TANZIA Meneja wa TANROADS Mkoa wa DSM, Mhandisi Ngusa Julius afariki dunia

Jana site leo unahifadhiwa kwenye mafriji.
Endeleeni kumchekea kima, mtavuna mabua.
Corona inaua, huyo anayewaambia mwombeni Mungu huenda amechanjwa au anatembea na madaktari hata 10
 
kwa hiyo alivyopata nafuu ya changamoto akarudi kazini jana?kama ni kweli mbona hatari si angepumzika ajiweke sawa?
 
Kwa masikitiko, tena makubwa, nimepata habari za kifo cha Manager wa TANROADS mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Ngussa.

Alikuwa rafiki yangu zaidi ya miaka 20. Kwa kweli nimeumia.

Nimeongea naye last week kumpa pole ya changamoto....!

Mungu amuweke mahali pema.
Changamoto za upumuaji aisee sio mchezo. Pole sana kwa familia
 
Pia aliyewahi kuwa Katibu mkuu wizara ya kilimo na ushirika mohamed Muya tunamzika jioni hii hapa daslam. Poleni wote mliofikwa na misiba hii.
 
Kwa uzembe mulionao ktk hospitali zetu hakuna atakayepona. Hospitali ambazo hakuna hata mitungi ya oksijeni! Mukiulizwa eti mahitaji ni makubwa, hamkujua? Kwa wanaotimiza wajibu, watoto na vijana hawaathiriki kiasi hicho.

Serikali inabidi isitishe miradi yake mikubwa kwanza kuokoa nguvu kazi ya waTZ ,hizo fedha wanunue mitungi ya kutosha ili kuokoa wananchi wake.....Uhai haurudi ukiondoka ila fedha inatafutwa.
 
Salaama wana bodi. Kwa kweli changamoto ya kupumua, a.k.a Niumonia a.k.a Covid 19 siyo mchezo wa kitoto. Mhandisi Ngusa alipata changamoto ya kupumua ambapo alilazwa hospitali kwa muda wa siku 4 hivi akipata msaada wa kupumua kwa mashine ambapo alipata nafuu na kuruhusiwa lkn jana tarehe 16/2/2021 alizidiwa tena na kufariki akiwa njiani kwenda hospitali.

Tatizo hili ni kubwa sana ndugu zangu, wala haliathiri wazee tu, huyu Mhandisi alikuwa bado kijana tu in early forties na pneumoniae imemuondoa. Kwa vyovyote wapo wengi wanaoondoka kwa tatizo hili lkn hatupati taarifa kwa sababu hawajulikani au hawatangazwi.
Tuchukue tahadhari zote ndugu zangu.
 
Sorry mkuu ulikuwa jela? Mbona thread ipo tangia jana?
 
Back
Top Bottom