Titicomb
JF-Expert Member
- Jan 27, 2012
- 11,291
- 17,737
Mkuu unajidanganya sana.1. Afrika (ukiacha nchi ya Afrika Kusini) bado mno. Kama mtu ananunua gari la 2001 leo hii 2018 halafu akiliingiza nchini analiita jipya ni tatizo.
2. Siasa za Afrika hazitaruhusu hizo teknolojia kwa hofu ya wapiga kura kukosa kazi. Mambo hayo yataishia huko huko Washington.
kama mambo yangekuwa hivyo hadi leo tungekuwa tunatumia Printer za Dot matrix badala ya Laser Jet Printers, au tungekuwa tunakomaa na barua au fax.
Mkuu nani alijua miaka 15 iliyopita hapa bongo matumizi ya smart card kama ya mwendokosi itatumika kwenye usafiri wa umma?
Nani alijua BVR kwenye upigaji kura itakuja haraka hivyo? Na karibuni tu itakuwa rahisi kumtambua mhalifu kwa kutumia fingerprints maana database ndio hiyo tayari tulitoa alama zetu kwenye zoezi la vitambulisho vya Taifa na uchaguzi mkuu.
Kwa taarifa yako matumizi ya digital currency(Hiyo Block chain) nchi masikini ambazo watu hawana vitambulisho vizuri, mabenki kam westunion hakuna huko vijijini watafaidika sana na hizi Bitcoin pale watakapotumiwa pesa na ndugu zao akina Drogba toka Ulaya au Mbwana Samatta toka huko Ulaya wanakotafuta riziki. wanachohitaji ni Smartphone tu ambazo sasa ni gharama nafuu zimeenea hadi vijijini.
Unafikiri yule aliekamatwa Julius Nyerere international Airport (JNIA) na dola kadhaa cash angetumia Bitcoin au digital currency yeyote angekamatwa?
Kwa kutumia banking system iwe swift, Visa, n.k. hizo lazima utakuwa controlled tu lakini sio hizo digital currency(Block chain kama Bitcoin).
NB: Hapa sifundishi watu kukwepa mkono wa sheria au cybercrime au ukwepaji kodi au utakatishaji fedha. Natoa mifano hii kwa lengo la kuelimisha tu(For Educational Purposes).
Tafuta hii documentary mpya kabisa.
Magic Money: The Bitcoin Revolution (2017)