Mengi: Wafungwa watumike kufichua majambazi nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mengi: Wafungwa watumike kufichua majambazi nchini

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Feb 28, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  Mengi: Wafungwa watumike kufichua majambazi nchini


  na Mwandishi wetu, Moshi


  [​IMG] VYOMBO vya dola vimeaswa kuwatumia wafungwa waliomaliza muda wao ili kuwafichua majambazi wanaoendelea kufanya uhalifu hasa wa matumizi ya silaha.
  Sambamba na hilo wananchi wameaswa kutowanyanyapaa wafungwa waliomaliza muda wao kwa kuendelea kuwaona wahalifu na badala yake iwape fursa sawa kushiriki fursa zote za kijamii.
  Rai hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, wakati wa harambee ya kuchangia Chama cha Waliokuwa Wafungwa (ERST), iliyofanyika katika ukumbi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Dayosisi ya Mashariki, mjini Moshi.
  Mengi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo, alisema wafungwa wengi wanawajua wahalifu na inawezekana kwamba walipata kushiriki pamoja katika matukio ya ujambazi na makosa mengine ya jinai kabla ya kufungwa.
  “Kwa sababu hiyo, wafungwa wanaorejea uraiani baada ya kumaliza vifungo vyao, wanaweza kuwa hazina kubwa ya kufichua uovu na waovu katika jamii kama wakishirikishwa vyema na polisi na jamii kwa ujumla,” alisema Mengi.
  Mengi ambaye aliahidi kukisaidia chama hicho kuanzisha miradi ya kujitegemea, alisema kwa bahati mbaya jamii imekuwa ikiwatenga na kuendelea kuwaona wahalifu wafungwa waliorejea uraiani, hali ambayo huwafanya wengi waishi kwa shida kiasi cha kutamani kufanya tena uhalifu, ili warudi gerezani kupata huduma za bure ingawa ni za mateso.
  Kwa mujibu wa Mengi, wafungwa wa zamani watumike hata kutoa ushauri nasaha kwa wenzao wanaomaliza muda wao magerezani, ili waweze kubadili maisha yao.
  “Nilikuwa nazungumza na katibu wa chama hiki cha wafungwa, Dk. Afred Kaaya, kwamba alipotupwa jela miaka kumi, alitarajia kwamba angerejea tena uraiani akiwa hai? …. Akasema hapana, alijua angekufa na ndio ungelikuwa mwisho wa maisha yake. Lakini leo yupo hapa, amepata ajira yake kama daktari na sasa ni katibu na amebadilisha kabisa maisha yake.
  “Kumbe jamii inaweza kubadilisha maisha ya watu wanaotoka gerezani kwa kuwashirikisha na kuwapa haki katika fursa mbalimbali za kijamii, hivyo naomba jamii isiwaone hawa ndugu zetu kwamba ni wahalifu wa kudumu na kuamua kuwatenga,” alisema Mengi.
  Kwa mujibu wa Mengi, wafungwa wawapo gerezani wapewe ushauri wa kiroho na viongozi wa dini na magereza, ili kuwajengea msingi wa kuwa raia wema baada ya kumaliza vifungo vyao.
  Mwenyekiti huyo wa IPP, aliwaasa viongozi wa chama hicho kujipanga katika kuanzisha miradi ya maendeleo badala ya kutumia fedha walizochangiwa katika matumizi yasiyo na tija.
  Naye Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Mashariki, Martin Shayo, aliitaka jamii kuwasaidia wafungwa wanaorejea uraini ili waweze kubadili maisha yao ya uhalifu na kuwa watu wema.
  Askofu wa jimbo la Moshi wa Kanisa Katoliki, Aman Masawe, alisema kuwa wahalifu wote wanatupwa gerezani na wale wanaoendelea kufanya uhalifu, hutengenezwa na jamii inayowazunguka.
  Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini, Musa Samezi, alisema kuwa serikali imetoa hekari kumi kwa ajili ya chama hicho cha wafungwa ili waweze kuanzisha miradi ya kilimo na kuweza kujikomboa kiuchumi kama njia ya kuwafanya waachane na uhalifu.
  Wakati huohuo, aliyekuwa mfungwa katika gereza la Karanga mkoani hapa, Shafii Kondo, ametoa siri kuwa amewahi kupora fedha na magari ya Mengi.
  Shafii ambaye ni Mwenyekiti wa EPST, alitoa siri hiyo jana mbele ya Mengi wakati wa harambee ya kukichangia chama hicho.
  Huku akimwacha Mengi akiwa amepigwa butwaa, Shafii bila woga alisema katika kipindi chake cha ujambazi, aliwahi kuyapora magari na fedha za kampuni ya vinywaji baridi ya Bonite Bottlers, inayomilikiwa na Mengi.
  “Sio siri, mimi leo naona kama muujiza kukaa meza moja na watu wakubwa kama Mzee Mengi, maaskofu, kamanda wa polisi, mkuu wa magereza na mkuu wangu wa wilaya wakati nilikuwa jambazi.
  “Nimeiba na kuyateka nyara mara nyingi magari ya Cocacola ya Mzee Mengi. Hapa nasema ukweli tu jamani, wengine hapa tunatembea na roho za watu tuliowaua wakati wa ujambazi.
  “Lakini leo nimetoka gerezani, nimekuwa raia mwema na sasa ni mwenyekiti wa chama cha wafungwa wa zamani. Tumekoma, hatutaki tena ujambazi,” alisema Shafii ambaye alitumikia kifungo cha zaidi ya miaka 15.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  Wazo ni jema lakini Mengi hakutaja mikakati ya utekelezaji.........................labda kaonyesha mwanga na njia ya kupita.................................

  Siku zote kufungwa kunaonekana na jamii ni malipizi badala nafasi ya kwenda kujirekebisha....................................Tuanze na prison reforms to make our prisons be refomatory centers rather places of punishmnet and getting even..........................

  Tuanza kwa kuanzisha vifungo vya nje tutungfe sheria ambazo zitakataza msongamano ndani ya jela zetu na kuwapa huduma muhimu kama vitanda, vyoo na kila chumba wasizidi wafungwa wanne....................................baada ya hapo mawazo ya Mengi yanaweza kuwa yamejengewa msingi wa kuanza kufanyiwa kazi.......vinginevyo tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu...........if you treat prisoners badly they are unlikely to co-operate with you after serving their terms.....................................it is that simple...................................................................
   
 3. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  na nani afichue mafisadi?
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo wafungwa ndiyo wanaishi na mafisadi? Naotaa au hii thread heading ni real?
   
Loading...