Invisible
JF Admin
- Feb 26, 2006
- 16,285
- 8,364
Waziri Mkuu za Zamani Jaji Joseph Warioba amesema anakusudia kumfungulia mashitaka ya kashfa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP na Media Solutions, Reginald Mengi.
Jaji Warioba, aliambia Mtanzania katika mahojiano ya Simu jana kwamba pamoja na Mengi, atayashitaki magazeti ya This Day na Kulikoni, wachapishaji wake, wahariri na waandishi wa habari.
Kauli hiyo ya Jaji Warioba inatokana na habari zilizochapishwa na magazeti hayo wiki hii zikidai kwamba Warioba anahusika na Kampuni ambayo inaelezwa na magazeti hayo kuwa imesajiliwa kwa ujanja na ambayo inahusishwa na chama tawala CCM
"Huko nyumba waliandika habari kama hizi. Tukawaomba watuombe radhi. Hawakutujali Badala yake wameendelea kuandika bila hata kutupa nafasi ya kueleza upande wetu.
Sisi ni watu ambao tunaamini Mahakama kuwa ndiko ambako mtu anaweza kupata haki yake. Hivyo tumeamua kuwafungulia mashitaka. Sasa siwezi kusema tutafungua lini, lakini itakuwa ni hivyi karibuni. Nitafungua mimi binafsi na kampuni ya Mwananchi GOld Mining nayo itafungua kesi yake," alisema warioba.
Alisema si kweli kwamba kwa kampuni hiyo kuna utata wowote na kwamba kilichochapishwa katika magazeti hayo ni ugongo wa dhahiri.
"Ninachoweza kukuambia tuu ni kwamba habari hiyo ni ya uongo. Walichoandika, pamoja na kwamba hawakujali kuniuliza kabla ya kuandika, ni uongo mtupu. Lakini kwa kuwa sisi tunaamini katika Mahakama, sasa sitazungumza sana kuhusu jambo hilo kwa kuwa tayari liko mahakamani," alisema na kuongeza:
"Nchi hii inaendeshwa kwa misingi inayofuata Sheria. Mimi naheshimu Sheria, kwa kuwa kati ya mambo haya mengine yako mahakamani, siwezi kusema zaidi. Naiachia mahakama.
Kama hatimaye jaji warioba na kampuni ya Mwananchi watakwenda mahakamani, hiyo itakuwa mara ya tatu katika kipindi kifupi kwa mengi na timu yake kufikishwa huko.
Wiki iliyopita balozi wa Tanzania nchini Italia, aliyemaliza muda wake hivi karibuni, Profesa Costa Mahalu, alimshitaki Mengi, wahariri na waandishi wa magazeti yake kwa kashfa akidai fidia ya billion 12
Shitaka hilo la Profesa Mahalu lilikuwa ni la pili, likiwa limetanguliwa na lile la mfanyabiashara wa Dar es Salaam, Yusuf Manji, ambaye anamdai mengi SH. Billion 100 kwa kashfa ya magazetini.
Source: MTANZANIA