Meno ya tembo tunduru yawanufaisha askari wa maliasili. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Meno ya tembo tunduru yawanufaisha askari wa maliasili.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Watunduru, Jan 20, 2012.

 1. Watunduru

  Watunduru Senior Member

  #1
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Msemo wa mbuzi hula sawa na urefu wa kamba yake unazidi kudhihiri ktk wilaya maskini na yenye utajiri ya tunduru baada ya maofisa ktk idara mbalimbali wilayani humu kutumia ofisi zao kujinufaisha binafsi.ktk idara ya maliasili ni jambo la kawaida kwa kila uchao kusikia meno ya tembo yamekamatwa lakini hakuna kesi iliyoko mahakamani bali wahusika huishia kupeana rushwa vichochoroni na kuwaachia watuhumiwa.

  Ktk tukio la hivi karibuni usiku wa tar 18/01/2012 kuamkia tar 19 maafisa wa maliasili wanaotambulika kwa majina ya Dulla,Stani,Limbega na wenzao,wakiwa ktk gari aina ya Toyota pick up nyeupe, walikamata pikipiki mbili zilizobeba kiasi cha kilogram 150 za meno ya tembo eneo la shule ya sekondary Mgomba.

  Ktk kuendeleza rushwa na ufisadi waliziachia pkpk kwa rushwa ya shilingi laki saba kila pikipiki na meno ya tembo waliyachukua lakini badala ya kupeleka kituo cha polisi kwa hatua zaidi walikwenda kuhifadhi nyumbani kwa afisa mmoja wapo kwa lengo la kuuza.

  Haya ni matukio ya kila siku na yameanza muda mrefu kiasi kwamba kama tungekuwa na serikali makini hali hii ingeweza kukomeshwa lakini si kwa serikali hii.

  Source:eyewitnes

  Ktk hatua nyingine maafisa wezi wa T.R.A Haule na mwenzake Ndunguru pamoja na afisa mwingine mwizi toka songea wiki iliyopita waliwafuata wafanyabiashara na kuomba rushwa ya shilingi laki 5 kwa kila mmoja kwa ahadi ya kuwahurumia ktk kuwakadiria kodi jambo ambalo ilidhihirika ni rushwa na utapeli,wapi taasisi ya kusimamia na kuendeleza rushwa?
   
 2. s

  sawabho JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Kama una ushahidi, toa taarifa kwa Mamlaka husika. Huko hakuna PCCB?
   
 3. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu ahsante kwa taharifa!.....hivi huko Tunduru kuna ofisi ya CDM? na je,wananchi wa huko wanapenda chama gani?
  ccm,cuf au cdm? Nimewahi kutembelea wilaya hiyo kama miaka 7 iliyopita....nakumbuka chama cha cuf kilikuwa na nguvu
  sana! je,kwa sasa hali ikoje?
   
 4. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,809
  Likes Received: 2,584
  Trophy Points: 280
  Hivi majuzi container mbili zilizosheni meno ya tembo zimezuiliwa mombasa ke. Meno yalikuwa yamehifadhiwa kwenye viroba yva Kilombero sugar hivo upo uwezekano mkubwa yalitokea hapa nchini. Ufisadi wa kutisha huu.
   
 5. Watunduru

  Watunduru Senior Member

  #5
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  pccb ndugu yangu ni mambo ya kufikirika,wote ni hao hao wanalindana tu,ukitaka matatizo we jihusishe nao.
   
 6. Watunduru

  Watunduru Senior Member

  #6
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nguvu ya chadema kwa sasa ni nchi nzima,cuf ilikuwepo kweli enzi hizo lakini kwa sasa inavyodorora kitaifa hali ni hivyo hivyo ktk ngazi za chini.
   
 7. Watunduru

  Watunduru Senior Member

  #7
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  pccb ndugu yangu ni mambo ya kufikirika,wote ni hao hao wanalindana tu,ukitaka matatizo we jihusishe nao.
   
 8. Mr. Bigman

  Mr. Bigman JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,853
  Likes Received: 629
  Trophy Points: 280
  Watunduru, mbona hao maafisa wa Tra unaowataja wala rushwa,huyo Haule ni mlokole mzee wa Kanisa? Iweje aombe rushwa?. Ila huyu Ndunguru nakubaliana na wewe, ni kafisadi fulani hivi
   
 9. Watunduru

  Watunduru Senior Member

  #9
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  asikudanganye mtu ndugu yangu,ogopa sana watu wanaojifanya wafia dini,wanatumia dini kama kichaka kuficha ujambazi wao,wafanya biashara wote hasa walio ktk VAT waulize tu watakuambia wamechangishwa kiasi hicho cha pesa.
   
 10. myao wa tunduru

  myao wa tunduru JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 9, 2010
  Messages: 615
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  baada ya kifo cha MAZEE (R.I.P) sidhani kama CUF itakuwa na nguvu iliyokuwa nayo miaka ya nyuma.....
   
Loading...