Meneja wa TANROADS nchini asema daraja la Kiyegeya limekatika kwa uchakavu. Je, Waziri Mkuu kumuondoa Meneja TANROADS-Morogoro alimuonea?

Daraja la mto Simiyu, Magu, lipo hatarini, daraja la mto Rubana, Bunda, linatishia .......
Ni madaraja mengi tu na serikali inajua, lakini pesa wapi? ... wana siasa wamekaa tu kama tai wakisuburi ajali watoe wataalam wetu kafara!
WANASIASA EEH, CHONDE CHONDE, MTATUMALIZIA WATAALAM!
 
Life Span ni 100 yrs lakini kuna kama miaka ,40 toka lijengwe je hapo unamlaumu vipi mtaalam? Suala la kukagua hata kama lipo je anavifaa vya kuonesha ubovu wa daraja au ndo anakagua kwa kuchungulia kwa macho kama polisi wa usalama barabarani wanavyokagua magari?
Yaani kurudishia calvart sikutatu kweli? Mbona jw wameenda pale masaa manne daraja likapitika
 
Serikalini kuna matatizo mengi hasa ajira za serikali kuna vita kali sana huko ndani ukiwaona wahurumie tu kuna mengi mno.kugombea vyeo,,kuchongeana uongo kwa wakubwa,kuzushiana na mitego mingi.
 
Mfugale amekua! Maana anachosema wala hatumuelewi! Km madaraja yamezeeka wao km wao wamechukua hatua gani sasa kabla ya kuleta shida?

We mzee umezeeka sasa.
 
Yaani kurudishia calvart sikutatu kweli? Mbona jw wameenda pale masaa manne daraja likapitika
Kazi waliyokuta imeishafanywa ndogo?
..... isitoshe, hivi unafikiri kwa vifaa maalum vya madaraja ya dharura ya medani, ambavyo havipo Tanroads, kwanini kazi isiende 'SHUTA'!
 
Kumbe ikitokea ajali mfano daraja livunjike magari yakiwa juu,watu wafe au kujeruhiwa itakuwa sawa sababu life span ya barabara imeshakwisha!!? This is possible only in Tanzania. Na watu wakifa tutasema"ni mpango wa Mungu"!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daraja la mto Simiyu, Magu, lipo hatarini, daraja la mto Rubana, Bunda, linatishia .......
Ni madaraja mengi tu na serikali inajua, lakini pesa wapi? ... wana siasa wamekaa tu kama tai wakisuburi ajali watoe wataalam wetu kafara!
WANASIASA EEH, CHONDE CHONDE, MTATUMALIZIA WATAALAM!
Huyo chapombe nae mtaalamu kweli? Siku tati hata Kijiji site hakipo
Mfugale amekua! Maana anachosema wala hatumuelewi! Km madaraja yamezeeka wao km wao wamechukua hatua gani sasa kabla ya kuleta shida?

We mzee umezeeka sasa.
Ni kweli Mfugale kazeeka Sana, Ni vyema akapumzika, tutaendelea kumuenzi kwa kazi nzuri
 
Barabara nyingi za lami zilijengwa miaka 40 zilizopita. Mfano hai ni barabara ya Mwanza - Simiyu border. Kwa ushauri tu barabara hii inatakiwa iwekewe tabaka mpya ya lami haraka iwezekanavyo.
 
PM anaweza kuwa alikuwa sahihi kbs, lkn kutokana na mazoea yetu ya kutotenga bajeti katika kufanya ukarabati wa miundo mbinu chakavu, je hata angekagua pesa ingetolewa ili kufanya ukarabati? Yani Kama tukijaribu kuangalia uhalisia, tunaona kweli hili lingetokea?


Ikiwa tu baadhi ya miradi mipya iwe mikubwa au midogo inasimama kwa kukosa pesa, ije kuwa hili la kutoa pesa ili kukatabati daraja ambalo lilikuwa likionekana liko vzr tu kabla ya kusombwa na maji hiyo juzi?

Sisi hatuna utaratibu madhubuti wa kumaintain assets au miradi mbalimbali tuliyoanzisha, yani inakuwa ikishajengwa ndy ntolee.

Embu chukua mfano wa mradi wa DART, yaani huu mradi hauna kbs muendelezo mzr, hv Sasa hakuna tena ule utaratibu wa kuscan tickets, vituo vyao vimeanza kuharibika baadhi ya maeneo, dustbins zile katika vituo zimen'golewa , utaratibu wa kutangaza vituo hakuna tena, achana na uozo ktk utaratibu wa kupakia abiria ktk mabasi yenyewe n.k lkn ajabu hakuna anaestuka hata kdg.

Nilitarajia ubunifu zaidi ktk huu mradi Kama kuweka Wi-Fi free ktk vituo na mabasi yake(kuonesha wanajali wateja wake), utaratibu mzr wa ticket, utaratibu mzr wa ratiba ya mabasi mfano kuwa na sign board au digital display device itakayoonesha bus la route gani litawasili baada ya muda gani, huu utaratibu wange u integrate na application maalum ambayo mtu hata kabla hayatoka nyumbani anaangalia kwa simu yake na anajua kbs bus atakalopanda litafika baada ya muda gani kituo husika.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
na pale jangwani panahitaji Meneja wa Tanroad DSM kukagua kila siku?

Ha Ha Haaaa!!!!!
Ktk. miradi ya ujenzi yenye aibu kubwa nchini ni Barabara inayopita Jangwani-Dar es Salaam, yakiwemo na majengo na miundombinu ya karakana ya BRT (Mwendokasi) yaliyo jengwa maeneo hayo.
 
Pamoja na hayo yote, kumeanzishwa utaratibu/ katabia kazuri kwa TANROAD/ TARURA kukata barabara kwa lengo la kuziba VIRAKA.
Hivyo VIRAKA vinakaa zaidi ya WIKI kuzibwa.
Unaleta USUMBUFU mkubwa barabarani.
Ukichangia na upuuzi wa Madereva wa DSM USUMBUFU unaongezeka dabali.
VIRAKA VIZIBWE MAPEMA/ MARAMOJA
 
Kama kweli walikua wanajua uhai wa makalavati si zaidi ya miaka 25 na anasema barabara imejengwa miaka 40 iliyopita walikua wanategemea nn sasa!? Waziri mkuu angeanza na huyohuyo Mfugale

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri Mkuu hakumuonea, kama meneja ni lazima akaguwe madaraja na barabara anazozi "manage" na yakarabatiwe kabla hayajaleta athari.

Sasa siku zote alijuwa ana "manage" nini mpaka daraja kubwa linaleta athari kubwa? Huyo alijuwa ana"manage" nini zaidi ya Ku"manage" tumbo lake tu?
Kilichokatika sio daraja lakini.
 
Back
Top Bottom