Mengi na Makamanda wa Ufisadi kutua Nzega J'mos Hii

M-bongo

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
338
71
Makamanda wa Ufisadi, (Wabunge wa CCM) na Bw Regnald Mengi wanatarajiwa kutua Nzega Jumamosi ya wiki hii na kupokewa kwa maandamano na shamra shamra kubwa zitakazoambatana na burudani kede kede

Aidha msafara huo unatarajiwa kuwa na makamanda wa Ufisadi ambao ni Dr Mwakyembe, Sendeka, Kimaro, Kilango, Aziza Ally, Lembeli, Nkumba, Selelii (Mwenyeji wa ugeni) na wengine ambao sijapata taarifa zao.

Chanzo cha habari kinasema kuwa maandalizi yote yameshakamilika ikiwa ni pamoja na utaratibu wa kukabidhi Hundi ya zaidi ya M150 kwa vikundi vya ujasiria mali 80 ambavyo kila mwana kikundi atajinyakulia kiasi cha Tshs 60,000/= ili kujikwamua na umaskini.

I wiil B there!

Welcome Mengi, welcome makamanda wa ufisadi Nzega!
 
Move nzuri sana hasa kwa wanasiasa wa kambi ya wapiganaji.NEC kwa kushirikana na mafisadi hawataki kuona hii kitu ikifanyika.

Lakini msaada wa tsh 60,000/= kwa mwanakikundi nadhani ni ndogo sana kumkwamua mtu katika umaskini !.Tafadhali Mzee Mengi ongeza walau ifike tsh 500,000/= kwa kila mwanakikundi.

Angalizo kuweni makini Mzee Makamba anaweza kuzuia msipate mapokezi kama alivyofanya kwa Mzee Six.
 
Karibu Mzee Mengi Nzega angalau umpe nguvu kidogo Selelii maana kabanwa kweli kweli na kijana, kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, asilimia 90 ya wagombea wanaojulikana wapo kundi la Selelii wamebwagwa na wagombea wote ambao wapo kundi la kijana( ? ) kitu ambacho si dalili nzuri kwa Mh Selelii hii inathibitishwa na mkutano wa hadhara aliotaka kuufanya Selelii kata ya NATA na kuambulia watu wasiozidi kumi tu. kwa ugeni wa Bwana Mengi nadhani angalau kidogo selelii atapata nguvu. karibu sana nipo Nzega mbele ya Gest mpya ya Seleli nikitengeneza baiskeli( Fundi)
 
Unamzungumzia yule kijana wa kisomali !,Zyansiku hacha ushabiki maandazi.Hivi Tanzania tuna uhaba wa viongozi mpaka tuwape uongozi wasomali walioshindwa hata kujitawala.Hapana nakataa imefika mahali watanzaia kuwaambia wageni wafanye kila kitu lakini siasa watuachie wazawa.

Wiki ijayo nitakuwa Morogoro mji kasora bahari kutoa somo la uraia ili waachane na kasumba ya kutulea wahindi wachovu pale mjengoni.Nikitoka huko nitapitia Tabora kuendeleza elimu ya uraia kwa wapiga kura wasimchague yule miran Rostam Azziz.
 
Pole kabonde! No matter mhindi au mwarabu the issue is content! ubaguzi huo unaotaka kuuhubiri hautatufikisha popote, hii inaanza kuthaminisha kuwa hata Zito kuenguliwa Chadema ni sababu ya ukabila wakati inawezekana si sababu ya msingi lakini unapoanza kusema msomali, mwarabu nk sijui unataka kutupeleka wapi anyway sisi vijana wa Nzega kwa swala la huyo unayemwita msomali hatulali mpaka kieleweke selelii analijua hilo hata joto la Nzega analijua vizuri Selelii hapo umekosea kidogo
 
Makamanda wa Ufisadi, (Wabunge wa CCM) na Bw Regnald Mengi wanatarajiwa kutua Nzega Jumamosi ya wiki hii na kupokewa kwa maandamano na shamra shamra kubwa zitakazoambatana na burudani kede kede

Aidha msafara huo unatarajiwa kuwa na makamanda wa Ufisadi ambao ni Dr Mwakyembe, Sendeka, Kimaro, Kilango, Aziza Ally, Lembeli, Nkumba, Selelii (Mwenyeji wa ugeni) na wengine ambao sijapata taarifa zao.

Chanzo cha habari kinasema kuwa maandalizi yote yameshakamilika ikiwa ni pamoja na utaratibu wa kukabidhi Hundi ya zaidi ya M150 kwa vikundi vya ujasiria mali 80 ambavyo kila mwana kikundi atajinyakulia kiasi cha Tshs 60,000/= ili kujikwamua na umaskini.

I wiil B there!

Welcome Mengi, welcome makamanda wa ufisadi Nzega!

Sh 60,000 ni za ujasiriamali au mboga ya mchana? Kidding huh?
 
Sh 60,000 ni za ujasiriamali au mboga ya mchana? Kidding huh?

Hahahahah,

Anyway akipewa mmoja mmoja atokomee nayo itakuwa ya mboga. Ila kama wanapewa kwenye kikundi wakaifanyia kazi kwa pamoja watafika mbali....
Tatizo jingine mara nyingi unakuta si mtaji, ila kuna vitu kama opportunities/ideas za jinsi ya kuitumia hiyo pesa kupata tija endelevu au elimu vinakosekana.

All in all, something is better than nothing....
 
Chama kipya nakisubiri kwa hamu sana .Binafsi sipendi kuwaona wakiendelea kunyanyaswa ndani ya ccm.Hii ndio naomba itokee hasa,maana hawa mabwana wanajua kila kitu jinsi nchi inavyoliwa ndio maana kwa kiasi fulani wanaonyesha uchungu japo unazimwa kwa nguvu ya mafisadi.....
nashauri waunde chama chao wajitoe CCM
 
nashauri waunde chama chao wajitoe CCM

Kuunda chama kingine si tatizo, tatizo ni kuhakikisha hawa fisadiz wanatoweka katika jamii. Wanapaswa kuwa jela na si vinginevyo.......hawa wapiganaji wana-fight kwanza kuhakikisha wanatoka katika chama chao na kisha kuwapeleka mbele ya sheria.
 
Karibu Mzee Mengi Nzega angalau umpe nguvu kidogo Selelii maana kabanwa kweli kweli na kijana, kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, asilimia 90 ya wagombea wanaojulikana wapo kundi la Selelii wamebwagwa na wagombea wote ambao wapo kundi la kijana( ? ) kitu ambacho si dalili nzuri kwa Mh Selelii hii inathibitishwa na mkutano wa hadhara aliotaka kuufanya Selelii kata ya NATA na kuambulia watu wasiozidi kumi tu. kwa ugeni wa Bwana Mengi nadhani angalau kidogo selelii atapata nguvu. karibu sana nipo Nzega mbele ya Gest mpya ya Seleli nikitengeneza baiskeli( Fundi)
Kweli kimbunga cha JF kinakwenda kwa kasi ya ajabu! Mafundi Baiskeli Nzega kama nao wanaingia humu naamini 2010 ujumbe (hoja za JF) utakuwa umesambaa nchi nzima.
Zyansiku, kamanda hakikisha kila anayekuja kutengeneza baiskeli asitoke hivihivi, mpe salama za JF ili BAISKELI YAKE NA UBONGO WAKE VYOTE VIPATE MAINTENANCE
 
Makamanda wa Ufisadi,
Jina Lina someka na kutamkika very good and promising. Lina chehe ya nuru ndani yake... kwa kweli linapendeza...!

Ni vipi kujenga morali ya dhati kwa jamii ya tu ...?
 
..hizo hela wanatoa wapi?

..binafsi mapesa yanapoanza kumwagwa karibu na uchaguzi nakuwa na wasiwasi sana.

..kwanini hawakutoa pesa hizo mwaka 2006, wanatoa leo wakati uchaguzi unakaribia?
 
On their way back can they Stop at Igunga wafanye kama waliyofanya huko Nzega!
 
Back
Top Bottom