi ya pesa ni kutransfer immovable property ni wajinga?

Acha kudanganya watu hata bold ana kusupport kwa kukuonea aibu mkuu
Sipo vizuri kwenye kuandika ila ntajaribu kidogo kwa uelewa wangu

Imagine kama kuna izo machine zenye uwezo wa kuprint kitu in 3d way mfano nyumba,gari,kikombe nk
Kwaio mtu unachotakiwa kufanya ni kua na uthibitisho wa muamala wa kitu ulicho tumiwa mf. Tv
Utakwenda kwa wakala mwenye io mashine yenye uwezo wa kuprint ambapo kwa wakati uo ztakua zimesambaa kila kona kama vile m pesa. Then utamuonesha muamala wako wa kitu ulichotumiwa mf. TV .baada ya apo ataprinti ndani ya dakika 3 unaondoka na TV yako

Ndo mm nmefkria nkaona kama kuna ka uwezekano wa hiki kitu kwa staili io
 
Asee this is so thrilling. Watu watabisha tu but kwa wale tulioelewa, tushajua ni uwanja upi tunatakiwa kuchezea. Yaan mpaka kuna watu wanaamini Elan Musk ni Allien haki ya mama. Kwa wanaohitaji soft copy ya kitabu cha The Industries of the future nimekinunua tayari. Kama hamtojali tuchangiane kidogo kurudisha gharama kama 5000 tu mi ntakiupload hapa.
Daah nmekitamani
 
I believe the only problem will be economy, when you put a system on tha basis of economy many wont afford(I will). But most will wander and have nothing to do except opt out... Me thinking, we'll adapt to the future.
 
Lakini hiyo program ya computer iliyoshindana na bwana Gary si umetengenezwa na binadamu?
So, binadamu bado yupo juu
 
Asee this is so thrilling. Watu watabisha tu but kwa wale tulioelewa, tushajua ni uwanja upi tunatakiwa kuchezea. Yaan mpaka kuna watu wanaamini Elan Musk ni Allien haki ya mama. Kwa wanaohitaji soft copy ya kitabu cha The Industries of the future nimekinunua tayari. Kama hamtojali tuchangiane kidogo kurudisha gharama kama 5000 tu mi ntakiupload hapa.
Wewe ki upload tu ..tutakutoa mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umelishwa kinyama ww ndio sababu huwezi ona zaidi ya urefu wa pua yako.

Unalidhalilisha jina businessman dogo..Jiulize leo hii USA ni percentage ya youth wangapi wanaofanya icho mnachofanya au nyie ndio mna awarenes kuwazid wao..ww unahitaji huruma na maombi..
The list hatar sana
 
ONTALIO BOY jamaa wa FX teh teh teh ...nilivo ona thread hii nimecheka sana wengi wamefaidika na wengine wengi sana kupitia FX umewapoteza
 

Similar Discussions

233 Reactions
Reply
Back
Top Bottom