Mengine ya EPA yaibuka

Zee la shamba

Member
Oct 17, 2007
55
3
UPELELEZI kuhusu mahali zilipo Sh133 bilioni zilizochotwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupitia Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) umeibua mambo zaidi mapya yanayokihusisha Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwananchi Jumapili limebaini.


Habari za uhakika kutoka ndani ya Timu ya Rais inayochunguza suala hilo la kifisadi, zinasema kuwa baadhi ya watuhumiwa ambao tayari wamehojiwa, bila kuuma maneno yao, walisema kuwa sehemu ya fedha hizo zilipelekwa CCM kwa ajili ya shughuli za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.


Vyanzo mbalimbali ndani ya timu hiyo inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, vimelieleza Mwananchi Jumapili kuwa, kwa jinsi upelelezi unavyokwenda CCM haiwezi kukwepa tuhuma hizo.


Kwa mujibu wa chanzo kimojawapo, mtuhumiwa mmoja alipohojiwa alikiri kuchukua mabilioni ya fedha kupitia kampuni yake, lakini akakataa kurejesha zote, kwa madai kuwa sehemu ya fedha hizo zilichukuliwa na watu wa CCM kwa ajili ya uchaguzi.


Habari zinasema kuwa mtuhumiwa mwingine aliamua kwenda kuhojiwa akiambatana na wakili wake na kuweka sharti kuwa kila atakachosema kiandikwe jinsi kilivyo, na katika maelezo yake alieleza kuwa sehemu ya fedha hizo alimkabidhi kigogo mmoja wa chama na serikali.


Uchunguzi zaidi wa Mwananchi Jumapili, umebaini kuwa hata fedha hizo zinazodaiwa kupelekwa CCM hazikufika zote kutokana na baadhi ya mafisadi �wajanja� kukiingiza mjini chama hicho.



Wadadisi wa masuala ya kisiasa wanasema kutajwa kwa CCM katika upelelezi huo unaiweka timu hiyo inayojumuisha ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) mahali pagumu ama katika kutaja majina ya wahusika au kuwafikisha mahakamani, kutokana na ukweli kuwa hatua hiyo inaweza kuiweka CCM mahali pabaya.


Kwa mujibu wa wadadisi hao, CCM inaweza kujisafisha katika kikao chake cha Halmashauri Kuu kitakachofanyika wiki ijayo kijijini Butiama, mkoani Mara kwa kuwatosa makada wake muhimu ambao wanadaiwa kuhusika moja kwa moja na suala la EPA.


Aidha, wadadisi hao wanasema hata fedha zilizokwenda CCM itakuwa vigumu kupata uthibitisho wake kwani aliyekuwa Mweka Hazina wa Chama hicho wakati, Salome Mbatia alifariki katika ajali ya gari Oktoba mwaka jana.


Chanzo kingine ndani ya timu hiyo, kimesema hali iliyopo sasa inaweza kuishia kama ile ya Richmond ambapo bunge lililazimika kuunda kamati yake na kutoa mapendekezo yaliyolitikisa taifa, licha ya awali kufanyika uchunguzi wa PCCB ambayo hatimaye ilionekana imeipamba rushwa badala ya kupambana nayo.


Kuibuka kwa mammbo hayo mapya, kunazidi kufunua sehemu ya ukweli alioeleza Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kuhusu kuhusika kwa CCM katika ufisadi huo na uwezekano mdogo wa mabilioni hayo kurejeshwa.


Vile vile maelezo hayo yanaipa nguvu hofu ya wananchi ya kutotajwa kwa majina ya wahusika kuwa hatua hiyo ina lengo la kuficha sehemu ya uweli na kuongeza uwezekano wa wahusika kutotajwa kabisa kutokana na unyeti wa nyadhifa zao.


Wakifafanua kuhusua hofu hiyo walipokutana na wahariri hivi karibuni, Mwanyika na IGP Mwema, mbali na kukataa katakata kutaja majina ya wahusika, walisema kipaumbele cha timu hiyo ni kutafuta zilipo pesa hizo na kuzichukua; baadaye watawafuatilia wahusika.


Hata hivyo, maelezo yao hayakuwa na jibu la moja kwa moja kuhusu hatua watakazochukua, kwani mwisho wa timu hiyo ni kuwasilisha ripoti kwa Rais Jakaya Kikwete na yeye ndiye atakuwa na uamuzi wa mwisho miezo mine ijayo.


Katika mkutano huo ambao Mkurugenzi wa PCCB hakuhudhuria, viongozi hao wa timu walishindwa kutoa maelezo ya kutosha kwa nini hawakutumia mtindo uliozoeleka wa wakamata watuhumiwa kwanza na kuwahoji wakiwa mikononi mwa dola, badala yake wakatumia mtindo wa kuwahoji wakiwa huru na kama ni kuwakamata iwe baadaye.


Vile vile si Mwanyika wala Mwema aliyeeleza kwa uwazi benki au akaunti zinapowekwa fedha zinazorudishwa na mafisadi hao, licha ya kusema tu ni akaunti maalum, jambo ambalo linaondoa urahisi wa kuifuatilia kubaini kama kweli Sh60 bilioni zilizorudishwa zimo au kiinimacho.


Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, John Chiligati, alikana chama hicho kushiriki katika ufisadi kwenye akaunti ya EPA.


Alisema madai hayo ni siasa za kupakana matope ambazo si sahihi katika jamii inayotaka kujadili mstakabari wa maendeleo yake.


�EPA ina tume ambayo haijatoa majibu. Sio sahihi kuanza kushikana uchawi wakati Tume haijamaliza kazi na hizi sio siasa nzuri�Ni siasa za kupakana matope,� alisema Chiligati


Alipoulizwa kama EPA ni miongoni mwa agenda zitakazojadiliwa katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa, Chiligati alisema hana uhakika, isipokuwa kikao hicho kitakajadili hali ya kisiasa na mambo yote yanayoathiri siasa za nchi.


�Sina hakika kama itakuwepo, isipokuwa katika mjadala huo wa siasa za nchi, linaweza kujitokeza kwa kuwa ni moja ya mambo yanayoathiri siasa hizo,� alisisitiza Chiligati.


Katika hatua nyingine, mpango wa Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila kufungua kesi dhidi ya mafisadi wa EPA umepokelewa kwa hisia tofauti kuwa una lengo la kuwalinda mafisadi.


Akizungumza na Mwananchi Jumapili kwa simu mkazi wa Ving�ung�uti, Joram Mushi, alisema mpoango huo wa Mtikila una lengo la kuwanufaisha mafisadi kwa kunyamazisha mijadala yote ya EPA kwenye vyombo vya habari, bungeni na kuizuia Timu ya mwanyika kufanya kazi.


Mtikila mwenyewe aalipoongea na gazeti hili alitetea uamuzi huo, kuwa una lengo zuri lakini akakiri kuwa utazuia vyombo hivyo ambavyo yeye haoni umuhimu wake kuendelea na kazi.


�Mahakama haitazuia mijadala kwenye vyombo vya habari. Inaweza kuzuia bunge na serikali peke yake�Kwani bunge lilipojadili Richmond nini cha maana kimefanyika, si umeona kwamba wameishia tu kupongezana. Mimi nataka mahakama itoe amri ya kuunda tume huru ya uchunguzi wa kina, walioiba washtakiwe na walipe pesa walizopora,� alisema Mtikila


Alikataa mpango wake huo kuwa na lengo la kuwanufaisha mafisadi.

Source: Gazeti Mwananchi
 
Mi naona bora wote tukakae msituni tume ya mwanyika inasema haitaki kuwataja hadi pesa zirudishe si ndio????It means wanawajua sana tena ni washkaji wao ndio nini sasa??
sasa hiki chama kikianguka nani/chama gani kitasimama??
 
Mmmmh....hivi yule Ruge alisema anaweza kueleza ukweli ili muhusika mkuu akamatwe.!!..itakuwa mojawapo ya maajabu makuu
 
Eleweni jambo moja Wahusika n wenyewe kw wenyewe ,kesi ya Nyani unaipeleka KW Ngedere?
Hapa nia ni kufwatilia hela kwn Serikali imekaukiwa.
 
Back
Top Bottom