Kwasababu yeye ndio "starring" wenu anayewaburuza, kila atakalosema vidampa kama wewe mnaitikia ameen!
Kama unahoja eleza sasa unachukia nini mtu akimfagilia mchangiaji jemedari wa JF? au una lako jambo??
Kwasababu yeye ndio "starring" wenu anayewaburuza, kila atakalosema vidampa kama wewe mnaitikia ameen!
Kila ulichosema ni kweli tupu...lazima utakuwa upo fit sana kichwani!! Haya kakojoe ukalale, muda wa kucheza gololi umekwisha!
Hujui kwenye civil case mahakama haina uwezo wakumuita shahidi au kuita ushahidi wowote na mtu akikataa kuitwa hakuna adhabu yoyote huwa wanaenda kwa hiari?
Tulia wewe mshauri wa mengi, NGOMA bado mbichi, usianze kutafuta wafuasi wako hapa watu tuko DEEP kufuatilia mchezo, hatulali mpaka tujue mwisho wa hili GAME, TUNATAKA MBEGU ZETU ZIRUDI tena na matunda (INTEREST).........
Hata Mengi naye katika kesi hii ni kama anazunguka mbuyu. Kwa nini asitafute ushahidi dhidi ya tuhuma za ufisadi za RA na kufungua mashtaka ili kesi iwe kweli ya kiini - ufisadi na si hizi za kutaka kusafishwa?
Ninavyojua mtu baki anaweza kuomba kibali cha kufungua kesi ya jinai kama anaona jamhuri inadolola. Hili limefanyika? Kuomba tu kufungua mashtaka dhidi ya Rostam?
Amandla...........
Kumbe vilaza mko wengi hapa. posts in the 60's of this thread are posts no. 60,61,62......69.
Issue iko wazi mahakama iko juu ya PCCB na inajitegemea hivyo iwe PCCB wamemaliza uchunguzi au la hiyo haiusiani na kesi iliyopelekwa mahakamani. Aliyeshitakiwa atatakiwa kujitetea na kutaja mashaidi wake hivyo yeye atakuwa na ushaidi kwani hata hivyo vitu alivyowakilisha PCCB anaweza kuleta kama ushaidi wake. Ila sasa kama alifanya usanii kama kawaida yao kwenye serious issues then ameumia labda watumie njia za panya.
Jamani, Nikifuatilia mambo haya nafikia wakati najiuliza mambo mabaya juu ya RA.
Huyu mtu ana elimu ya kiwango gani??
Hawezi pia kuwatumia waliokwenda shule kuliko yeye? Au ni jeuri ya uhusiano na wana-siasa maana naona kama hata PCCB wameingia na kupokea ushahidi kwa sherehe za kamera na microphone.
Kwasababu yeye ndio "starring" wenu anayewaburuza, kila atakalosema vidampa kama wewe mnaitikia ameen!
Ingawa nilikosa mengi sana kuhusiana na ugomvi huu baina ya Mengi na Rostam, ninadhani kuwa wote wana makosa yao ingawa kwa viwango tofauti. Vile vile yule mama Simba naye kama kiongozi wa serikali alijiingiza katika malumbano yasiyomhusu.
(1) Mengi alipotoa ile orodha ya mafisadi, inawezekana kuwa alifanya makosa kutegemeana na lugha aliyotumia katika kuwataja. Kama alisema kuwa watu wale wana hatia ya ufisadi basi alikosea na ni haki ya walituhumiwa kumfungulia mashitaka ya kuchafuliwa majina yao. Ila kama aliwataja kwa kunukuu taarifa zilizopo na kutumia taarifa hizo kutoa hisia zake kuwa wanaweza kuwa ni mafisadi, na wala si hakuwahukumu, basi Mengi is clean.
(2)Rostam anaweza kuwa na makosa mengi kidogo kuliko Mengi. Kosa la kwana ni lile la kutoa hadharani taarifa za account za benki za makampuni ya Mengi (kama alifanya hivyo kweli) bila ridhaa ya mwenyewe au kibali cha mahakama kufanya hivyo linaweza kuwa ni kosa. Kosa la pili ni kutoa tuhumu za madeni na kuhukumu kuwa Mengi alikataa kulipa madeni yake hayo kinyume cha ukweli pia ni makosa, hasa baada ya Mengi kuonyesha ushahidi kuwa tuhuma hizo ni za uwongo. Kosa la tatu na baya zaidi ni lile la kupeleka nyaraka hizo TAKUKURU huku akijua kuwa hata kama ni kweli Mengi alikopa na hakulipa madeni yaho, hilo siyo kosa la rushwa na haliko kwenye mamlaka ya TAKUKURU. Chombo chenye haki ya kumshitaki Mengi ni Benki iliomkopesha Mengi wala si DPP wala TAKUKURU wala mwanasheria wa Serikali.
(3)Kwa vile ugomvi kati ya Mengi na Rostam ni baina ya watu wazima wawili wenye akili timamu, mama Simba kama kiongozi wa serikali hakuwa na sababu ya kuuingilia kabla wagonvi wenyewe hawajaomba msaada wa serikali. Na wala nafasi yake ya uongozi haimpi mamlaka ya kuingilia swala hilo.
.............karibuni mchwa na nguchiro.
Huyu Rostam anafikiria yeye nani au ana nguvu gani against mitungo ya FITNA ambayo tayari ilikwisha andaliwa kama chambo kwenye ndoana..Hivi kweli anafikiria Mengi ni mjinga aliyeibuka toka usingizini na kutoa maneno yale!..