Mere prediction about the future: Yajayo yanafurahisha, upo tayari?!

ONTARIO

JF-Expert Member
Oct 16, 2013
1,891
2,000
Salute bosses!

Sina takwimu zozote (kama alivyosisitiza Anko), lkn binafsi nahisi nimekumbwa na ugonjwa wa micropsia, yani naona kama mwaka 2017 umekua mfupi kuliko miaka mingine yote, juzi tu tulikua Jan 2017 mara paap 2018 hii hapa. Mwaka ulioisha nilibahatika kusoma jumla ya vitabu 86, nikibakiza vitabu 14 kufikia lengo langu la kusoma vitabu 100. Kuna baadhi ya vitabu vimenisisimua sana, na mpk nikaona ni vyema kama nikishare nanyi vitu viwili vitatu nilivyotoka navyo. Nilisoma vitabu viwili vinavyohusu dunia na maisha ya siku zijazo, cha kwanza ni "The extreme future" the top trends that will reshape the world in the next 20 year pamoja na kitabu kilichoandikwa na Alec Ross kiitwacho the industries of the future


Yajayo yanafurahisha, upo tayari?!

Sipo hapa na siandiki huu uzi kupromote ama kudiscredit biashara ya mtu ama kampuni yoyote. Vodafone kampuni mama ya Vodacom wametuletea kampeni mpya na iliyopamba moto ya "The future is exciting, are you ready!". Ni kampeni maalumu ya kutuandaa tuwe na matumaini makubwa kuhusu siku zijazo hasa katika kupokea mapinduzi ya kiteknolojia, Voda wanabackup kampeni yao kwa jinsi ambavyo tayari simu zetu za mikononi zilivyobadili maisha yetu kiujumla, kuanzia kibiashara, kijamii, kiuchumi, kisiasa, kiburudani, kielimu nk. Tumeona haya madiliko kupitia operators kama Facebook, AirBnB, Doctor Pro, Amazon, PayPay, Uber, Alibaba, JamiiForums, Apple, Google, eBay hadi vitu kama M-Pesa. View attachment 670292

Teknolojia imefanya maisha yawe mazuri, mepesi na kufurahisha sana. Leo daktari akiwa nyumbani kwake anaweza kumfanyia diagnosis mgonjwa aliye kwake, kiziwi anaweza kuwasiliana na watu wengine kwa kuchomekewa kifaa cha wireless kinachomwezesha kusikia, tunaweza kula, kuvaa, kusafiri, kukutana, kuuza na kununua kwa kusukuma tu kitufe cha simu. Maisha yamebadilika sana ukilinganisha na miaka 15 iliyopita, lkn je ni kweli maisha ya siku za baadae yanafurahisha kama tunavyoaminishwa?? Je kuna mtu atabaki salama??, je kuna makampuni yatabaki salama??, vipi kuhusu baadhi ya nchi masikini kama TZ??

Nani atasuluhisha vita kati ya binadamu na teknolojia?? Wanadamu tumejiandaaje kupambana hiyo vita?? Nini utakua mwisho ikitokea kwamba teknolojia ikatuzidi kete?? Nani ataizui teknolojia isiendelee kutunyoosha kama tayari tumeshindwa kupambana nayo??
Tuliona ile project ya IBM technologies ya kutuonesha ulimwengu kuwa binadamu si lolote si chochote kwa teknolojia. Bwana Garry Kasparov mcheza chess bora zaidi kuwahi kutokea duniani, na mmoja ya watu wenye IQ kubwa zaidi duniani ya karibu 210, aliwekewa mezani pesa ndefu sana acheze Chess na deep thought (program ya kompyuta), bwana Garry akachukua mzigo ule akaingia ulingoni, ilimchukua dakika 15 tu kushinda game na kuigaragaza kompyuta. Kampuni ya IBM ikarudi mzigoni kuumiza kichwa na kuunda deep blue, ili waipambanishe na bwana Garry. Dunia ikashangazwa, Garry akagalagazwa kwa mara ya kwanza, akaomba mechi ya marudiano na deep blue, akagalagazwa tena... kuanzia hapo wanasayansi wakaamini ipo siku mwanadamu hatoweza kusimama kifua mbele kwa teknolojia. Haya yote yalitokea 1997, leo tupo 2018. Je ni nini tutegemee kuona miaka 10, 15, 20 ijayo?? Je ni sahihi tunavyokaririshwa kuwa yajayo yanafurahisha??

Twende pole pole!!

1. Artificial Intelligence (AI)

Sijui kama nipo sahihi kama nikitafsiri directly kama 'Akili ya kutengeneza', ni akili iliyounganishwa katika mashine ili kuweza kumsaidia binadamu baadhi ya shughuli, akili hii inaweza kufanya reasoning, problem solving, kujifunza nk. Hii idea iliibuka baada ya wanasayansi kuwa optimistic kuwa mashine zinawezwa kuunda kuzifanya kuwa na uwezo mkubwa kuliko binadamu, yani mashine zimuongoze binadamu badala ya binadamu kuongoza mashine. Mapinduzi yaliyofikiwa ni makubwa sana, lkn bado kuna mengi ya kushuhudiwa miaka ya baadae.

Kampuni ya Blue River technologies wametulitea smart agriculture yenye AI, tayari kampuni ya John Deere wameshawanunua. Jamaa wamedesign agricultural robots zenye uwezo wa kufanya kila kitu, kuanzia kupanda mbegu, kutambua muda sahihi wa kupiga dawa na mbolea, kufanya palizi hadi kuvuna na post harvest. Yani tayaru dunia inaelekea kufanya kilimo kwa programmed computee softwares, ambapo mtu anaweza kuwa Dar na shamba likawa Tukuyu au Manyoni, akaweza kulima, kuvuna na kuhifadhi bila kupigizana kelele na mfanyakazi hata mmoja. Tunajua zaidi ya 50% ya population ya Afrika wameajiriw kwenye sekta ya kilimo, nini hatima ya ajira zao iwapo tukifika ulimwengu wa 100% smart agriculture. Je ni kweli the future is exciting??

Dunia sasa hivi tuna magari tunayoyaita "futurist cars" yani ni magari yasiyohitaji dereva, yameunganishwa na rada moja kwa moja, pamoja na laser light, GPS pamoja na odometry yani mfumo unaoweza kujiendesha bila kukosea dira. Hii mada nitaizungumzia baadae kidogo kwenye hii thread, lkn tayari makampuni makubwa kama Uber tayari wameshaamza kutuletea haya magari, kampuni ya Ujerumani ya ZF wametoa ProIA. Tesla Autopilot tayari imeweza kujiendesha kwa usahihi wa asilimia 100 kutoka Los Angels hadi New York. Tukifika huko madereva watakua na ajira gani?
Tesla Autopilot

Kampuni ya PayPay sasa wana AI system za kutambua bidhaa za udanganyifu, magendo na mali haramu bila msaada wa wahudumu. Citi bank nao wamewekeza pesa kwemye kampuni ya Feedzai ambao wameunda mfumo wa kudukua na kutamvua mihamala ya udanganyifu kabla haijatekelezwa, vitu kama money laundering vinasimamiwa na robots. Mwaka huu ulioisha tumeona makampuni mengi sana kama Aidijia ya HongKong, sentient technologies, Nsaisense ya uswisi na Acitis ya Ujerumani wameunda mifumo ya AI kwajili ya fund and capital managements, nawaza mabenki hakianza kutumia AI hawa tellers na maafisa wengine wa benki wataajiriwa wapi.

Ray Kurzweil mkurugenzi mkuu wa uhandisi wa kampuni ya Google kwenye interview aliyofanya na FB live studio alieleza kidogo kuhusu theory yake ya "Singularity". Singularity ni hatua tutakayoifikia ambapo ukuaji ktk teknolojia hasa AI utasababisha uvumbuzi wa mashine zenye uwezo wa kiitelijensia maradufu kulinganisha na mwanadamu. Huko ndipo utampenda ama kumchukia Elon Musk kwa kuja na kampuni ya Neuralink, kiufupi mimi hua nasema tangu dunia iumbwe, hajawahi kutokea mwanadamu mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri na kufanya vitu vya ajabu kama Bilionea Elon Musk. Tumeona Neuralink walipofikia leo hii, wanasayansi wake wameweza kuunda electroencephalogram (EEG), kifaa kinachoweza kutambua signals za umeme ktk ubongo wa mwanadamu, baadae kuunganisha ubongo wa binadamu na computer, kisha kuuwezesha ubongo wa mwanadamu kuweza kulivestream taarifa zote ktk internet. Idea nzima ya Neuralink ni kuunganisha ubongo wa mwanadamu na computer pamoja na internet na kuweza kutunza taarifa zote kwenye kwenye cloud.

Yote hayo ni 9, kitu kinachonisisimua zaidi ni teknolojia ya Cyborg, guys the future is not not exciting kama tunavyoambiwa. Mimi sio mpenzi sana wa movies lkn nimemsikia sana huyu cyborg, sijui alikua anafanya nini kwenye hizo movies lkn ninachofahamu ni kuwa cyborg technology inatisha sana. Dunia tumefika hatua ambayo tunaweza kutengeneza bionic human beings, leo tunaweza kuunda viungo vya binadamu kuliko kipindi chochote kile, kuanzia macho, masikio, mifupa, ubongo... na hivi viungo vina efficiency kuliko viungo asili. Wanasayansi wana uwezo wa kupandikiza artificial brain ktk kichwa cha mwanadamy ili kuongeza IQ, wanatumia sumaku ya RFID. Prof Kevin Warwick ndio wapo mbele kwenye kusukuma cybernetic science, kuhakikisha kua miaka ijayo wanadamu wanaweza kuwa kama terminator na cyborg.
Prof Kevin na mwanafunzi wake wa Cybernetic


2. Artificial human being

Tangu dunia ianze haijawahi kutokea kipindi ambacho wanadamu wameenda extra mile kama kipindi hiki, tumefikia hatua ya kushindana na Mungu kuumba. Hata kama haupendi au hautaki, tayari kuna watu wameshafika huko, na miaka ya usoni tutarajie wajukuu zetu kuundwa maabara from scratch.

March 2017 wanasayansi ya chuo cha Cambridge waliweza kuunda kiinitete (embryo) ambacho kilidevelop ndani ya 3D scaffold na kuweza kubehave kama human embryo. Haya ni mapinduzi makubwa ktk sayansi ya bioengimeering. Wanasayansi hao kwasasa wanatafiti juu ya kuweka uhai ktk kiinitete hiko, mwisho wa kila kitu tutashuhudia kiumbe hai aliyetengenezwa maabara, na baadae mika kama 20 au 30 tuone mwanadamu wa kwanza wa maabara atakuaje.

Tayari tuna uwezo wa kuunda viungo vya ndani from scratch, ubongo, moyo, mapafu, ini, figo nk. Teknolojia ya CRISPR imewezesha kampuni ya eGenesis kutengeneza genetic engineered pigs ambao viungo vyao vya ndani vinaweza kuwa transplanted kwenda kwa binadamu bila madhara yoyote kiafya. Trust me, tutafika ulimwengu ambao mtu anachagua kuwa na mapafu kama ya muogeleaji mashuhuri Phelps ama moyo kama wa mwanariadha Usain Bolt ama ubongo kama wa Prof Steve Hawkings. Cha ajabu viungo hivi haviwezi kushambuliwa na bacteria ama virusi wala uvimbe wa tumor unaosababisha kansa.

Tumeona mwaka jana kampuni ya Organovo ya San Diego walianza kuuza 3D bioprinters za kwanza zenye uwezo wa kuchapisha viungo vya binadamu. Mwishoni mwa mwaka jana tukaona kituo cha utafiti cha Wake forest wameweza kutumia mashine hizo kutengeneza ngozi, misuli,mishipa ya damu na vibofu. Figo waliyoitengeneza imeweza kufanya kazi kwa ufanisi wa juu sana kwenye mwili wa mnyama wa majaribio. Cha ajabu zaidi unatumia dakika 40 kuprint kiungo, yani kama vile mtu anachukua selfie.

Wanasayansi wanamalizia utafiti ambao utawezesha wanadamu wa kawaida kuishi miaka 150.

3. Afya, dawa na matibabu

Hii sekta inakua kwa kasi isiyo ya kawaida, kuna mapinduzi mengi tyr tumeshuhudia na tutarajie kuona maajabu miaka 10-20 ijayo. Acha niorodheshe chap chap baadhi ya vitu tulivyoachieve mpk sana.

(a). Intelligent knife (iKnife)


Watafiti wa tiba wa chuo cha imperial tayari wamegundua na kufanyia utafiti kisu janja cha iKnife. Kisu icho kinatumia teknolojia ya electrosurgery, wakati kinatumika kwenye upasuaji umeme hupita kwa kasi na kuleta joto kwenye tishu za mwili, huku ikiwa na faida ya kupunguza upotevu wa damu, husababisha tishu hizo kutoa mvuke unaoambana na moshi, moshi hua unanyonywa 1 kwa 1 ka kuingia kwenye 'mass spectrometer' kisha kifaa hiko hutoa signals kueleza magonjwa yaliyopo kwenye mwili wa mgonjwa. Zoezi hili hadi kukamilika ni chini ya dakika 10 tu. Ndipo tulipofika huku, mwaka jana wale vijana wa Taiwan walishinda tuzo ya x prize baada ya kugundua kifaa walichokiita Dexter chenye uwezo wa kudetect magonjwa 13 bila haja ya kumuona daktari.
iKnife

(b). Google brain

Hii nimeizungumzia kidogo lkn kwenye Artificial intelligence, lkn ngoja nitilie msisituzo tena. Google kama Google walimkodi Prof Ray Kurzeil (huyu naweza kusema ndio futurist maarufu zaidi duniani kwa sasa - unaweza kutazama ted talks zake kama getting ready for hybrid thinking). Google brain ni concept ya kuUpload ubongo wa binadamu kwenye computer ili kuweza kutufanya tuishi kidigitali. Kwa mantiki hiyo ubongo wetu utaunganishwa na kompyuta, kisha App ya kuchunguza mwili itakua installed kwenye kompyuta, huvyo kuufanya ubongo kuweza kugundua hali ya afya ya mwili muda wowote ule bila haja ya kumuona daktari... Lets see how fast this might happen, still crossing my fingers.

(c).Tricorder

Dunia inapoelekea yawezekana kusiwe na umuhimu wa kuwa na maabara, madaktari nk. Vifaa kama tricorder vinabadili kabisa jinsi tunavyopata huduma ya afya na matibabu. Mwaka jana tricorder ya kwanza ililetwa kwenye uso wa dunia, kifaa hicho kimeundwa na darubini kali (high power microscope) na simu janja (smart phone), hivyo unaweza kupima magonjwa ya ngozi kutumia tu fingerprint scanner ya simu, unaweza kupima DNA nk. Kifaa hiki bado kinaendelea kusukwa na naamini miaka 10 ijayo hakitakua kama kilivyo leo. Sasa najiuliza physicial, dentist, optician, medical doctor, clinician na manesi watakua na kazi gani hivi vifaa vikiwa yebo yebo.
Tricorder

(d). IBM Watson

IBM baada ya kuunda deep blue iliyomgaragaza bwana Garry, sasa waliamua kutumia muda wao kudesign vitu ambavyo vina tija za moja kwa moja, wana hiki kifaa chenye uwezo wa kung'amua magonjwa kwenye mwili wa mwanadamu bila kufanya vipimo, tena kwa accuracy ya juu kuliko madaktari.
Uwepo wa vitu kama smart contant lens yenye uwezo wa kusimamia magonjwa kama kisukari, kansa na BP vinatuonesha dunia itafananaje miaka 10 ijayo.http://www.jamiiforums.com/mobile-gallery/2b744777c81be809c38428df58407e5e.j

Mwaka jana pekee kifaa cha Da Vinci Robot kimefanya upasuaji milioni moja na nusu kwa ufanisi wa asilimia mia bila daktari kusika hata mkasi mmoja.[IMG]http://www.jamiiforums.com/mobile-gallery/e2d21feb09f024207f1e431defeabec2.jpgDa vinci robot

4.Sector ya Usafiri

Tumeona maendeleo makubwa sana ktk hii sekta, kuanzia enzi za kina nabii Nuhu na Ayubu kutumia farasi hadi , hadi kizazi cha kutumia 4 wheel chariots, hadi mnamo mwaka 1885 ambapo Karl Benz aligundua gari la kwanza, kisha 1905 Wright brothers wakaufundisha ulimwengu jinsi ya kuunda na kurusha ndege. Hapa kati kumekuwa na maboresho mengi sana ktk sekta ya usafiri, lkn bado wanasayansi wamekuwa na kiu kubwa sana ya kuja na teknolojia za kibabe zaidi.

Tumeona ujio wa segway human transporter, tena zimekuja kwa kasi ya ajabu sana. Naamini kabisa miaka 20 ijayo segways zitakua tofauti sana na hizi za leo. Achilia mbali selfdrive cars, hiyi ni kitu ambayo ipo na itashika kasi siku si nyingi sana, na nina imani watoto na wajukuu zetu wataishi katika kizazi ambacho kuondesha gari ni kosa la jinai. Kama asili itaturuhusu kuishi miaka 20 kutoka leo, tutegemee yafuatayo

(a). Hyperloop

Bado hua sina uhakika kama Elon Musk ni mwanadamu mwenzetu ama ana genes za eliens, sielewi!!. Tangu alivyopropose concept ya hyperloop mwaka 2012, mambo yamekuwa moto. makampuni mengi makubwa kama Virgin, Transpod, Arrivo, hyper chariot nayo yameingia kwenye challenge ya kudevelop hyperloop ya uhakika zaidi.

Hii kitu tayari ipo na tuitegemee very soon, najiuliza tu hali itakuaje miaka ya baadad. Aug 28 mwaka jana Elon Musk alipost video kwenye page yake ya IG kuonesha jinsi Hyperloop WARR pod inavyokata upepo na katika 1 ya comments zake alieleza kua ile ni sample ya hyperloop iliyoundwa na mwanafunzi tu wa Tesla tena kwa bajeti ndogo sana, fikiria nini kitatokea katika project kubwa na ambago imetengewa bajeti nono.


Kiufupi hyperloop ni mfumo wa usafirishaji ambao pods ama kontena zilizoungwa na sumaku zinaweza kusafiri kwa kasi kubwa sana ndani ya tubes ama mifereji tupu (vacuum tunnels). Hyperloop inaweza kusafiri kwa speed ya kilomita 1200 kwa lisaa. Sawa na kutumia dakika 52 kutoka Dar - Mwanza. Tayaru tunnels kadhaa zimeundwa kuikaribisha hiyo teknolojia mfano Vienna - Budapest, Estonia - Finland, Helsinki - Stockholm, Spain - Morocco, Abudhabu, Liverpool - Glasgow, Poland, Cardiff - Glasgo, Germany, US nk. Tayari tumeona hyperloop 1, hyperloop Delft pamoja na Hardt hyperloop, hivyo tutegemee kuona mapinduzi makubwa zaidi na zaidi.

Najiuliza hizi elimu zetu za vyuoni za uhandisi, je wahandisi wetu wataweza kwemda sambamba na hii kasi? Au tunachomeshana tu mafuta?

(b). Flying cars (Magari yapaayo)

Zamani kidogo siku 1 niliwahi kupiga story na mdingi mmoja, tulikutana hospitali; akawa anaelezea kuhusu mambo ya magari kupaa, nikawa namuona kama mpayukaji, mtafuta sifa na mtu asiyefahamu alisemalo. Lkn baada ha kuona kasi katika teknolojia ya drones, autonomous cars pamoja na AI, nadiriki kusema yule mdingi alikua makini sana na futurist wa nguvu.

Mwaka jana tumeona makampuni kama Aeromobil, Boeing, E-volo, Aeronatics, Lilium Aviation yakizindua mifano (prototypes) ya magari yapaayo. Mbali zaidi tumeona kampuni ya PAL-V wameanza kuuza gari lake la Liberty pioneer flying car na mwaka huu ndio wataanza usambazaji mkubwa. Uber pia walizindua program ya "Uber elevate' yenye kusudi la kuchochea ukuaji wa hii teknolojia kwa kuandaa harambee maalum ya kusisimua serikali, mashirika binafsi, makampuni makubwa ya usafirishaji na utengenezaji magari. Tayari makampuni kama Google na skype wameinvest pesa ndefu sana kwenye makampuni changa kama Kitty na Lilium Aviation ili kuchochoe ukuaji wa magari yapaayo.
flying cars

Kampuni ya Colossus Airbus nao wameshatoa concept 3 za magari yao, na wanajitamba kuwa mwaka huu watabadili kabisa upepo wa hii teknolojia na tutegemee mambo adimu zaidi na zaidi miaka ya baadae.

(c) Electric transportation

Mwaka jana CEO wa Benz, Dieter Zetsche alipokuwa na interview alisema sasa hivi kampuni yake haishindani tena na makampuni kama General Motors, Volkswagen, BMW n.k bali anaumizwa kichwa na makampuni kama Tesla, Google, Amazon na kadhalika. Hakuna mtu anampa stress kama Elon Musk, na hii yote imeletwa na idea ya electric cars. Haya ni aina ya magari yasiyochoma fuel yani hayatumii mafuta wala gesi, hivyo basi hayahitaji kufanyiwa service, kubadili oil n.k hapa ndipo tutaona gerage zote na mafundi wa mtaani wakikosa ajira.

Tayari dunia imeshafika hapa, makampuni karibu yote ya uzalishaji wa magari yamehamia huku.Soon hatutaona haya magari tuliyonayo leo. Nchi kama Norway, India na Germany wameshasema by 2025 hakutakuwa na magari ya Petroli kwenye nchi zao. Hayo yote tisa, 10 ni kuwa tayari kuna electric planes.

Magari ya umeme kwa sasa yanatumia mabetri ya lithium kama smartphone zetu, tablets na laptops. Sasa hivi watafiti wanaumiza vichwa kupata jibu la muda mrefu katika kuongeza nguvu katika hizi betri.Yani tutafika kipindi ambacho ukicharge gari unaweza kuendesha mwezi mzima bila presha ya kuingia petrol station kunyonya mafuta wala kuchaji betri. Hapa ndipo mafuta yatakosa soko na kuwa rank moja na maji, tukifika huku waarabu hawatakua na thamani waliyonayo leo. Naona wazi mafundi garage, wauza mafuta na oil wote watabaki wanasaga meno, madini kama graphite, silicon na lithium vitakuwa lulu sana.

Wakati dunia nzima inawaza kuhusu electric cars siemens aliamua kuustajabisha ulimwengu na inawezekana dunia nzima ikaadoptteknolojia yao. Wao walidai kuwa suluhisho si electric cars bali ni kuelectrify barabara. Hii kitu yao inajulikana kama eHighway. Hii teknolojia imeundwa maalumu kwa ajili ya mabasi makubwa na malori lakini teknolojia ina kasi ya umeme, tusishangae miaka 20 ijayo tutakuwa katika hizi eHighway. Kiufupi hizi eHighway gari linapata charge moja kwa moja likiwa barabarani, so hakuna haja ya mafuta,gesi wala betri kama za gari za Tesla. Hata makonda na wapiga debe hawatakuwa na mwisho mzuri.
Model ya awali ya eHighway, kuonesha jinsi malori yatakavyokua yanapata charge directly kwa kuendeshwa barabarani bila haja ya kuwa na mafuta wala gesi

(d) Teleportation

Hii kitu inaumiza sana kichwa, ni moja ya vitu vinavyonifanya nianze kufikiri kuwa mwanadamu anaweza kuwa smart kuliko supernatural power (sijasema Mungu). Concept nzima ni ngumu kidogo na imekaa kinadharia zaidi kuliko uhalisia wake, lakini ndo hivyo tena wanasayansi wanaendelea kutufungulia dunia.

Teleportation ni sayansi ya kusafirisha kitu kutoka sehemu moja hadi sehemu nyingine bila kukatiza katika ulimwengu wa kimwili. Ndugu zangu tuliosoma vitu vigumu tunafahamu kua katika quantum electrodynamics, kuna uwezekano kusafirisha nishati (energy) hali (state) na chembe chembe ndogo(microscopic particles) katika hali tupu(vacuum state).

June mwaka jana tumeona particle kubwa ya kwanza imeweza kuwa teleported kutoka katika uso wa dunia hadi kwenye ulimwengu (universe), mpango mzima ulitekelezwa na wanasayansi wa China, chini ya usimamizi wa prof Hooke wa chuo kikuu cha Oxford.

Naamini Mambo hayatakuwa hivi miaka 20-30 ijayo, mambo yatakuwa moto sana , zamani miaka 20 iliyopita hatukuwa na smart internet, ili mtu kufikisha ujumbe ilibidi uandike barua, kisha mtu aisafirishe from point A-B, leo hii mtu anatuma email kutoka Mbezi hadi Arlington ndani ya sekunde 2 au 3. Tutafika kipindi ambacho teleportation itatuwezesha kituma mizigo kama fridge, simu, viatu kama tunavyotuma email na labda hata wajukuu zetu wakawa wanasafiri kama email. You never know!!

5. 3D printing technology

Dunia ipo kasi mno, na hii kasi sijui kama itamuacha mtu salama. Si ajabu tukawa tunakata lile shina la mti tulilokalia, ni jambo la kuhuzunisha lakini hatuna jinsi ndio tumeshafika huko. Miaka ya nyuma kidogo kabla teknolojia haijakuwa ilimhitaji mtu aandike kila kitu kwa kutumia mkono na peni, leo hii unaweza kuchapisha hata vitabu 1000 ndani ya saa moja. Hii ni 1D printing, dunia sasa imefika kwenye 3D printing, ambapo mtoto akivunja kikombe mama anawasha printer anachapisha kikombe kingine anakoroga uji.

Tumeona 3D bioprinters zimefika uwezo wa kuprint viungo bandia, mifupa, ngozi, pua, maskio, mapafu na vitu vingine vingi sana. Viwanda vingi sana sasa wanatumia 3D printer, Google imetoa takwimu kuwa zaidi ya 11% ya viwanda wamehamia kwenye 3D printing. Hapa ndugu zangu wengi watakosa ajira miaka 20 ijayo ambapo karibia 95% ya viwanda watakua wanatumia 3D printers.

Dunia tumefika hatua ambayo tunaweza sasa kutengeneza vitu kama drones,viatu,urembo,vifaa vya muziki,vifaa vya magari na ndege, nguo.Yani utashangaa unaposhangaa kuona 3D printer inaprint 3D printer mwenzake, tayari zipo Printers zinazoprint printer.

Wakati kila mtu anawaza kuunda driverless car mzee baba Kevin Cringer kaamua kutuletea 3D printed car kupitia kampuni yake ya Divergent 3D. Makampuni makubwa kama KIA, BMW, Strati tayari nao wameanza kuprint magari, yani gari unalichapisha kama gazeti.
gari la kuprint

Mwaka jana tumeshangazwa baada ya nyumba ya kwanza kuwa printed na 3D printers, start up company moja huko San fransisco wameweza kujenga nyumba nyumba nzima kwa 3D printer ndani ya masaa 24.

Hivi majuzi China na Dubai wamejenga maghorofa marefu zaidi duniani yenye floor 5 ndani ya siku 17. AUE tayari wameanza mpango wa kuprint sky scraper ndefu zaidi kuwahi kuwa 3D printed. Ndugu zangu wahandisi watu wa michoro, quantitative survey, wabeba zege watakuwa na hali ngumu sana miaka 10-20 ijayo. Wazalishaji wa simenti, mbao, mabati na wafyatua matofali sijui watasurvive vipi.
nyumba iliyojengwa kwa teknolojia ya 3D printing

6. App, Mobile and internet technology

Sihitaji kuzungumza sana hapa kwakua nina uhakika wote Tumeshuhudia wenyewe kwa macho yetu ndani ya miaka kumi mapinduzi makubwa yaliyoonekana.

Mobile Apps zimebadili game kabisa... Leo mtu haitaji kuangalia taarifa ya habari saa 2 usiku wakati habari zinaflow JF mwanzo mwisho... leo mtu haitaji kutangaza bidhaa yake radio fulani wakati kuna FB, IG nk. Dunia yote imehamia kwenye App store na Playstore, TV zinarun kwenye YouYube na Vimeo, Radios zinarun kwenye TuneIn, Ajira zinatangazwa LinkedIn na CV zinatumwa kwa Xender.

Chakula hatufati tena restaurant bali Jumia... Wallet hazihitaji tena credit cards, kila kitu kipo square... Taxi hatuzifati tena kituoni, kila kitu uber... Huitaji tena mambo ya kukata tiketi kienyeji, kila kitu ni YPlan... Wanafunzi wanasoma Duolongo na Voxy, hata hawa wetu wanaweka kupiga msuli kupitia DesaApp... Huitaji tena dakika, unaweza kupiga popote duniani kwa hangouts dialer au whatsapp messenger... window shopping unafanya kwa App... dunia nzima imesogezwa kiganjani. Hapa watu wengi sana sana sana wanapoteza na watapoteza ajira zao, biashara nyingi zinakufa na zitakufa.

MySugr inaweza kumonitor kisukari, SimpleC kumonitor Alzheimer, Cellscope inaweza kufanya diagnosis ya sikio na xRapid inaweza kufanya vipimo vya Malaria, TB na yellow fever... baada ya mzunguko wote unaingia GoodRx ama MymedicalShopper kuchukua dawa pharmacy. Je bado tuseme the future is exciting wakati hatuna maandalizi. Nikihitaji mwanasheria sihitaji kwenda kwa xxx advocates ama yyy attorneys, kila kitu unachohitaji unakikuta Fastcase ama Notary.

Elon Musk wetu tena!!
Mwaka 2015 alitangaza mpango wa kusambaza internet dunia nzima, internet yenye uwezo wa kukamata kila kona ya dunia kwa kasi ya mara 3 ya 4G. Na Musk alivyo mtu wa mikakati tuliona 2016 alivyotuma rockets yake ya speceX iliyolipua satellites za FaceBook zilizopo kwenye orbit. Sasa hivi anapambana kuuwa makampuni pinzani kama OneWeb, Qualcomm, Teledesic, SoftBank. Musk ameshapata vibali vya Federal Communication Commision na sasa atalaunch satelites zake 4425, project itakayomgharimu $10 bilioni. Mpango wa Elon ni kusambaza internet dunia nzima, kila pembe kwa gharama nafuu ambapo taarifa za awali zinasema GB 300, unlimited calls pamoja na unlimited messages kwa dollar 10 tu kwa mwezi. Makampuni mengi ya mitandao ya simu yatakufa kifo cha mende, kodi Anko atakusanya kwenye viwanda vya bia na sigara. Na hapo ndipo tutaona Elon akiwa the richest man to ever live on earth.

(7) Banking, money $ Financial services

Hii kitu nilitaka niiweke kama Blockchain technology, lkn kiukweli nimechoka sana kutype na hiyo blockchain ni mada ndefu ndefu ndefu, nikianza kiandika sitamaliza hivi karibuni so nimeamua kusummarize kama banking and financial institution.

Utafiti uliofanywa na Global Investment in FinTech walitoa takwimu kuwa mwaka jana mabenki yote kwa ujumla duniani yalitumia $355 billion katika sector ya IT pekee ambayo ni kiwango kikubwa zaidi kuwahi kutumika kwa mwaka mmoja tangu dunia ianze. FinTech bado inakua polepole lakini leo hii mtu anatembea na benki mfukoni kwake, unaweza kufanya mihamala kwa kusukuma kitufe tu, benki karibu zote zimeanza kuadopt online services, kufanya transactions kupitia mobile App, dunia leo tuna eWallets, vitu kama eloctronic payments operators kama Skrill, Neteller, PayPal, webmoney, payoneer, nk nk. Haya ni mapinduzi makubwa sana ktk Fintech na naamini kuwa bado tutashuhudia mambo moto moto miaka 10 ijayo. Nikudokeze tu kidogo kuhusu future ya hii industry.

Utakubaliana na mimi kuwa hii ni moja ya mhimili muhimu zaidi duniani, na hivyo tutarajie mapinduzi yasiyo ya kawaida... hapa ndio ndugu zangu wengi zaidi wataachwa nyuma, watabaki wanatumbua macho.

Kikubwa zaidi ninachokiona kwenye hii industry in Blockchain Technology. Hii teknolojia kidogo ni ngumu na ipo complicated sana kumuelezea mtu lakini kiufupi ni sytem inayoweza kurekodi mihamala kati ya pande mbili kwa ufasaha umakini na uthibitisho mkubwa mno na kwa njia ya kudumu.

Blockchain ya kwanza duniani iliundwa na mtu mmoja asiyejulikana ama kundi la watu wasiojulikana anayetambulika kwa jina la Satoshi Nakamoto mwaka 2008, teknolojia hiyo ikaanza kutumika mwaka 2009 kwa product ijulikanayo kama Bitcoin.Juzi tumeona Bitcoin 1 ikiwa na thamani ya $20,000. Muda huu natype huu uzi tayari kuna zaidi ya cryptocurrencies 1300, kama nilivyosema awali, teknolojia ni kama radi, kamwe huwezi kuizui kwa mkono, hata kama hatuyataki haya mapinduzi bado yatatufikia tu.

Ninachoamini miaka kadhaa pesa itakuwa full digitalized na decentralised, hakutakuwa tena na hizi noti na sarafu bali tutakuwa na cryptocurrencies nyingi, tayari dunia ipo huko, lkn watu hawajaanza kuadapt mabadiliko, hapa ndio hua nasema only the fit will survive. Mzee baba Bill gates tumeona akitia mzigo kwenye crypto iitwayo Ethereum sawa na makampuni kama Itel, JP Morgan, Watu kama kina JohnMcafee na Mark Cuban wote wanatia mizigo yao huku. Kama mtu aliyesmart mwaka 2012 angenunua bitcoins 102 kwa $100 tu,leo hii mtu huyo huyo angekuwa na $1,667,000 kutoka $100. Hapa ndio inakuja ile, I wish, I could, I would, I should.

Mimi binafsi hivi vitu nimechelewa kuvijua, na wala sijilaumu na sasa nimetumia muda mwingi sana kuvifahamu kwa undani. Kama Jan 2017 mtu angewekeza $1000 kwa kila 1 ya top 7 cryptocurrency yani Bitcoin, Ethereum, Ripple, Litecoin, Monero, Dash na Neo leo hii mtu huyo angekua anavuna $1,156,000 kiutani utani tu. Mimi Sept mwak jana nilitumia $800 kununua ripple 8012, leo hii kila coin 1 ya ripple inathamani ya $3 na si ajabu by December mwaka huu coin 1 ya ripple ina thamani ya $100. Siku si nyingi sana nimeinvest $103 kwenye coin inaitwa mintchip nimenunua coins 100,050 ndani ya masaa machache nimeweza kutripple capital na hapa plans zangu niendelee kuhold hadi December ambapo labda coin 1 itakuwa na thamani ya $1 kwa hivyo investment yangu ya $100 itakuwa imeleta zaidi ya $100,000 kiutani utani.Tumeona hii inawezekana baada ya ripple kutoka $0.0063 hadi $4 kuanzia Jan 2017-Jan 2018.Huku ndipo dunia ilipofikia. Muda huu unasoma hii thread fahamu kuwa Larsen Founder wa Coin ya Ripple ndio tajiri namba 5 duniani, kawaacha kina Mark Zuckerback wa FB na hata mafounder wa Google Larry Page and Sergey Brin. Mpk mwaka unaisha jamaa atakua anamtuma Bill Gates sokoni akamnunulie ugoro.

ONTARIO
Cofounder and CEO, TMT.


*****************************************

My current book on the table

Nimetumia muda mwingi sana kucompile hii thread, nimechoka sana. Lakini nikitulia baadae kidogo nitakuja kutoa hutimisho yenye mawazo yangu, ushauri, way forward, nini kifanyike ili tuwe on the safe side, nini business owner wanabidi wafanye, mtu mmoja mmoja, mashirika na hata serikali kwa ujumla wake. Uzi mrefu Nimeshindwa hata kuurudia, hivyo mtanisamehe popote penye typing error, pia epuka kuquote huu uzi ili kupunguza kero kwa watumia simu.
Huku ndipo teknolojia inapotupeleka na hatuwezi kupingana na matokeo.
 

Khalidoun

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
2,740
2,000
5. 3D printing technology

Dunia ipo kasi mno, na hii kasi sijui kama itamuacha mtu salama. Si ajabu tukawa tunakata lile shina la mti tulilokalia, ni jambo la kuhuzunisha lakini hatuna jinsi ndio tumeshafika huko. Miaka ya nyuma kidogo kabla teknolojia haijakuwa ilimhitaji mtu aandike kila kitu kwa kutumia mkono na peni, leo hii unaweza kuchapisha hata vitabu 1000 ndani ya saa moja. Hii ni 1D printing, dunia sasa imefika kwenye 3D printing, ambapo mtoto akivunja kikombe mama anawasha printer anachapisha kikombe kingine anakoroga uji.

Tumeona 3D bioprinters zimefika uwezo wa kuprint viungo bandia, mifupa, ngozi, pua, maskio, mapafu na vitu vingine vingi sana. Viwanda vingi sana sasa wanatumia 3D printer, Google imetoa takwimu kuwa zaidi ya 11% ya viwanda wamehamia kwenye 3D printing. Hapa ndugu zangu wengi watakosa ajira miaka 20 ijayo ambapo karibia 95% ya viwanda watakua wanatumia 3D printers.

Dunia tumefika hatua ambayo tunaweza sasa kutengeneza vitu kama drones,viatu,urembo,vifaa vya muziki,vifaa vya magari na ndege, nguo.Yani utashangaa unaposhangaa kuona 3D printer inaprint 3D printer mwenzake, tayari zipo Printers zinazoprint printer.

Wakati kila mtu anawaza kuunda driverless car mzee baba Kevin Cringer kaamua kutuletea 3D printed car kupitia kampuni yake ya Divergent 3D. Makampuni makubwa kama KIA, BMW, Strati tayari nao wameanza kuprint magari, yani gari unalichapisha kama gazeti.

Mwaka jana tumeshangazwa baada ya nyumba ya kwanza kuwa printed na 3D printers, start up company moja huko San fransisco wameweza kujenga nyumba nyumba nzima kwa 3D printer ndani ya masaa 24.

Hivi majuzi China na Dubai wamejenga maghorofa marefu zaidi duniani yenye floor 5 ndani ya siku 17. AUE tayari wameanza mpango wa kuprint sky scraper ndefu zaidi kuwahi kuwa 3D printed. Ndugu zangu wahandisi watu wa michoro, quantitative survey, wabeba zege watakuwa na hali ngumu sana miaka 10-20 ijayo. Wazalishaji wa simenti, mbao, mabati na wafyatua matofali sijui watasurvive vipi.
nyumba iliyojengwa kwa teknolojia ya 3D printing 

katib mkoa

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
902
1,000
Mkuu nilikuwa nakusapoti ila nmegundua wewe ni muongo na ni smartest tapeli eti fridge isafiliashwe kama pesa kudadeq acha uongo kuiyo ikitumwa itapaa hewani au tutakuwa tunaenda kutoa fridges m-pesa?

Kwa waliosema kazi ya pesa ni kutransfer immovable property ni wajinga?

Acha kudanganya watu hata bold ana kusupport kwa kukuonea aibu mkuu
Sipo vizuri kwenye kuandika ila ntajaribu kidogo kwa uelewa wangu

Imagine kama kuna izo machine zenye uwezo wa kuprint kitu in 3d way mfano nyumba,gari,kikombe nk
Kwaio mtu unachotakiwa kufanya ni kua na uthibitisho wa muamala wa kitu ulicho tumiwa mf. Tv
Utakwenda kwa wakala mwenye io mashine yenye uwezo wa kuprint ambapo kwa wakati uo ztakua zimesambaa kila kona kama vile m pesa. Then utamuonesha muamala wako wa kitu ulichotumiwa mf. TV .baada ya apo ataprinti ndani ya dakika 3 unaondoka na TV yako

Ndo mm nmefkria nkaona kama kuna ka uwezekano wa hiki kitu kwa staili io
 

katib mkoa

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
902
1,000
Asee this is so thrilling. Watu watabisha tu but kwa wale tulioelewa, tushajua ni uwanja upi tunatakiwa kuchezea. Yaan mpaka kuna watu wanaamini Elan Musk ni Allien haki ya mama. Kwa wanaohitaji soft copy ya kitabu cha The Industries of the future nimekinunua tayari. Kama hamtojali tuchangiane kidogo kurudisha gharama kama 5000 tu mi ntakiupload hapa.
Daah nmekitamani
 

palangana

JF-Expert Member
Jan 14, 2017
509
500
I believe the only problem will be economy, when you put a system on tha basis of economy many wont afford(I will). But most will wander and have nothing to do except opt out... Me thinking, we'll adapt to the future.
 

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
537
1,000
Lakini hiyo program ya computer iliyoshindana na bwana Gary si umetengenezwa na binadamu?
So, binadamu bado yupo juu
 

Ollachuga Oc

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
10,127
2,000
Asee this is so thrilling. Watu watabisha tu but kwa wale tulioelewa, tushajua ni uwanja upi tunatakiwa kuchezea. Yaan mpaka kuna watu wanaamini Elan Musk ni Allien haki ya mama. Kwa wanaohitaji soft copy ya kitabu cha The Industries of the future nimekinunua tayari. Kama hamtojali tuchangiane kidogo kurudisha gharama kama 5000 tu mi ntakiupload hapa.
Wewe ki upload tu ..tutakutoa mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Baba Swalehe

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
16,249
2,000
Umelishwa kinyama ww ndio sababu huwezi ona zaidi ya urefu wa pua yako.

Unalidhalilisha jina businessman dogo..Jiulize leo hii USA ni percentage ya youth wangapi wanaofanya icho mnachofanya au nyie ndio mna awarenes kuwazid wao..ww unahitaji huruma na maombi..
The list hatar sana
 

LUKAMA

JF-Expert Member
May 28, 2017
486
500
ONTALIO BOY jamaa wa FX teh teh teh ...nilivo ona thread hii nimecheka sana wengi wamefaidika na wengine wengi sana kupitia FX umewapoteza
 
Top Bottom