Mengi adai Polisi wahusika kutaka kumbambikizia mwanae madawa!

babayah67

JF-Expert Member
Mar 28, 2008
493
79

Jamani nimesikia kutoka taarifa ya habari ya hivi sasa (saa mbili usiku Tz time) ya Radio One Mzee Mengi akilalamika kuwa Polisi wakishirikiana na wafanyakazi wa JKN Airport walimtegea mwanae madawa ya kulevya.

Mengi ameenda mbali zaidi kwa kuwataja kwa majina hao askari waliohusika na akasema kuwa wametumwa na mmoja wa mafisadi. Pia Mengi amewataka hao askari kwenda mahakamani kama wanaona wamekashifiwa.
 
Last edited by a moderator:
namuona hapa reginald mengi akilibwatukia jeshi la polisi live bila chenga kupitia itv
 
Jamani nimesikia kutoka taarifa ya habari ya hivi sasa (saa mbili usiku Tz time) ya Radio One Mzee Mengi akilalamika kuwa Polisi wakishirikiana na wafanyakazi wa JKN Airport walimtegea mwanae madawa ya kulevya.

Mengi ameenda mbali zaidi kwa kuwataja kwa majina hao askari waliohusika na akasema kuwa wametumwa na mmoja wa mafisadi. Pia Mengi amewataka hao askari kwenda mahakamani kama wanaona wamekashifiwa.

Sasa mleta hoja kwa nini umeiweka hii habarikwenye siasa? Unataka watu waijadili kisiasa Tuwe tunaangalia uzito wa thread na kuiweka sehemu sahihi.
 
hii itakuwa kwa vile Mzee Mengi amewasaidia Chadema na CCM wakabumburuka sio? wanaamua kumfanyizia! unajua hata ITV sasa inaonyesha Chadema news kiuwazi sasa! naona imewauzi wakuu sasa huu ni mtego wa kuifunga ITV!
 
kweli cha mtu mavi , ni muda mrefu sijaangalia itv lakini leo imenibore how can some one talk for more than 10 min just for his boy . Utaifa uko wapi ? Where we now kwanini asitueleze kuhusu uchaguzi morever anawasifia polisi na kuwaponda . Inchi hii .............. Am bored
 
Wadau, nimeikutia hii habari katikati kwenye tv, Mengi akizungumzia kuwa mtoto wake alipangiwa kubambikizwa madawa ya kulevya, akiwa safarini kuelekea India........mwenye habari kamili atujuze tafadhali
 
kweli cha mtu mavi , ni muda mrefu sijaangalia itv lakini leo imenibore how can some one talk for more than 10 min just for his boy . Utaifa uko wapi ? Where we now kwanini asitueleze kuhusu uchaguzi morever anawasifia polisi na kuwaponda . Inchi hii .............. Am bored

Ungesema alichozungumza halafu tungepima kama kina worth 10 minutes na siyo kuja tu hapa na kupiga blah blah
 
Bora ya mkute maana amezidi kuwa beba hao mafisadi... hivi hajui kuwa mafisadi hawabebeki?
 
Nimeangalia TV kama anachosema Mengi kina Ukweli basi alikuwa anastahili hata kutumia dakika 20
 
Millioni 300 alizowapa CHADEMA zimewauma sana CCM...tatizo MANJI anadhani kila BIFU against CCM anaweza kulinunua kisa serikali inampa favour za tenda...sasa atakaa,mtandao wa CHADEMA ndani ya TISS/Police ni mkubwa sana....
 
kwani ulikuwa hujui kama habari yoyote inayomhusu mengi ITV huwa wanailezea sana mpaka wanaishiwa maneno
hujalazimishwa kuangalia ITV, ni televisheni binafsi unaweza fungulia TBC inayomuonyesha JK siku nzima kwa gharama ya kodi yako kama at all unalipa kodi!!! Pambaf!
 
Millioni 300 alizowapa CHADEMA zimewauma sana CCM...tatizo MANJI anadhani kila BIFU against CCM anaweza kulinunua kisa serikali inampa favour za tenda...sasa atakaa,mtandao wa CHADEMA ndani ya TISS/Police ni mkubwa sana....
Muiran yule anawafanya Wadanganyika wajinga! tuone nani ataleta fujo nchi hii!
 
hii mupya jamani. kasema mafisadi papa wanahusika so ni rostam na lowassa. mengi karibu chadema.
 
kweli cha mtu mavi , ni muda mrefu sijaangalia itv lakini leo imenibore how can some one talk for more than 10 min just for his boy . Utaifa uko wapi ? Where we now kwanini asitueleze kuhusu uchaguzi morever anawasifia polisi na kuwaponda . Inchi hii .............. Am bored

jamani si mali yake?....ana uhuru wa kuongea chochote mradi havunji sheria
 
Hilo ni dili la CCM. CCM wanawachikia watanzania kuliko mafisadi. Mengi anapinga mafisadi kwa nguvu zote.
 
Nimeangalia TV kama anachosema Mengi kina Ukweli basi alikuwa anastahili hata kutumia dakika 20

Nimefurahia ujasiri wake wa kuwataja hao Mafisadi na na hakika kuwa kama hana ushahidi asingeweza kusema hayo. Pili, ni nani asiyejua umafia wa Polisi na ushirikano wao na Wafanyabiashara haramu?

Kila siku wanyonge wanaumizwa kwa kubabimbikiwa kesi na hakuna wa kuwatetea lakini kwa hili ni nafasi yetu kujua uovu na uhalifu tunaofanyiwa na dola.

Kazi iko kwa serikali na Wazirfi Masha, tuone kama atachukua hatua gani maana wamezoea kubebwa na Polisi nao sasa tuone kama watawabeba hao Pilisi waliohusika pamoja na huyo Fisadi Papa aliyehifadhiwa na Mebi.
 
Mmiliki wa IPP Ndugu Reginal Mengi amwalipua maafisa kadhaa wa vyeo vya juu kwa kupokea mulungula ili kumbambikiza mwanae madawa ya kulevya na alikuwa asafiri kwenda India tarehe 26/9/2010.

Maafisa hao wa vyeo vikubwa amesema wamelipwa na "tajiri" mwenye ofisi Nyerere Rd na wote waliahidiwa $40,000 kila mmoja na wamekwisha pokea nusu ya kiasi hicho ($20,000) kila mmoja.

Maafisa hao ni Zonal Crimes OfficerNd Mkumbo, Ofisa wa kuzuia mihadhatrati, Nd Nzowa na ofisa mmoja wa Interpol.

Vile vile kuna vijana wa kampunu moja ya simu na wengine pale DSM Airport waliopewa kila mmoja Tshs 15 mil.

Hii taarifa ni kadri ya HABARI za saa mbili jioni leo 12/10/2010.

Mengi amwaomba hawa maofisa wajiuzulu na amewachallenge wamfungulie mashtaka ya kuwa chafua majina yao.

Sasa wananchi lazima watajiuliza hivi majambazi wakubwa wako upande gani? na imani yetu kwa polisi baada ya sakata la Zombe itakuwa wapi?
 
Back
Top Bottom