Meneja wa TANESCO kanda ya Mbagala inabidi atumbuliwe kila siku umeme unakatika saa 2 usiku na kurudi usiku wa saa 8 au 9

Katika hii serikali mpya wewe unatakiwa uwe wa kwanza kutumbuliwa

Kwa nini kilasiku umeme unakatika saa 2 au 3 na kurudi usiku wa saa 8 au 9 kama ni mgao kwa nini hamtoi taarifa

Na kama ni tatizo la kiufundi kwa nini litokee kila siku
Hama mbagala noma sana kule
 
Mi nipo maeneo ya shule ya secondary chamazi hili jambo Kwa kweli linakera sana

Juzi J5 umeme umekatika saa 3 usiku umerudi saa 11 alfajiri

Jana Umeme umekatika saa 2 usiku umerudi saa 9 usiku

Kama huu ni mgao basi ni wa aina yake ila mimi naamini sio mgao Ila kuna watu hawatimizi majukumu yao

Au kwa sababu muheshimiwa alisema amechoka kutumbua
 
Kuwa specific ni Mbagala sehemu gani?
Mi naishi karibu chamazi secondary katika hivi viwanja vya city lakini pia huwa hunakatika eneo kubwa maana ukitoka nje kuangalia unakuta giza limetanda eneo lote

Yani kila siku ndio mchezo wao kwa kweli imekuwa to much
 
Katika hii serikali mpya wewe unatakiwa uwe wa kwanza kutumbuliwa

Kwa nini kilasiku umeme unakatika saa 2 au 3 na kurudi usiku wa saa 8 au 9 kama ni mgao kwa nini hamtoi taarifa

Na kama ni tatizo la kiufundi kwa nini litokee kila siku
Umeme unazalishwa Mbagala au na yeye anapokea toka kituo (vituo) vinavyosambaza? Hajaletewa awaunganishie nini?
 
Meneja wa TANESCO Mbagala hazalishi umeme....

In short, nasikia hili tatizo lipo sehemu nyingi tu Dar es salaam licha ya porojo za kisiasa tunazoambiwa tangia Jiwe aingie madarakani, tatizo la umeme limeisha!!!

Few months ago nilienda kwa uncle na wao kituo chao wala sio Mbagala lakini nimefika hakuna umeme, na hadi nimetoka hakuna umeme na wakasema kwa miezi sasa hilo suala ni kawaida!!!
 
Ngoja nisimsemee huyo meneja maana muda wake wa utumishi unakaribia kufika tamati
Kwanini yeye ndo anazalisha umeme?! Sehemu nyingi tu Dar es salaama mara kwa mara huwa zinakatika umeme na wala sio Mbagala peke yake!!
 
Mda uliokatika mda ulio rudi
J3 saa 2 usiku. Saa 10 alfajiri
J4 saa 2:30 saa 9 usiku
J5 saa 3 usiku. Saa 10 alfajiri
Alhamisi saa 2. Saa 11 alfajiri
Leo ijumaa ,,,,,,,,,. Saa ,,,,,,,,

Kwa kweli mnatakiwa mtumbuliwe
 
Kwanini yeye ndo anazalisha umeme?! Sehemu nyingi tu Dar es salaama mara kwa mara huwa zinakatika umeme na wala sio Mbagala peke yake!!
Ndio maana nimesema kama kuna mgao ambao unapelekea kila siku kwetu umeme ukatike saa 2 au 3 usiku na kurudi usiku wa manane au alfajiri basi tupewe taarifa ili tujue
 
Huyu meneja bahati yake Muheshimiwa Magu amehamia Dodoma kama angekuwa bado yopo pale magogoni sahizi angekuwa ameshatumbuliwa
 
Kwani kuna tatizo la kimiundo mbinu au ndio kukomoana? Maana umeme unazalishwa wa kutosha kabisa
 
Back
Top Bottom