Mengi na Uanachama wake CCM

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
May 24, 2008
10,943
428
Makamba amuomba Mengi msamaha kuhusu uanachama wake

kuna habari nimezipata hivi punde makamba amuomba mengi msamaha kuhusu tuhuma alizopata za uanachama wake na amesema mzee mengi ni mwanachama hai wa CCM tokea mwaka 77
 
kuna habari nimezipata hivi punde makamba amuomba mengi msamaha kuhusu tuhuma alizopata za uanachama wake na amesema mzee mengi ni mwanachama hai wa CCM tokea mwaka 77
amemuomba radhi kama mkosaji?
ai miini makamba ni mkosaji?
 
do i really care kuhusu uanachama wa mtu na muda wake? I do care abt hicho chama kimefanya nini na kinafanya nini sasa. Just another waste of time wa huyo makamba-just another biggest looser.
 
viongozi wasio na busara hugeuza midomo yao majalala,,,sasa tutaona sophia mwana wa simba atasema nini kama makamba mwana wa yusuph kaanza kuuma uma maneno...mambo ya kukurupuka bila data bwana kweli matatizo, iki backfire unaanza kujinyeanyea.
 
do i really care kuhusu uanachama wa mtu na muda wake? I do care abt hicho chama kimefanya nini na kinafanya nini sasa. Just another waste of time wa huyo makamba-just another biggest looser.

Kuna vilaza wengi tz lkn yule maza kiboko....yan huwa namsahau kila nnapoambiwa kutaja majina ya mawaziri...cjui mkuu analifikiriaje hili manake sio first time anafuka.....
 
Yaani hichi chama kimekuwa kama kijiwe cha wavuta bangi vile
 
Duh huyu mzee leo nimesoma anasema amebakiza miaka 4 afe kwa hiyo mwacheni amaliza miaka hiyo.
 
Makamba adai ana miaka mnne ya kuishi ambao afe kwa amani, azikwe kwa heshima
broken-heart.jpg
Na Joyce Mmasi

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amewaomba watu wanaomfuatafuata kumuacha ili afe kwa heshima kutokana na kubakiza miaka michache ya kuishi duniani.
Makamba alitoa kauli hiyo juzi alipozungumza kwenye mahafali ya wanafunzi wa Shule za St Anne Marie eneo la Mbezi kwa Msuguli jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Aliwataka watu wasiomtakia mema kuacha kumfuatafuata na badala yake waachwe afe kwa heshima kwa kuwa amebakia miaka minne afikishe umri wa kuishi duniani.

Akinukuu vifungu kwenye Biblia , Makamba alisema umri mtu kuishi duniani ni miaka 70 na wachache ni 74 na akasema yeye amefikisha umri wa miaka 71, hivyo anapaswa aachwe amalizie miaka mine iliyosalia ili azikwe kwa heshima.

“Mimi nina miaka 71 sasa, nimebakiza miaka mine tu nife, lakini kuna watu wananifuata ooh Makamba kafanya hivi, wanataka kuniharibia bure, kwanini wasiniache nife nizikwe kwa heshima” alisema Makamba na kuwaacha watu wakiangua kichezo.

Akizungumzia utendaji kazi kwa walimu nchini, Makamba aliwataka kuongeza upendo kwa watoto wanaowafundisha ili kuweka kichocheo kwa wanafunzi wapende kusoma na kuwa na bidii katika masomo.

Makamba alisema, walimu ni watu muhimu wanaoweza kudumaza au kupandisha kiwango cha kufaulu kwa wanafunzi na kwamba penye upendo pana elimu, na mwalimu mzuri ni yule anayeonyesha upendo kwa wanafunzi na kwa masomo anayofundisha.

Katibu Mkuu aliwakumbusha walimu nchini kwamba wanafunzi wengi ni vijana na ni taifa la kesho na akasema kwa kuwalea katika maadili ya kupenda kusoma ni kusaidia kujenga taifa imara lenye wasomi wengi na wazuri.

Alilaumu tabia ya baadhi ya walimu wanaogoma kufundisha akisema mwalimu anapogoma kufundisha asifikiri anamgomea mwajiri wake au serikali na badala yake wajue kuwa wanawagomea watoto hao.

Awali akizungumza wakati akimkaribisha, Mkuu wa shule hizo Nelson Theonest alisema wanafunzi wote waliomaliza shule waliandaliwa vizuri na wote wapo tayari kujiunga na shule zingine kila mmoja kwa kiwango chake na akawapongeza wanafunzi wote kwa adabu na utii walioonyesha shuleni hapo kwa muda wote waliokuwa wakisoma. Katika mahafali hayo, jumla ya wanafunzi 359 wadarasa la saba, kidato cha nne na cha sita, walimaliza shule na kukabidhiwa vyeti vyao.
 
Kama kweli Makamba kaomba msamaha kama katibu mkuu wa chama kwa niaba ya chama na ili kufuta kauli za dharau zilizotolewa na mwenyekiti wa chama Dar, atakuwa amefanya the classy thing.

Yaani yule mwenyekiti wa CCM Dar alionyesha tacky behavior iliyokuwa riddled with infighting.
 
kuna habari nimezipata hivi punde makamba amuomba mengi msamaha kuhusu tuhuma alizopata za uanachama wake na amesema mzee mengi ni mwanachama hai wa CCM tokea mwaka 77

Janja ya Nyani hiyoooo...
Si tumeambiwa juzi juzi Makamba amechukua mchango shs 100m kutoka kwa Mengi; akichangia chaguzi za vitongoji? Kwamba Makamba kama hakuziwasilisha/declare kwenye chama chao basi aseme ameziweka wapi, na kwa nini alichukua maela ya mchango kutoka kwa mtu ambaye si wamanchama wao?
Kama alilamba kiasi, hana njia nyingine ni kuomba radhi!!! Amejisetiri.
Huu ndio ukweli nyuma ya pazia.
 
Na Mwandishi Wetu

KATIBU wa CCM mkoani Dar es salaam, Kilumbe Ng'enda amekanusha taarifa kuwa alipingana na ufafanuzi uliotolewa na mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi dhidi ya madai kuwa mfanyabiashara huyo maarufu si mwanachama wa chama hicho tawala.

Ijumaa iliyopita, Mengi aliitisha mkutano na waandishi wa habari kupinga taarifa iliyotolewa na Kilumbe kuwa matawi ya CCM mkoani Dar es Salaam hayamtambui Mengi kama mwanachama wa chama hicho na kuonyesha vielelezo vinavyoonyesha kuwa alijiunga na CCM tangu Aprili mwaka 1977.

Jumapili, gazeti la Mwananchi Jumapili lilimkariri Kilumbe akimpinga Mengi kwa kusema kuwa kama ni mwanachama wa CCM, basi hana budi kwenda ofisini kwake (Kilumbe) kuthibitisha uanachama wake kwa kuwa hayumo kwenye orodha ya wanachama wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Mwananchi Jumapili ilichapisha habari hiyo ikimkariri Kilumbe akizungumza kwenye kipindi cha moja kwa moja cha kituo cha televisheni cha Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) cha Jungu Kuu.

Lakini jana, Kilumbe alitoa taarifa akisema: "Baada ya Ndugu Mengi kuthibitisha uanachama wake kwa kuonyesha kadi ya mwaka 1977 iliyotolewa na tawi la Kisutu Dar es Salaam na baada ya tawi la Mkunguni kuthibitisha uanachama wake wa Ndugu Mengi na kwa kuzingatia kwamba jukumu la kumpa mtu uanachama ni la kamati ya siasa ya tawi, ofisi ya CCM Mkoa inaridhika kwamba tawi la Kisutu limetimiza wajibu wake katika kumpa uanachama Ndugu Mengi. Kwa hiyo mkoa wetu hauna sababu ya kutotambua uanachama wake."

Taarifa hiyo inaendelea kusema: "Kwa kuzingatia kwamba ni nadra sana kwa wafanyabiashara wakubwa wa aina ya Ndugu Mengi kukiri hadharani uanachama wao katika vyama vya siasa, Ndugu Mengi ameonyesha mfano mzuri na mapenzi makubwa kwa Chama Cha Mapinduzi, kwa hiyo anastahili pongezi za chama chetu.

"Ni matumaini yetu basi kwamba Ndugu Mengi ataendelea kushirikiana na tawi lake anakoishi sasa kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi kwa kuendelea kutoa michango ya hali na mali kama anavyofanya sasa."


Source: Mwananchi
 
Hiyo ndio Tanzania yetu, where leaders on the frontline, dare to talk boldly only to think later on!Siyo Kilumbe tu, tukiomba wanajamvi walete quotes za viongozi kuropoka then next day baada ya kufikiri wanasahihisha utashangaa. Kama unakumbuka any of those confusing statements rusha hapa. Tunaanza na Kilumbe, who is next? Kazi kwenu wanajamvi
2.
3.
4.
5.
6.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom