Kwa kweli... Huyu mzee anaheshimika lakini amekuwa na tabia fulani ya kutuweka Watanzania upande wake kila akizungumzia matatizo yake na wafanyabiashara wenzake!!! Nakumbuka hata wakati wamepelekana mahakamani na Manji alipohojiwa alikuwa anajiunganisha na Watz kana kwamba tunajua bifu lao. Nimemfuatila kwa muda mrefu ni mtu anayetafuta public sympath siku zote.
Itabidi naye achunguzwe, mbona kodi alizokwepa watu wanaelewa na hawasemi? au tuanike uozo wake hapa Jf? Nadhani hajawa msafi kiasi cha kujiunganisha na watanzania kana kwamba tuna vita moja na yeye!
Sio kweli hata kidogo!!!! Na wewe kwa maana moja au nyingine ni.....
...bora ya Mengi ambaye practically kutokana na biashara zake amesaidia familia nyingi sana through ajira na analipa kodi na kutuletea services nyingi tuu,impact ya Mengi ni kwa maelfu for the better....akifilisika msifikiri he'll go down by himself ni wengi watahangaika sana,i respect mengi kwa anayofanya ingawaje naona mmeanza kumponda eti its all publicity,waulizeni ambao watoto wao wanakula na kwenda shule kwa ajira za mengi ndio mtaelewa,hope tungekuwa na Mengi wengine maelfu tungeendelea sana...heshima mbele kwa watu kama kina Mengi sio wanasiasa uchwara wa CCM ambao ni kulinda maslahi yao tuu na matumbo yao!
Kumbe sikuwa peke yangu......!
Au angalau angetujulisha hayo waliyomfanyia hata aseme wanataka kuvuruga amani then we (Tanzanians) ndo tujaji kama ni mbinu za kuvuruga amani au ni personal issues zao yeye na wao. Kuna kilichofichika hapa
Sijui pengine amekisema sikukisikia. mimi huwaga nabadilisha chanel mara awekwapo huyu maana akianza kuhutubia basi wimbo unaanza chanel 5 na kuisha bado akiongea..... anabore sometimes.!
Nitamtambua Mengi kuwa anasaidia wananchi wakawaida kama atafanya kitu kinachoitwa au kuepuka 'Nepotism'. Kwani misaada yake si anaielekeza kasikazini maeneo mengine hawajwahi hata kunusu senti ya Mengi. Wakuu niambieni kanda ya Magharibi wamenufaika nini na utajiri wa Mengi? yeye aendelee kufaidisha maeneo fulani fulani kwa sababu anazozijua yeye. Kwa hilo ameteleza
Wengi wanajua ndiko aelekeako hasa haya mambo ya kijipublicise kwa kila afanyanyacho kwa jamii
Mzee Mengi ni chui aliejivisha ngozi ya kondoo, ni silent killer wa wafanyaiasara wenzie kila akizidiwa kete hutumia vyombo vyake kuwamaliza wenzie na haraka anakimbilia kwa wananci kuomba huruma yao.
wengi wanajua ndiko aelekeako hasa haya mambo ya kijipublicise kwa kila afanyanyacho kwa jamii
Mengi Anafanya Biashara Kwa Misingi Ya Kibepari...Mwenye Kuweza Kushindana Naye Ajaribu Kama Walivyofanya Clouds FM, Wao Wameweza; Kama Wengine Hawawezi Wanaweza Pia Kufanya Biashara Zingine Tofauti Na Zile Anazofanya Yeye...Mbona Biashara Zipo Nyingi Tuuuu.
Sawa kwanini wakizidiana kete anawakimbilia wananchi?
Kwa Sababu "Amewekeza" Kwa Namna Moja ama Nyingine Kwa Wananchi Na Anajua Fika Kuwa Wananchi Watamuonea Huruma...Hebu Baric Gold Au Mohamed Intreprise Walalamike Kwa Wananchi Halafu Tuone Kama Kuna Mtanzania Yoyote Atakayetega Sikio Lake Kusikiliza.
"Amewekeza" kivipi? kuna gawiwo la dividends kwa kila mwaka kwa "wananchi" au kivipi?