Mengi: Manji anatoa wapi kiburi na ujasiri?

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,483
159
Wakuu habari za leo,

Jana Baada ya kutolewa kwa shauri kati ya madai ya Manji kukashifiwa na ITV katika moja ya taarifa zake za habari, ila ITV wameshinda kwa kutokuonekana na hatia yoyote kutokana na shauri hilo.

Baada ya Kutoka ndani ,Mzee mengi akihojiwa na waandishi wa habari, aliuliza watanzania, ''Hiki Kiburi na ujasiri alionao Manji nani anampa? Mzee mengi alisema “anatoa wapi nguvu hizi?” Hii ni baada ya Manji kukosekana pale katika siku ya kutoa maamuzi. Hii mzee Mengi aliona kama ni dharau kubwa kwake. Manji aliwakilishwa na wakili wake.

Najua mna mambo mengi ila naomba tujibu swali la Mzee Mengi, Je Manji anatoa wapi kiburi cha na namna hii na ujasiri mkubwa kiasi hiki?? Nani anampa? Nani yuko juu yake?
 
Nafikiri ni vizuri tukimjua huyu Manji in details! Most of the things i hear about him are like town gossips lakini sina uhakika yeye ni nani haswaaa....
please...
 
You dont have to look far to knw manji..angalieni board of directors ya NSSF..Link it to the present cabinet...mtamjua manji anatoa wapi kiburi!
 
huyo ni kati ya wale wanaotoa maamuzi ktk nchi hii.yeye yupo juu ya sheria na katiba ya nchi hata jk anampigia magoti huyu bwana mkubwa.
 
huyo ni kati ya wale wanaotoa maamuzi ktk nchi hii.yeye yupo juu ya sheria na katiba ya nchi hata jk anampigia magoti huyu bwana mkubwa.
Manji Bwana Mkubwa au Bwana Mdogo??au ukishakuwa na pesa unakuwa bwana Mkubwa?
 
Huyo ndiye mwakilishi wa Aghakhan hapa nchini...yeye ndio anawakilisha ile jumuiya ya Aghakhani na kulinda maslahi yao..mnajua hilo??
 
Nafikiri ni vizuri tukimjua huyu Manji in details! Most of the things i hear about him are like town gossips lakini sina uhakika yeye ni nani haswaaa....
please...

Luteni Makamba ammiminia mabusu mfadhili wa miradi
2005-07-21 14:57:21
Na Maabad Msuya, Temeke

Baada ya kushindwa kujizuia kuonyesha furaha yake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Luteni Yusuph Makamba, amejikuta akimfagilia mfadhili wa miradi mbalimbali wilayani Temeke Bwana Yusuph Manji na kumtaka agombee ubunge wa jimbo la Kigamboni kwa tiketi ya CCM.

Kama vile haitoshi Mkuu huyo wa Mkoa kwa kuonyesha ni jinsi gani alivyovutiwa na kufurahishwa na ufadhili huo, aliamua kumpa mabusu Bw. Manji kama ishara ya shukrani na furaha.

Luteni Makamba ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo, baada ya kuvutiwa na mwamko wa wakazi wa eneo hilo, naye ameahidi kuchangia Sh. milioni 1.5, kati ya hizo, milioni moja ikitoka mfukoni mwake na laki tano kwenye mfuko wa ofisi yake.

'Kusema kweli umenifurahisha sana na ili kukuonyesha ni jinsi gani umenifurahisha nakuomba usogee tena hapa karibu yangu ili nikupe busu la furaha,' akasema Mkuu huyo wa Mkoa na kisha akaanza kumimina mabusu mfululizo.

Source: Alasiri
 
Kawaida..tu!!...Nafikiri Ni Muoga tu...Ndio maana Hakuja..
Mzee Mengi endelea na kazi zako!!....Achana naye...
 
Kawaida..tu!!...Nafikiri Ni Muoga tu...Ndio maana Hakuja..
Mzee Mengi endelea na kazi zako!!....Achana naye...

ila bado tunajiuliza nani anayempa kiburi Manji,Je ni huyu aliyempiga Mabusu tu au kuna Mwingine juu ya mengi.

Na hii tabia ya Mzee Mengi kulia lia kama mtoto ameitoa wapi,kama anaona anaonewa kwanini asiwataje hao ambao wanampa kiburi Huyu kijana kuliko kutoa Speculation tu ?
 
Huyu kaiweka siri kali yote mfukoni mwake kwa jinsi anavyowamwagia michuzi, na anajua hawezi kufanywa lolote ndio maana anakuwa na kiburi cha hali ya juu.

Nashangaa mahakama haikumwamuru alipe gharama zote za kesi alizoingia Mengi. Si ajabu alishamwaga ngawira hata huko pia.
 
Mimi sio mbaguzi wa rangi lakini naanza kuoji kiburi cha hawa magabachori wetu hapa, inawezekana Mchungaji Mtikira alikuwa sahihi wakati furani maana sasa watatu wako juu ambao ni RA, Manji na BV sielewi kwanini wanatuzidi ujanja na kutuibia namna hii.
 
Huyo ndiye mwakilishi wa Aghakhan hapa nchini...yeye ndio anawakilisha ile jumuiya ya Aghakhani na kulinda maslahi yao..mnajua hilo??
nani alimchagua??kuna mtu anajua utaratibu wa jinsi hawa wanavyochaguliwa??
 
Huyu kaiweka siri kali yote mfukoni mwake kwa jinsi anavyowamwagia michuzi, na anajua hawezi kufanywa lolote ndio maana anakuwa na kiburi cha hali ya juu.

Nashangaa mahakama haikumwamuru alipe gharama zote za kesi alizoingia Mengi. Si ajabu alishamwaga ngawira hata huko pia.

Yusufu Manji ni CEO wa QUALITY GROUP (ilisajiriwa baada ya Quality Garage kufilisiwa na hii ilisajiliwa baada ya K. J. motors kufilisika) kampuni ambayo kati ya biashara zake nyingi za ujanja ni agent wa pikipiki za Honda, magari ya Isuzu na Honda. Kwa hapa amefanya na anaendelea kufanya biashara na serikali yetu - kama kawaida lazima hapa 10% zinatembea!

Enzi za JAPANESE IMPORT SUPPORT FUND, huyu kijana akishirikiana na marehemu babake walisajiri makampuni mengi ambayo yalichota mipesa hiyo enzi zile Yona akiwa waziri wa pesa. Wakati wa funds hizo wabunge na mawaziri karibia woote walichukua pesa hizo na kumuuzia Quality Garage kwa sababu hawakuwa na cash cover kwa ajili ya fund hizo ya 30%.

Hawa waheshimiwa walikuwa wanamfuata hadi ofisini kwake kuomba pesa.....

Kifupi huyu kijana kawaweka mfukoni watu wengi serikalini kuna tetesi kamlipia katibu Mkuu wa CCM deni la nyumba aliyonunua serikalini pia alimnunulia Land Cruiser wakati ule wa mgogoro wa Manji na Waisilamu kuhusu kiwanja cha pale Chang'ombe Kibasila.

Kama kawaida viongozi wa kiTZ wanahusudu mno wahindi..
 
Hawa watu ni wa kuwaangalia sana wanajikaribisha kwa viongozi matokeo yake ni kutuibia pesa zetu halafu wanakwenda kuinvest nje ya nchi na kuacha waTZ wakiwa masikini.
 
Hawa watu ni wa kuwaangalia sana wanajikaribisha kwa viongozi matokeo yake ni kutuibia pesa zetu halafu wanakwenda kuinvest nje ya nchi na kuacha waTZ wakiwa masikini.

Enzi za TANU na CCM ya Nyerere mafisadi kama hawa walikuwa hawakisogelei chama wala viongozi ndani ya chama au serikali. Sasa hivi viongozi wa chama na siri kali wanapigana vikumbo kwa wahidi hawa kwenda kuchukua mabulungutu kila kukicha.
 
Muhindi hata siku moja hawezi kutumia pesa yake kwa ajili ya mweusi.Ukiona anatumia pesa ujue au atapata nyingi zaidi kwa kufanya hivyo au kishaiba serikalini na ndio anatumia.
Majority ya wahindi matajiri hapa ni wezi.
Mtu kama Rostam(sio muhindi),nani alimjua kama tajiri huko nyuma?Kampuni ya Caspian ni ya baba yake ambaye tayari karudi kwao Iran,na kama ni tajiri halali kwa nini kwenye kila dili ya wizi yumo?Jiitu Patel nae hivyohivyo....na hawa wote wanajua weakness ya CCM ni pesa,hapo utapata ubunge au chochote unachotoka.CCM ni kama kinyesi kisichokauka,always attracting flies! Na kama wasipopata njia ya kuwa na viongozi kama ilivyo zamani
wataendelea kuzongwa na nzi tu.Ni rahisi sana kwa mtu mwenye pesa kujipenyeza ndani ya CCM.Mtu kama Masha mfano,alikuwa upinzani kwenye uchaguzi wa 2000,angekuwa ni mlalahoi unadhani angepata huo uwaziri,achilia mbali ubunge?Kuna watu wamezaliwa na kuzeekea CCM,tena wasomi,lakini wanaonekana ni nuksi. Na huo ni mfano mmoja tu,iko mingi sana.
Ingawa sasa zinaonekana dalili za kuporomoka tabia ya kulindana...mfano ni juzi tu Philip Marmo alisema hakuna kiongozi wa CCM aliyekiuka maadili,then baadae PM anasema kashtushwa kusikia pesa alizonazo Chenge.Zamani,PM angesema kitu kama 'hilo suala labda liko mikononi mwa vyombo vya sheria na yeye hawezi ku comment',lakini tunaona sasa kidogo hali imeanza kubadilika.
Hawa wakina Ruhinda,wote walikuwa ni untouchables,they could have even shut us down wakati huo,not now.The cookie has crumbled,and i hope zile fununu kuwa kuna kundi la wafanyabiashara within CCM wanaotaka kuanzisha CCM yao ni kweli,maana CCM tunayo,na tutakuwa nayo kwa muda mrefu sana...ni vizuri kukawa na CCM ya mafisadi na CCM halisi.
 
CCM Halisi aka CCM-Z (Zalendo)......patamu hapa!
 
Wakuu habari za leo,
Jana Baada ya kutolewa kwa shauri kati ya madai ya Manji kukashifiwa na ITV katika moja ya taarifa zake za habari,ila ITV wameshinda kwa kutokuonekana na hatia yoyote kutokana na shauri hilo.
Baada ya Kutoka ndani ,Mzee mengi akihojiwa na waandishi wa habari,aliiuliza watanzania,Hiki Kiburi na ujasiri aliona Manji nani anampa?Mzee mengi alisema "antoka wapi nguvu hizi?".hii ni baada ya Manji kukosekana pale katika siku ya kutoa maamuzi ,hii mzee Mengi aliona kama ni dharau kubwa kwake.Manji aliwakilishwa na wakili wake.

Najua mna mambo mengi ila naomba tujibu swali la Mzee Mengi,Je Manji anatoa wapi kiburi cha na namna hii na ujasiri mkubwa kiasi hiki??nani anampa?nani yuko juu yake??

Mkuu,

Kiburi cha Manji tumempa sisi wenyewe, Waswahili ambao kupitia ufisadi
tumemwachia achume atakavyo. Utajiri uliokithiri kupitia njia za mkato huwa unaongeza kiburi mno.

Tuliwalaumu mababu zetu kuuza nchi kwa pipi na gobore? Hawa viongozi wetu wa sasa wanauza nchi kwa bei poa kuliko hata wale mababu zetu.

Mtu kama Manji, kwanini asidharau Watanzania baada ya kuona yeye anatajirika kwa cost ya wananchi wetu wengi?

Hatuna wa kumlaumu zaidi ya ndugu zetu ambao wamejifanya vikaragosi vya Manji shauri ya pipi anazotoa.
 
Waheshimiwa sana heshima yenu.

Ninajua mjadala huu wa Kiburi cha Manji ni muhimu sana ingawaje sioni ni kwa jinsi gani wanaJF watajikuta wakishiriki kwa pamoja na kwa wingi zaidi ili kinachosababisha tatizo katika kiburi chake kiweze kung'olewa.

Ninakumbuka enzi za mvutano mkubwa baina ya hawa watu wawili Manji na Mengi kuhusu vyombo vya IPP Media kuandika kuhusu ufisadi wa huyo mkubwa kwenye mikataba ya vichekesho iliyowagharimu wafanyakazi wa Tanzania wanaochangia mifuko ya PSPF na NSSF.

Hasira ya Manji dhidi ya Mengi ilikuwa kwa nini vyombo vyake vilithubutu kuandika habari iliyohusu dhuluma na ufisadi ambao alikuwa akiifanyia nchi ya Tanzania.

Ninakumbuka hata pale alipojikuta kwenye hoja nyingine ya aina yake iliyomhusisha Mengi huyo huyo na Mhe. Adam Malima mbunge wa Mkuranga. Kulitokea maneno ambayo Mbunge wa Moshi Mjini Mhe. Philemon Ndesamburo aliona kwa heshima ya bunge si busara kuyanyamazia. Maneno haya yalitolewa kwa Mhe. Ndesamburo na aliyekuwa Waziri Mkuu wakati ule Mhe. Edward Ngoyai Lowasa. Katika maneno yake Lowasa alimwambia Ndesamburo kuwa Manji ametoa rushwa kubwa kwa wajumbe wa kamati ya Maadili ya bunge ili kupindisha haki na kuhakikisha kuwa Mengi analazimika kumwomba radhi Mhe. Malima na bunge. Mhe. Lowasa alikuwa na nia ya kumshawishi Ndesamburo naye aridhie kuwa Mengi asulubiwe kwa kosa la kuwapa changamoto wakubwa.

Ndesamburo alipotoka na hoja hiyo kwa ujasiri na uzalendo mkubwa alirudi katika vikao vya kamati ya bunge na kutaka apewe taarifa za kugawiwa kwa rushwa kulikofanywa na Yusuf Manji kama alivyoambiwa an Lowasa (WM) Mheshimiwa Ndesamburo alikataa kila mpango wa kumsuluhisha ama kumpoza. Wakati viongozi wengine wa serikali na bunge wakihaha kumbembeleza Ndesamburo Manji aliandika TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI ikiwa na kichwa kilichosomeka NDESAMBURO UNA NINI NA MIMI?
Ndani ya habari hiyo kulisheheni vijembe vya kutosha vyenye dharau kubwa kwa mtu mzima kama Ndesamburo ambaye Yusuf Manji ni mtoto wake wa kumzaa.

Wengi walihoji pia nguvu za Manji hapa zinatokana na nini?

kwa taarifa yenu niwahakikishie tu bila wasiwasi wowote. Manji Ni mmoja kati ya wafadhili kumi bora wa CCM. Wafadhili wa CCM ndiyo waamuzi wa nchi ipelekwe wapi. Hawa wana nguvu juu ya sheria na kila wakati wanalindwa sana na viongozi wa chama na serikali. Wamehodhi sehemu kubwa ya biashara za serikali. Ndio wanaoshinda tenda nyingi serikalini.

Niwahakikishie wanaJF kuwa serikali ya CCM haiwezi kuacha kukumbatia watu (mafisadi) wanaokifadhili chama. Hilo naona lisiwasumbue sana vichwa vyenu. Hapa mtu anayetaka kutoa dawa ya kukwepesha udhalilishaji huu wa utanzania wetu basi aishinikize serikali ya CCM ikubali na kuendesha mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya inayofaa mazingira ya siasa ya vyama vingi.

Kinachoniumiza kichwa mimi ni habari za leo hii kuwa eti CCM wamemkana Chenge kwamba si mwenzao na utajiri wake haukihusu chama. CCM ni chama chenye kuonyesha udhaifu mkubwa mbele ya wahindi. Ufisadi ukimkuta Rostam hakamatwi wala kukemewa. Chama kinajitolea kufa kupona kumlinda Rostam kwa kuwa ni mhindi ingawaje cheo chake ni mbunge wa kawaida tu. Lakini kinashindwa kumlinda Lowasa aliyekuwa na cheo cha Uwaziri Mkuu. Tatizo ni nini. Ufisadi wa Lowasa katika Richmond hauwezi kutenganishwa na Rostam. Hayo ndo yametokea leo kumhusu Mheshimiwa sana Chenge. Yeye si Mhindi CCM imeshamkana tayari.

Hii ndiyo kiburi ya Manji. manji anajua wazi kuwa kwanza yeye ni mfadili wa CCM na viongozi wa CCM kibinafsi. Kwa hiyo ulinzi wa kawaida na kukumbatiwa na viongozi wa chama na serikali ni haki yake ya msingi kabisa katika siasa za kipuuzi zinazoendeshwa na CCM hapa Tanzania. Pili Manji anajijua kuwa yeye ni Mhindi na hivyo lazima atapata ulinzi wa ziada ambao wahindi hupewa pale inapobainika kuwa wameboronga.
KWA HAYA HANA SABABU YOYOTE YA KUMHOFIA MTU YEYOTE HAPA TANZANIA NA WALA HAIHITAJI KUWA NA TAHADHARI.

Kwaherini
 
Back
Top Bottom