Mengi VS Rostam: Where is the Government?

Imagine MBOWE ndio rais je hali ingekuwa tofauti?

There is something nice about new people, new party new rule! They set new motion to everything! Sudden people realize they have power! New government want to prove how different they are from the previous government. So, in many different way dynamic of power changes and new problem emerge and for sure it won't be the current problems! And when they mess up so bad, citizens will deal with them upfront because they have realized the power of change!
 
How can the government investigate itself? Mnacheza nyinyi. Hapa hakuna lolote zaidi ya sarakasi na mazingaombwe.

Halafu malumbano ya hawa wawili sidhani kama yanaihusu serikali. Wao waachwe wapakane kwenye vyombo vya habari na mwishowe wataacha wenyewe.

Kinachoniogopesha tu ni kwamba malumbano ya hawa watu yana divert attention kabisa kutoka mafisadi nyangumi na papa wengine kama Li Mkapa na lile Li Mbuna, Mi Chenge..Mi Mahalu na mingineyo.

Upuuzi mtupu unaoendelea hapa.

Maandishi yako msumari kabisa ,hayana utata ,nawashangaa wengi humu JF kwa kujiegemeza katika moja ya kambi hizi za Chama Cha Mafisadi ,sasa naelewa kuwa kuna waliojivalisha ngozi ya kondoo tatizo ngozi yenyewe haina tena manyoya ya kujihifazi na kipupwe hiki kinachopiga kwa kasi.

Nani Mengi nani Rostam ? Hawa ni nani katika Chama tawala ? Ni lini wamejivua uanachama ? Ninachokiona ni kuwa kila mmoja anaonyesha makeke yake na zaidi wanatutaka tuelewe nani ni juu juu juu zaidi ,katika serikali hii ya kiwete.

Yeyote atakae sapoti upande katika hawa na wengine wa aina hii atakuwa nae ni fisadi ,hivi mnapoambiwa CCM imejaa mafisadi mlifikiri ni wale wapiga debe ?
 
Hii imetundikwa jana na NasDaz member mpya katika thread ya mapenzi nadhani ni ugeni tu lakini nahisi inahitaji kupewa nafasi, kwa idhini yako mkuu NasDAz Nomba kuwakilisha


Rostam Aziz/Reginald Mengi na Mpiga Filimbi wa Amelin


Ni bahati mbaya sana Rostam Aziz hana ubavu wa kumshinda Mzee Reginald Mengi katika uwezo wa kuwateka wananchi kiakili! Uwezo huo anao Reginald Mengi ambapo umwangiliapo tu wakati anapoongea, sura yake inatoa ujumbe wa mtu safi, mpole, mkarimu na ambae watu hupenda kumuonea kutokana na upole wake! Hata hivyo, kwa upande wa Rostam Aziz hutachelewa kuiona jeuri ya pesa na majivuno wakati wa maongezi yake! Labda kinachoonekana kutoka kwa wote, hususani kwa yule asiyetaka kuumiza kichwa, ni uchungu walionao watu hawa kwa ndugu zao watanzania!


Kwangu mimi, si Rostam wala Mengi ambae tuhuma zake zimetokana na uchungu alionao kwa nchi hii! Hawa wote hawana tofauti yoyote na Mpiga Filimbi wa Amelini aliyekusudia kuwatokomeza panya na ambapo mwisho wa mchezo na watoto wa vijiji vile nao wakapotelea kusikojulikana walipokuwa wanamfuata mpiga filimbi wa Amelini!


Kama nilivyosema awali, Rostam keshazidiwa kete na Mzee Mengi tangu zamani hizo! Wakati Rostam alijikita zaidi kuwashika viongozi na watendaji mbalimbali wa serikali, Mzee Mengi alijikita zaidi katika kuziteka hisia za watu, hususani wanyonge! Mengi alishafanikiwa tangu zama hizo kujionesha kuwa yeye ni mtu safi, mpole, mnyonge, muonewa wivu, na kubwa zaidi ni mpenda maskini na watanzania kwa ujumla!


Hata hivyo, nasikitika kwamba si Rostam Aziz wala Reginald Mengi aliyefanikiwa kunipata kwenye tundu lake.


Hata hivyo, kwavile naamini kati yao ni Reginald Mengi ndie aliyefanikiwa kubeba ipasavyo mikoba wa Mpiga Filimbi wa Amelini, basi nahisi kusononeka kutokuwamo kwenye msafara wake! Sina shaka yoyote kwamba mpiga filimbi huyu alipopita mtaani kwetu, mimi nilijumuika na watoto wenzangu kumfuata nyumanyuma huku tukifaidi utamu wa muziki kutoka kwenye filimbi yake! Sifahamu ni nini kilinitokea, lakini kabla hajakata kona kiasi cha kutoweka kwenye upeo wa macho kutoka nyumbani kwetu, nilishituka na kurudi mbio nyumbani huku nikihema!Pamoja na yote hayo, hivi sasa nahisi kama najutia maamuzi yangu ya kumuacha Mpiga Filimbi wa Amelini aende zake! Rafiki zangu wote ambao nilikuwa nao awali kwenye msafara wa mpiga filimbi; bado hawajarejea! Siamini kama wamepotea, bali nahisi wanaendelea kufaidi muziki wa filimbi, na ndio maana hawataki kurejea nyumbani! Kwani si wapo wanaoamini kwamba hata wafu nao kuna kitu wanafaidi huko kuzimu na ndio maana hawataki kurejea duniani!? Sio siri, naowaonea wivu watoto wenzangu, nahisi wanafaidi muziki wa mpiga filimbi!
Good! Nimeikumbuka sababu iliyonifanya nimshiti Mpiga Filimbi wa Amelini aende zake na mimi kurejea nyumbani, haijalishi hata kama hivi sasa najilaumu! Pamoja na ala tamu za filimbi, lakini mashairi yalikuwa ni yaleyale ya akina Marijan Rajabu, TX Moshi William, Muhidini Ngurumo na wengineo wengi kama hao! Ni mashairi ambayo nahisi yalishayachosha masikio yangu! Lakini kwavile natamani kwenda kuungana na watoto wenzangu ili tuserebuke wote na ala za filimbi yake, basi namshauri angalau aweke chorus (kibwagizo) ya muziki wa kizazi kipya!


Ngoja kwanza nijaribu kutengeneza theory kama ita-fullfil:
First Law:
“To every grand corruption action there must be two dependent bonds responsible for completing the corruption circuit, these are business people and decision makers bonds!”


Second Law: “For any corruption circuit to be disconnected and allow no more electrons to pass through,there must be a committed techinician who’s able to expose both bonds from a connected terminal”


Mzee Mengi bado hajanishawishi kwamba yeye ni committed technician kwavile haja-expose both bonds! Mbaya zaidi ni kwamba napata mashaka zaidi na commitment yake kwavile bonds alizozi-expose ni zile tu zinazowafanya watu wahisi kuwepo kwa conflicting objectives! Kama tunakubaliana angalau kwa 50% na theory zangu basi wale ambao Mzee Mengi hajawataja ni Decision Makers, ambao wengi wao kama sio wote ni wanasiasa na watendaji wakuu wa serikali au taasisi za umma!


Binafsi, hawa watu kwangu ndio muhimu zaidi kuliko hao akina Jeetul Patel! Si kwamba wakina Rostam si watu muhimu katika hili, ninachosema ni kwamba watu ambao hawajatajwa ni wale waliowekwa sehemu walizopo ili kulinda maslahi ya watanzania! Jeetul Patel na wenzake hawafanyi biashara kwa maslahi ya watanzania, bali wanafanya kwa maslahi yao binafsi na ndio maana hawaoni aibu kuwahujumu watanzania walio wengi. Endapo ningepewa nafasi ya kuulizwa ni bond ipi itajwe na ipi isitajwe, basi sina shaka ningeitaka bond ya decision makers ndio itajwe. Hii ni kwavile muda si mrefu bond hii itajinadi mbele yetu kwamba wao ni watu safi hivyo wangependa kutuongoza na kuendelea kulinda maslahi yetu kumbe ndio wala rushwa wakubwa!


Mzee Reginald Mengi alikaririwa kwamba kuna mafisadi kama kumi hivi nchini, miongoni mwao watano ni mafisadi papa ambao wote ni wafanyabiashara! Sasa kama nia yake si kuwamaliza washindani wenzake wa kibiashara ni kwanini asiwataje hao mafisadi wengine ambao bila shaka ni wanasiasa hata kama ni mafisadi sangara au vibua?! Kama kweli aliwataja mafisadi papa kwa ajili ya uchungu alionao nao kwa watanzania basi hana budi kuwataja na mafisadi sangara kwavile ndio hasa tuliowaweka ili wayalinde maslahi ya watanzania wote! Asipowataja, basi nitahisi wale aliowataja amesukumwa zaidi na:
1. Maslahi Binafsi ya Kibiashara,
2. Inawezekana kweli Mzee Mengi ana ndoto za kugombea urais wa nchi hii hivyo asingependa kujiundia maadui wa kisiasa ambao bila shaka wengi wao kama sio wote watakuwa ndio wajumbe wa NEC
3. Kama kweli Mzee Mengi anakwepa kodi basi anaogopa kuwaumbua wanasiasa ambao ndio wadau wakuu katika kuwezesha ukwepaji kodi wa wafanyabiashara wakubwa. Maana yangu ni kwamba anawaogopa kwavile anajuwa ameshawahi kuwatumia katika kukwepa kodi!


Kama nilivyoeleza hapo awali, natamani kumfuata mpiga filimbi huyu wa Amelini, lakini aweke kibwagizo cha Bongo Flavor kwa kuwataja na mafisadi sangara!
 
Mengi, Rostam wamweka Kikwete njia panda

Mwandishi Wetu Mei 6, 2009

Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

Iddi imba ampinga Rostam kuhusu NICO

KUNA maoni kuwa ombwe la uongozi ndilo ambalo linachangia katika malumbano, ambayo yameigawa nchi, kati ya wafanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi na Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, ambao kila mmoja anamtuhumu mwenzake kwa kuhujumu Taifa.

Baadhi ya wanazuoni, wanasiasa wastaafu na raia wa kawaida, wameiambia Raia Mwema wiki hii kwamba malumbano hayo hayawezi kuachwa yaendelee, na kwamba sasa lazima Serikali ionyeshe njia katika kuyamaliza kwa kuwatosa, japo wote wawili wanaelezwa kuwa watu wa karibu na Rais Jakaya Kikwete.

Mmoja wa wanazuoni wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), amesema kinachojulikana kwa Watanzania wote ni kwamba hakuna Serikali ya Rostam Aziz au Reginald Mengi, na kwamba ukimya wa Serikali unaweza kuchochea wananchi kujichukulia sheria mikononi.

Mhadhahiri Mwandamizi wa UDSM, Profesa Mwesiga Baregu, ameiambia Raia Mwema kwamba Serikali ina wajibu wa kuchunguza tuhuma zinazorushwa kutoka kila upande na kwamba kilichofanywa na kila mmoja kati ya Mengi na Rostam ni kila mtu kutoa vidokezo tu na sasa Serikali ichukue hatua.

“Kama Serikali ikiendelea kukaa kimya italeta mguno miongoni mwa wananchi na hiyo ni hatari, wanaweza (wananchi) kuamua kuanza kujichukulia sheria mkononi,” alisema Profesa Baregu na kuongeza:

“Katika maelekezo yake au hatua itakazochukua, Serikali inapaswa kulinda haki za raia kwa mujibu wa sheria zilizopo lakini kwa maslahi ya Taifa.”

Naye Mhadhiri Msaidizi wa UDSM, Bashiru Ali, alisema malumbamo yanayoendelea hayatakuwa na maana kama maisha ya Watanzania hayataboreshwa.

“Kuna jukumu la Serikali kusimamia na kutoa haki na mwelekeo kwenye mkanganyiko huu…hii ni Serikali ya wananchi si ya Rostam Aziz au Reginald Mengi…tupate msimamo wa Serikali,” alisema Bashiru na kusisitiza:

“Maelezo au tuhuma za watu hao wawili zote zinagusa maslahi ya Taifa, na ni bayana kuwa kama Taifa tumeibiwa, sasa nasema mjadala umenoga serikali itoe mwelekeo.”

Hata hivyo, alionya kuwa katika mvutano huu zipo dalili zisizo na manufaa kwa Taifa, dalili zinazohusisha udini, ukabila na hata ubaguzi wa rangi.

Kwa upande wake, Mbunge wa Viti Maalumu, na ambaye aliwahi kuwa waziri katika wizara mbalimbali na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Anna Abdallah, haoni mvutano huo kama utasaidia kuwapunguzia matatizo Watanzania.

“Hayo ni mambo yasiyohitaji kupewa nafasi ya kipaumbele katika vyombo vya habari na maeneo mengine…msiwaendekeze…yapo mambo mengi muhimu na si hayo,” alisema Anna kwa muhtasari.

Waziri na Mbunge wa zamani wa Ilala, Dar es Salaam, Iddi Simba, hakutaka kuzungumzia kwa kina mvutano huo lakini akasema anasikitishwa na hatua ya Rostam Aziz kuihusisha Kampuni ya Uwekezaji ya Taifa (NICO) katika mzozo kati yake na Mengi, akisema hakuna ukweli wowote kuhusu hilo.

“Madai haya yanapohusishwa na NICO hayana maana wala ukweli wowote…hapa Rostam amejenga hoja isiyohusika, nimesikitishwa sana.

“Nafahamu tamko rasmi litatolewa na Mwenyekiti wa NICO, lakini niseme tu kwamba Mengi hakuhusika na chochote kama ilivyoelezwa na Rostam kuhusu NICO. Alijitoa mara baada ya kubaini kuwa mdogo wake Benjamin Mengi anataka kujiingiza katika uwekezaji na alipinga hatua hiyo,” alisema Simba ambaye ni kati ya vigogo wakubwa ndani ya NICO.

Viongozi wengine waliowahi kutoa maoni yao kuhusu mpambano huu ambao sasa unaelekea kuwa wa Mengi na Rostam zaidi ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utawala Bora, Sophia Simba, aliyesema hatua ya Mengi kutaja hadharani majina ya wafanyabiashara watano, akiwamo Rostam Aziz, alikuwa “amechemsha.”

Mwingine alikuwa ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika, aliyesema kuwa Serikali inachunguza tuhuma dhidi ya Mengi kuwa anatumia vibaya vyombo vyake vya habari, hususan televisheni.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari wiki karibu mbili zilizopita, Mengi alitaja wafanyabiashara watano, akiwamo Rostam, aliodai ni mafisadi papa, wanaohusika katika karibu kila kashfa ya fedha nchini.

Katika orodha hiyo ya Mengi wamo pia Subash Patel, Tanil Somaiya, Yusuf Manji na Jeetu Patel, aliowatuhumu kwa kashfa za ufisadi katika ununuzi wa rada, ndege ya Rais, wizi wa mabilioni Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na ufujaji hususan katika mikopo kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Taifa wa Jamii (NSSF).

Wengine waliowahi kutoa maoni yao ni pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ambaye alimshutumu Mengi kwa kuwataja wafanyabiashara hao kuwa ni papa wa ufisadi akimtafasiri kuwa mbaguzi.

Wiki hii, akizungumza na kituo kimoja cha televisheni, Lipumba naye alirejea wito wa wengine wa kutaka Serikali kuonyesha uongozi kwa kuwa suala hilo sasa linakwenda nje ya mipaka.

Hayo yakiendelea, yamekuwapo maoni pia kwamba yanayoonekana sasa ni matokeo ya mtikisiko wa serikalini na katika chama tawala, Chama cha Mapinduzi (CCM), ambao unaakisi makovu ya kampeni za uchaguzi wa mwaka 2005, na kama ilivyo kawaida ya CCM, ni utangulizi wa mivutano na mizengwe ya uchaguzi wa mwakani.

“Hizi ni dalili za wazi kwamba hali si shwari ndani ya chama chetu. Sipendi kuzungumzia jambo hili lakini nakwambia kuna mambo mazito yanafukuta chini kwa chini na Mwenyekiti wetu (Rais Kikwete) asipokuwa makini CCM itampasukia mikononi mwake.

Mkapa alikwepa CCM isimpasukie, sasa Kikwete anakoelekea si kuzuri kabisa. Ni lazima achukue hatua za haraka kuondoa tofauti zilizopo,” alisema mstaafu mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina.

Mstaafu huyo ameliambia Raia Mwema kwamba kuna kila sababu sasa kwa Kikwete, “kufumba macho na kuchukua hatua za kisheria na kinidhamu dhidi ya wale wote wanaombebesha mizigo mizito”.

Alipotakiwa kufafanua kiongozi huyo mstaafu alisema: “…siwezi kukwambia zaidi, we subiri, si unaona hali ilivyo, watu wanaangalia madaraka kuliko hata maslahi ya CCM na wananchi wake. Wameanza kampeni tena chafu zaidi hata ya zile za mwaka 2005. Hii ni hatari sana na itatufikisha kubaya kama Taifa.”

Alisema tuhuma za ufisadi na mgawanyo wa mali za Muungano kuwa miongoni mwa mambo yanayochochea kuyumba kwa CCM na Serikali yake.

“Hebu fikiria tuhuma za ufisadi ni nyingi lakini wanaopelekwa mahakamani ni wale ambao wanatuhumiwa kuwa hawakuwaunga mkono watawala wa sasa katika uchaguzi wa mwaka 2005.

“Angalia orodha iliyoko mahakamani, na wengine nasikia wako njiani ama wanatishiwa kushitakiwa, si kwa sababu tu wana makosa, lakini kwa sababu pia hawakuunga mkono kundi lililoshinda huku watuhumiwa wengine wakiachwa wanatamba,” alisema.

Mwanasiasa huyo mstaafu pia alielezea kushitushwa kwake na kauli ya mawaziri wawili waandamizi kutoa kauli kutetea watu waliotajwa ama kutuhumiwa hadharani wakati mawaziri hao wamekuwa kimya wanasiasa wenzao akiwamo rais mstaafu Benjamin Mkapa walipotuhumiwa na kuanikwa hadharani.

“Sasa hawa mawaziri (Sophia Simba na George Mkuchika) wanamtetea nani? Mbona wakati Mkapa na wenzake wanatuhumiwa hadi aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa na mawaziri wawili wakajiuzulu, hakuna waziri aliyesimama kuwatetea? Serikali hii iko kwa maslahi ya nani? Kuna ambao wakiguswa Serikali na nchi inatetemeka na wengine ni mbuzi wa kafara?” alihoji mstaafu huyo.

Alisema anavyoona yeye ni mjadala wa tuhuma za ufisadi umepoteza mwelekeo hasa baada ya kugeuzwa kuwa vita ya watu binafsi isiyojali uzito wa hoja na tuhuma dhidi ya wahusika.

katikati ya haya yote, Raia Mwema imeambiwa kwamba kuna mjadala wa chini kwa chini wa urithi wa nafasi ya Rais Kikwete katika uchaguzi wa mwakani, mwaka mmoja sasa kabla ya muda wenyewe kufika na kinyume cha utamaduni wa CCM wa kumuachia kiongozi wao kumaliza vipindi viwili.


Mwaka 2000, Rais Mkapa akiwania kipindi cha pili huku Dk. Salmin Amour naye akiwa bado madarakani, mjadala kama huu ulizuka huku Dk. Salmin akidaiwa kutaka kubadili Katiba, madai ambayo yeye mwenyewe hakupata kuyasema na hatimaye ukaanza mchakato uliomuibua Rais wa sasa wa Zanzibar, Amani Karume.

Raia Mwema imefahamishwa kwamba wakati huo, walisimama watu ndani ya Kamati Kuu, kuhoji uhalali wa utamaduni huo wa kumwachia rais aliye madarakani kuwania vipindi viwili bila kupingwa kwa maelezo kwamba inapotokea kwa kiongozi huyo kutokidhi matakwa ya wana CCM na Watanzania, itakuwa na athari mbaya kwa CCM, lakini hoja hiyo “ilimalizwa kiutu uzima” na CCM.

Sasa hoja hiyo inadaiwa inaibuliwa upya kumtisha Kikwete anayedaiwa amewageuka wenzake waliomsaidia mwaka 2005 japo yeye mwenyewe ndiye aliyetangaza kuvunja kambi zote za wakati wa mchakato.
 
Mafisadi papa: Si ubaguzi ni masilahi ya taifa

Padri Privatus Karugendo Mei 6, 2009

Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

SIKUSUDII katika makala hii kumtetea Reginald Mengi, na wala siandiki kumlaumu na kumlaani.

Kama ningeamua kuandika kumtetea ningefanya hivyo kwa uhuru na si kwa kushawishiwa na msimamo wake; pia kama ningeamua kuandika kumlaumu na kumlaani ningefanya hivyo kwa uhuru wangu bila shinikizo wala kupokea bahasha.

Wiki hii nilikutana na mtu (jina nalitunza) aliyenishawishi nichukue upande katika swala hili ili niupige kisogo umasikini; hanifahamu vizuri – fedha za kununua uhuru wangu hakuna tajiri wa kuzipata!

Hakuna utajiri mkubwa kama wa mtu kuwa huru. Hivyo ninaandika makala hii kutetea masilahi ya Taifa. Naandika kuwakumbusha Watanzania wenzangu ule msemo wa “Wajinga ndio waliwao”.

Ingawa sifahamu kwa hakika malengo na nia ya Mengi kutangaza mafisadi papa, ninaelewa vizuri hasira aliyo nayo. Hasira hii iko mioyoni mwa Watanzania wengi.

Bahati nzuri au mbaya Mengi, ana vyombo vya habari; anaweza kuvitumia vizuri au vibaya. Lakini kuna Watanzania wasiokuwa na jukwaa la kutoa hasira zao; siku wakisema imetosha, patakuwa padogo!

Hata hivyo, alichokifanya Mengi hakikuwa kipya. Labda ni kwa vile Watanzania tuna ugonjwa wa kusahau au tunaendeleza ule ugonjwa wa “Wajinga ndio waliwao”. Majina matano aliyoyatangaza yamekuwa kwenye vyombo vya habari kwa muda mrefu; yametajwa kwenye Richmond, EPA, Ununuzi wa Ndege ya Rais na mengine mengi ya kuhujumu na kupora rasilimali za Taifa.

Alichokifanya Mengi ni kuchambua kwenye vyombo vya habari na kutangaza. Kama kuna mtu anayetaka kumshitaki, asianzie kwake – aende mbali kwanza kuvifikisha mbele ya sheria vyombo vyote vya habari vilivyotangaza majina hayo.

Sipendi kumtetea Mengi, lakini ninashawishika kuamini kwamba nia na lengo lake ni jema. Binafsi simfahamu kwa karibu. Jitihada zangu za kutaka kumfahamu kwa karibu ziligonga Mwamba. Mwaka 2002, nilipojitokeza kuunga mkono matumizi ya kondomu kwenye Mkutano wa Ukimwi kitaifa kule Arusha; nilishawishika kumtafuta Mengi, ili tuungane na kuwa na sauti mmoja, yeye pia wakati huo alikuwa akigombana na maaskofu kuhusu swala la kondomu.

Nilifunga safari kutoka Karagwe kwenda Dar es Salaam. Ile picha niliyokuwa nikiona kwenye vyombo vya habari kwamba yeye ni mtu wa watu ilinifanya niamini kwamba isingekuwa vigumu kukutana naye.

Ofisini kwake, wasaidizi walinishauri niandike barua ya kujieleza na kuomba kukutana naye. Niliandika barua na kuwapatia wasaidizi wake. Nilishauriwa nirudi Karagwe, ili
Yeye, Mengi, akipata nafasi aniite. Mwaka mzima wa 2003 ulikatika.

Mwaka 2004 nilikwenda ofisini kwake tena, wasaidizi wakaniambia barua yangu ilifika, nisubiri kuitwa. Mwaka mzima wa 2004 nao ulikatika. Nilifunga tena safari mwaka 2005 kutoka Karagwe, hadi ofisini kwa Mzee Mengi,lakini sikufanikiwa kuonana naye. Nilikikata tamaa; hivyo hadi leo hii sijafanikiwa kukutana naye. Hivyo simfahamu kwa karibu!

Nakumbuka siku ya mwisho nilipokata tamaa nilikutana na mlemavu aliyeniambia siku hiyo kwake ilikuwa ni mara ya 99 akijaribu kukutana na Mengi, bila ya mafanikio! Wasaidizi wa Mengi, kama nilivyojaribu kuwasoma, wanafikiri kila mtu anayekwenda pale, anataka msaada; hivyo wanamkwepesha bosi wao asikutane na waomba misaada. Nafikiri hata mimi niliwekwa kwenye kapu la kuomba msaada!

Sikutaka kabisa kujiingiza kwenye swala hili la mafisadi papa na sasa fisadi nyangumi. Taifa limekumbwa na siasa za makundi. Jambo likitokea, linaangaliwa kimakundi. Ninajua hata sasa hivi kuna wanaofuatilia kwa makini kuona ni nani anaandika nini, ni nani anamuunga mkono Mengi, au ni nani anampinga.

Hata vyombo vya habari vimegawanyika kimakundi. Ukisoma magazeti unaweza kuona wazi ni gazeti gani liko upande upi. Maadili na utaalam wa uandishi wa habari umewekwa kando; hata waandishi wanaoaminika wameanza kuyaangalia matumbo yao na familia zao, na kusahau kabisa kazi ya kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha.

Nimeamua kuandika baada ya kuona baadhi ya Watanzania (hata na wale ninaowaheshimu) wanataka kupotosha swala zima la mafisadi papa. Wanataka kuingiza ubaguzi.

Wanafikiri kuwataja wahindi ni kuwabagua. Hili si kweli! Na kama nilivyosema hapo juu ni kwamba hasira ya Mengi, ni ya Watanzania wengi; ikitokea wakasema inatosha – ni kweli hapatatosha! Si kweli kwamba hoja ya ubaguzi ikitumika basi watetezi wa haki za binadamu watafunga midomo juu ya swala hili la mafisadi papa. Wamepotea njia! Tutasema!

Maoni yangu binafsi ni kwamba mtu anayehujumu uchumi, mtu anayepora rasilimali za Taifa, awe mweusi, awe mzungu, mhindi, mwekundu, mweupe, kijani au rangi yoyote ile ni adui wa umma! Ni lazima umma umchukie, ni lazima umma umtenge na ikibidi upambane naye! Tusitumie hoja ya rangi kuendeleza mshikamano wa kihalifu.

Kwa upande mwingine mimi siwalaumu hawa wahindi; ni wajanja, wanajua jinsi ya kuishi kiujanja ujanja ili kuendeleza kizazi chao na kulinda mshikamano wao. Ni wajanja sana katika biashara; wanakuhitaji na kukupenda wakijua una faida kwao; wakisha kukutumia wanasahau sura yako na jina lako.

Wameishi zaidi ya miaka 100 hapa lakini hadi leo ni jamii iliyoshikamana, hawakujichanganya na weusi kama walivyofanya waarabu na baadhi ya wazungu. Wametunza lugha yao, wametunza mila zao, wametunza dini yao na wala hawakutaka kuieneza miongoni mwetu kama walivyofanya wazungu na waarabu; wanatawanya ndugu na jamaa kwenye nchi mbali mbali duniani, ili kesho na keshokutwa yakitokea matatizo eneo moja wapate pa kukimbilia.

Hata wale tulioamini ni Watanzania wazalendo, waliolitumikia Taifa hili kwa uaminifu mkubwa wamezikwa nje ya nchi. Hivyo hawa watu wanaishi kwa malengo na kwa mshikamano.

Tujilaumu sisi wenyewe; tumebaki kuwa wajinga ndio waliwao. Tumeshindwa kuwa wapole kama njiwa na wajanja kama nyoka. Kwa vile wahindi ni wajanja, tulipaswa kuwa wajanja vilevile. Tunawaruhusu kufanya biashara, lakini tuwabane kwenye ushuru na masharti mengine ya kuchangia shughuli za maendeleo. Sisi tuna wasomi wengi katika serikali yetu; kusema kweli walio wengi wamesoma sana kuwazidi hawa wahindi wanaoliyumbisha taifa.

Inakuwa vipi, wasomi wetu wanayumbishwa na wajanja, inakuwa vipi wasomi wetu ambao ndio wenye mali, wanawapigia magoti wageni? Inakuwa vipi tenda zote wanazipata wahindi? Inakuwa vipi wahindi ndio wanasamehewa kodi? Inakuwa vipi wahindi ndio wanaendesha uchumi wa taifa? Inakuwa vipi tunasimama na kuwatetea? Kwa vile wanatoa misaada mikubwa kwenye vyama vyetu vya siasa? Kwa vile wanatoa misaada kwenye timu za mpira? Hizo fedha wanazitoa wapi? Huo utajiri wameutoa wapi kama si hapa hapa kwetu? Si kwamba wanatoa msaada,
bali wanarudisha walichokipora!

Wanaoendesha magari mazuri na ya kisasa ni wahindi, wanaoendesha biashara kubwa ni wahindi, wanaougua na kwenda kutibiwa nje ya nchi ni wahindi, wanaosafiri kwa wingi nje ya nchi ni wahindi. Ukienda uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, unashangaa jinsi ndugu zetu wanavyotoka na kuingia. Watanzania weusi wanaozea Ubungo, Tabata na Kigogo.

Kama wanafanya biashara halali, hakuna neno, maana sisi tumesinzia. Ila kama wanahujumu, kama wako kwenye ufisadi wa EPA,RICHMOND na kashifa nyingine zilizoibuka katika uongozi wa awamu ya nne, ni lazima tusimame na kusema. Na hili lisitafsiriwe kama ubaguzi; ni kutetea masilahi ya Taifa.

Kama ni ubaguzi kwanini asibaguliwe Profesa Issa Shivji? Au kwanini wasibaguliwe makamaradi wengine wa kihindi tunaowafahamu vizuri katika taifa letu? Mbona kuna wazungu Watanzania na wazalendo, hawabaguliwi? Suala si rangi, suala ni uzalendo; suala ni unalifanyia nini taifa la Tanzania. Tusitumie hoja ya rangi kuvuruga jitihada za kupambana na ufisadi.

Tunaweza kuiga mifano ya nchi nyingine. Nigeria, hawakugombana na wahindi wala hawakuwafukuza kama alivyofanya Idi Amin wa Uganda. Wao walikuwa wapole kama njiwa na wajanja kama nyoka. Walifanya uamuzi wa kuyasusia maduka na biashara zote za wahindi; kwa vile wahindi wana mtandao mkali katika nchi mbali mbali na kwa vile hawakuwa Nigeria kama wazalendo waliamua kutimuka kutoka Nigeria, na kuhamia nchi nyingine.

Tunaweza kufanya hivyo kwa wale wanaoendesha biashara na kukwepa kodi, lakini kwa mapapa, ni lazima wabanwe, warudishe fedha na rasilimali walizoficha nje ya nchi. Ni lazima wabanwe ili wawataje wale wanaoshirikiana nao ndani ya serikali.

Hatuwezi kuendelea kuimba wimbo wa ufisadi wakati tunawalea mafisadi; hatuwezi kupambana na ufisadi wakati tunawatetea mafisadi na kuwakingia kifua.

Wale wanaompinga Mengi na kuwatetea mapapa, ninawaomba wasimame na kuwaelezea Watanzania undani wa familia za hawa ndugu zetu wahindi: Je, familia zao ziko wapi? Wajomba, shangazi, watoto na ndugu zao wengine wako wapi? Mtu anayefanya biashara hapa wakati familia yake iko Marekani hawezi kufanya biashara kwa moyo wa kizalendo. Mtu anayefanya biashara hapa wakati watoto wake wanaishi India, hawezi kufanya biashara kwa moyo wa kizalendo.

Rafiki yangu msukuma, anayefanya biashara ya samaki, alinielezea alivyoshangaa alipokwenda India kumtembelea rafiki yake aliye na kiwanda cha kusindika samaki pale Mwanza. Anasema, mhindi huyu akiwa Mwanza, anajifanya ana maisha ya chini na kuishi kwenye nyumba ya msajili; lakini kule India amejenga jumba la kifahari na ndugu zake kule India wanaishi kwenye ufahari wa hali ya juu.

Rafiki yangu mwingine Mhindi wa Bukoba, tulishibana kweli kweli, maana nilikuwa nikimuuzia dola, wakati huo tunaziuza kama bangi; nilikuwa nikikaribishwa hadi nyumbani na kula chakula; nilifahamiana na ndugu zake wote na kila wakati alinielezea mipango yake yote.

Nilipoishiwa zile dola na maisha yakabadilika, alisahau sura yangu na jina langu! Hata nikikutana naye leo hii, kwa vile sina zile dola tena na sina faida yoyote kwake, mimi ni mtu ambaye sikuwahi kuishi!

Siandiki haya kupandikiza chuki, na wala mimi si mbaguzi! Lengo langu ni kutaka kuwaamsha Watanzania wenzangu kutoka kwenye ndoto za “wajinga ndio waliwao”.

Ni lazima tuwe wapole kama njiwa na wajanja kama nyoka. Ni lazima na sisi tuishi kwa malengo, ni lazima na sisi tuishi kwa mshikamano; si mshikamano wa kihalifu bali mshikamano wa kujenga Taifa letu.

Nampongeza Mengi kwa ujasiri wa kusema; na nawapongeza wengine wote wanaopambana na ufisadi kwa malengo ya kizalendo; wale wanaopambana na ufisadi bila kulenga kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu wa 2010, wale wanaopambana na ufisadi bila kulenga kuwania urais wa 2010; wale wanaopambana na ufisadi bila kuwa na nia na lengo la kuwania tenda ama kuvuruga biashara ya watu wengine.

Nawaunga mkono wale wote wanaopambana na ufisadi kwa moyo wa kizalendo. Tanzania ni yetu sote na ni lazima tuilinde kwa gharama yoyote ile!
 
Ndugu tabia ya kukopi kwenye magazeti inakera? ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Pole kwa kukerekwa maana wengi tunafurahia taarifa hizo, take care this about others! Acha Ubinafsi :rolleyes:
Wadau tupeni michapo sio rahisi wengine kupata magazeti hayo! Wewe upo kiwandani kabisa na yanapotengezwa tulio SHITINDI tutafanyaje?
 
Ndugu tabia ya kukopi kwenye magazeti inakera? ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

HUJALAZIMISHWA KUSOMA NDUGU!ukijisikia kutapika tapika 'CLICK NEW POST' hama jukwaa kabisa.nenda kwenye jukwaa lenu la MAMBO YA KIKUBWA.hapa tunataka watu wenye HOJA.

bravo bubu!
 
Kuna watu hawajui kwamba Jamiiforums ni International au??? Endelea ku copy and paste watu tunaofuatilia mambo ya nyumbani tusome.
 
- Wananchi tusitishwe na maneno ya kuharibika wka amani, kinachoendelea sasa hivi ndio demokrasia yenyewe hasa na haiwezi ku-get better than this yaani Mengi Vs Rostam, serikali iake pembeni kama anavyofanya Kikwete sasa hivi,

- In the process ya hii malumbano kuna uchumi pia, mawakili wanalipwa na pande mbili, media inauza, wananchi wanaelimika na siasa ya first hand, wasioyaweza haya wakae pembeni, ubepari tuliutaka wenyewe, sasa haya ndio matokeo yake.

Wacha malumbano yaendelee, ni afya kwa taifa letu rais na serikali wakae pembeni kwanza, time yao on this ishu itakuja lakini sio sasa!

Respect.

FMES!
 
Hawa wote ni makada wa CCM na wamenufaika sana na ukada wao. Sitashangaa kama hawataitwa pembeni na kuambiwa waache mchezo wa kitoto. Sitashangaa kusikia kuwa Mengi na Rostam wakitoa joint statement wakisema haya yote yalichochewa na mkono wa tatu. Mengi atafuta kesi na Rostam ataondoa vielelezo vyake au Takukuru watasema tu hakuna ushahidi! Mwaka 2010 wote kwa pamoja watazunguka nchi nzima kumnadi mgombea wa chama chao! Na nyie mliotegemea makubwa mtabaki kugunia chini chini!

Amandla.......
 
Uchambuzi makini...

wananchi tungependa kuwafahamu zaidi decision makers wanaochochea rushwaa....

ni kweli jeetu, tanil, subash wako tayari kutoa rushwa biashara zao zisongeee..hiyo ndo rule of the business (cost minimization vs profit maximazation)....
 
Back
Top Bottom