Mengi atunukiwa tuzo za kimataifa za kusaidia jamii

anastahili,hana magumashi katika biashara zake ndio maana anaweza kusimama mbele ya uma na kukiri kua cash anayo,tofauti na hao wengine wezi ,wakwepa kodi na wauzaji wa bidhaa feki.bravo mzee MENGI
 
Tafadhalini bandugu niambieni, hizi tuzo zinatumikaga wapi?
labda nitapata hamu ya kuisalandia tuzo moja.
 
Kwa matendo yake ambayo sisi watz wakawaida tunayaona, huyu mzee anastaili tuzo za namna hiyo. Mungu azidi kumbariki kwa wema wake....
 
"MATAJIRI wanapaswa kutambua kuwa mwisho wa maisha ukifika, hawatakumbukwa kwa utajiri wala mali walizonazo bali kwa matendo waliyoyafanya kwenye jamii kupitia utajiri wao.


"Duniani patakuwa mahala pazuri kuishi kama wote matajiri na maskini watakuwa na utamaduni wa kusaidiana."


Hii ni kauli ya Mwenyekiti wa makampuni ya IPP na mfanyabiashara maarufu nchini, Dk. Reginald Mengi, mara baada ya kutunukiwa tuzo mbili za kimataifa ambazo ni mara ya kwanza kutolewa kwa Mwafrika.


Hafla ya kutunukiwa tuzo hizo iliyofanyika Jumamosi iliyopita katika Hoteli ya Serena, iliweka historia mpya katika maisha ya mfanyabiashara huyo ambaye ametunukiwa tuzo hizo kutokana na moyo wake wa kusaidia watu hasa wenye ulemavu na wasiojiweza.
Tuzo hizo ambazo ni za kwanza kutolewa kwa Mwafrika ni pamoja na tuzo ya Uongozi na Utu inayotolewa na taasisi ya Umoja wa Mataifa (UN), Global 2000(2010).


Tuzo nyingine iliyotolewa kwa Dk. Mengi ni tuzo ya mafanikio katika maisha ya mwaka 2010- 2011, inayotolewa na mashirika binafsi ya Umoja wa Mataifa (UN-NGO's).


Kwa kupata tuzo hizo, Dk. Mengi si tu kwamba amevunja rekodi kwa kuwa Mwafrika wa kwanza kutunukiwa, bali pia ni mara ya kwanza kwa hafla ya kutunuku tuzo hiyo kufanyika barani Afrika, tena nchini Tanzania kwani kwa kawaida hufanyika katika makao makuu ya UN, New York, Marekani.


Dk. Mengi ambaye alizaliwa kwenye familia maskini, alitunukiwa tuzo hizo katika hafla maalumu iliyofanyika katika Hoteli ya Serena na kuhudhuriwa na watu mbalimbali mashuhuri wakiwamo, viongozi wa dini na baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini, huku Jaji Mkuu Athuman Chande akiwa mgeni rasmi.


Wengi waliopata nafasi ya kuzungumza katika hafla hiyo iliyofana kutokana na kupambwa na burudani ya vikundi mbalimbali, walimwelezea Mengi katika mitazamo tofauti.


Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, Alberic Kacou, alisema Dk. Mengi amekuwa si msaada tu kwa Watanzania bali kwa watu wengi duniani na kuongeza kuwa tuzo mbalimbali alizowahi kupata kama ile ya Martin ya Luther King aliyopewa na Ubalozi wa Marekani ni mifano michache tu inayodhihirisha kwamba ni mtu mpenda watu, aliyejitoa kusaidia jamii.


"Mengi amesaidia watu wengi hapa Tanzania, lakini amevuka mipaka na kwenda kusaidia hata watu wa nje ya nchi, Mengi amefanya mengi na anastahili tuzo ya 2010 United Nation Global Leadership," alisema.


Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Nchini), (CTI), Felix Mosha alisema licha ya ukweli kuwa tuzo hizo amepewa Dk. Mengi lakini zimeleta heshima kubwa kwa taifa.


Alimuelezea Dk. Mengi kuwa ni mtu anayetumia sehemu kubwa ya mali yake kusaidia wenye shida na wakati wote amekuwa akiwasisitizia wenye uwezo kusaidia makundi yasiyo na uwezo kama walemavu.


Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Balozi Juma Mwapachu, alisema walikutana kwa mara ya kwanza na Mengi mwaka 1980 na akawa mshauri wake mzuri katika mambo mengi.


Alisema Dk. Mengi amekuwa mtu asiyekata tamaa na anayependa kukabiliana na changamoto yoyote anayokumbana nayo na kwamba hiyo ndiyo imemfikisha hapo alipo.


"Regi ni mtu wa kutekeleza kile anachoamini na amefika hapo alipo kwa kujiamini na kwa kufanya kazi kwa bidii," alisema Balozi Mwapachu.


Mbunge wa Maswa, John Shibuda (CHADEMA), ambaye alikuwa mmoja wa wabunge waliohudhuria hafla hiyo, alimmwangia sifa Mengi kutokana na moyo wake wa kusaidia makundi mbalimbali ya jamii bila ubaguzi.


Akielezea namna anavyomfahamu baba yake, mtoto wa kiume wa Dk. Mengi, Abdiel Mengi, alisema: "Mzee Mengi ni baba yangu rafiki yangu, mjasiriamali, pia ni bosi wangu na wakati mwingine ni mwanafunzi wangu."


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kimataifa ya Global 2000(2010), Dk. William Morris, alisema tuzo hizo zimewahi kutolewa kwa mchezaji wa kimataifa wa Liberia, George Weah na Sir Roger Moore.


Akizungumzia uteuzi wa tuzo hiyo, Dk. Morris alisema majina ya washiriki hupendekezwa na taasisi na mashirika 10,000 ya UN kwa siri na majina ya mwisho matatu, hupigiwa kura na Baraza la Umoja wa Mataifa kupitia mashirika na taasisi 10,000 za umoja huo.
Alisema jina la Dk. Mengi lilipendekezwa tangu mwaka 2008, 2009, lakini hakuweza kuchaguliwa kwani wakati huo alikuwa hajajulikana sana.


"Mwaka 2010 jina lake liliingizwa tena, tukaanza kumfuatilia shughuli zake na mambo aliyofanya kwenye jamii, hatukuamini, tumekusanya mikanda ya video yote ya shughuli alizofanya, hakika tumeshangazwa, ni mtu wa aina yake na safari hii alipigiwa kura ya ushindi wa asilimia 80," alisema Dk. Morris.


Akieleza sababu za kuchelewa kutoa tuzo hiyo, Dk. Morris alisema hata baada ya ushindi, UN iliandika barua tatu mwaka 2010 kumjulisha, lakini hakuzijibu na walilazimika kusafiri kuja nchini kumtafuta, hawakuweza kumpata.


"Mwaka huu nimetumwa tena kumtafuta, nikasema siwezi kuendelea kukaa na tuzo hizo wakati mwenyewe yupo na kama amefariki dunia, ni bora tujue. Basi nikaja, nimemtafuta kwa miezi miwili na hatimaye nimempata na sasa tunafurahi kumkabidhi tuzo hizo," alisema.
 
Back
Top Bottom